Siku ya Uhuru wa Eritrea

Siku ya Uhuru wa Eritrea

Imefasiriwa na/ Hasnaa Hosny
Imeharirwa na/ Mervat Sakr

Siku hii mwaka 1991, Vikosi vya Ukombozi wa Watu wa Eritrea (EPLF) viliingia katika mji mkuu wa Asmara, na kupata Uhuru wa nchi hiyo baada ya mapambano ya miaka 30 dhidi ya utawala wa kijeshi wa Ethiopia.

Tangu miaka ya themanini ya karne ya kumi na tisa, Eritrea imekuwa ikijulikana kama Eritrea ya Italia, kama ukoloni wa Italia, na baada ya kushindwa kwa Italia katika Vita vya Pili vya Dunia, Eritrea ilianguka chini ya udhibiti wa Uingereza hadi 1952. Kufuatia azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Eritrea ilielekea Uhuru na bunge la Eritrea na kipindi cha miaka 10 cha msaada kutoka Ethiopia. Hata hivyo, mwaka 1962, serikali ya Ethiopia ilifuta bunge la Eritrea na kuitwaa rasmi Eritrea. Chama cha Ukombozi wa watu wa Eritrea (EPLF) kiliendelea kupigania Uhuru hadi mapambano hayo ya silaha yalipofikia kilele cha Uhuru mnamo Mei 24, 1991, wakati Vikosi vya Ukombozi wa Watu wa Eritrea  vilipoingia mji mkuu, Asmara.

Kupitia historia, mahusiano ya Misri na Eritrean umekuwa na sifa ya ubora na udugu wa hali ya juu, na Misri ilikuwa na jukumu kubwa katika kusaidia na kuunga mkono mapinduzi ya Eritrea hadi kukamilika kwa mradi wa Uhuru wa kitaifa wa Eritrea, ambapo Kairo ilichukuliwa kama makao makuu ya kuanzishwa kwa Eritrean Liberation Front mnamo Julai 1960, na kabla ya kufungua kituo cha redio kwa viongozi wa mapinduzi mnamo mwaka 1954 huko Kairo kuwa jukwaa la kuchochea roho ya kitaifa kati ya Waeritrea. Baada ya mapinduzi, Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza kuiunga mkono na kuipatia aina mbalimbali za msaada wa kisiasa, vifaa na elimu, pamoja na makazi kwa viongozi wa kitaifa kama vile Idris Mohamed Adam na Ibrahim Sultan, na marudio kwa wanafunzi wa Eritrea.

Katika mapambano yote ya silaha, Misri ilidumisha mahusiano mazuri na makundi ya kimapinduzi ya Eritrea, na baada ya Ukombozi ilichangia gharama za kura ya maoni. Misri ilifanya ziara rasmi nchini Eritrea kupongeza tamko la Uhuru na kuweka misingi imara ya kuendeleza mahusiano na ushirikiano wa baadaye kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote. Diplomasia ya Misri pia ilikuwa na jukumu muhimu katika kutatua mgogoro kati ya Eritrea na Ethiopia, na Misri ilipanua juhudi za amani kati ya nchi hizo mbili na daima ilikuwa na nia ya Umoja wa Afrika.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy