Misri yaangalia mradi wa kuunganisha baharini kati ya ziwa la Victoria na Bahari ya Kati

Misri yaangalia mradi wa kuunganisha baharini kati ya ziwa la Victoria na Bahari ya Kati

 

Balozi Suha El Jundi, Msaidizi wa Waziri wa mambo ya Nje kwa Masuala ya Mashirika na Mikusanyiko ya Afrika aliongoza mkutano wa kamati ya kitaifa ya utaratibu kwa ajili ya kuimarisha Ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Afrika( NEPAD) uliofanyika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, nayo ni kamati iliyoundwa katika utekelezaji wa uamuzi wa Waziri Mkuu wa kuunda kamati ya kitaifa inayojumuisha Wizara kadhaa miongoni mwao ni Wizara ya Usafiri, Umeme, Umwagiliaji, Mazingira, Mawasiliano na Utalii ili kufuatilia miradi ya miundombinu ambayo Misri inatekelezwa kwa Ushirikiano na NEPAD ndani ya mfumo wa programu ya miundombinu ya bara inayojulikana kama PIDA.

Wakati wa mkutano huo, miradi ya kuunganisha Urambazaji wa Mito kwenye kando ya Nile nyeupe ilipitwa upya kati ya ziwa la Victoria na Bahari ya Kati, na mradi wa barabara ya Kairo ( Cape Town), na miradi ya uunganisho wa Umeme katika kaskazini na mashariki ya Afrika, na kupanua mistari ya fibre-optic kati ya nchi za Afrika, na jinsi ya kuongeza manufaa ya bara la Afrika kutokana na uzoefu wa Misri katika kuboresha mfumo wa posta, na kupanua programu za ujumuishaji wa kifedha kupitia programu za kidijitali.

Mkutano huo pia unahusisha hatua za kuendesha kituo cha Ubora wa Afrika katika uwanja wa kupambana na mabadiliko ya hali ya Hewa kinachohusiana na Shirika la maendeleo la Afrika. itakayokaribishwa nchini Misri ndani ya mfumo wa kasi iliyotokana na kuitishwa mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa, utakaofanyika Sharma El Sheikh mnamo Novemba 2022.

Balozi wa Suha Jundi, alieleza kwamba mkutano huo unaofanyika mara kwa mara kwa ajili ya kuangalia hatua zinazohitajika ili kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo na kusanya fedha zinazohitajika kwa ajili ya miradi hiyo, wakati huo unakuja baada ya kumaliza kwa mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya uliofanyika Brussels mwezi uliopita, ambao uliidhinisha kuanzishwa kwa upande wa Ulaya, kufadhili miradi chini ya mpango wa maendeleo ya miundombinu wa Afrika na miongoni mwao mradi wa kuunganisha Urambazaji wa Mto kwenye kando ya Nile nyeupe unaongozwa na Rais El-Sisi, kwa upande mwingine, kuna miradi mingine ambayo Misri inatilia maanani zaidi kwa kuzingatia kile kinachopata katika kukuza Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Afrika.