Kumbukumbu ya miaka 60ya uhuru wa Burundi

Kumbukumbu ya miaka 60ya uhuru wa Burundi

Burundi ilikuwa ufalme huru hadi ikawa sehemu ya koloni la Afrika Mashariki  la Ujerumani mnamo 1884, na baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, Ubelgiji ulitawala eneo la Rwanda-Urundi, na Burundi ikawa chini ya Mamlaka ya Ubelgiji mnamo 1924, na utawala wa kifalme uliendelea licha ya kutawaliwa kwa nguvu za Ulaya.

Mnamo 1959, Mtawala wa Burundi, Mwami Mwamubsa wa nne, aliomba uhuru kutoka kwa Ubelgiji na kufutwa kwa Muungano wa Rwanda-Urundi. 

Mnamo Julai Mosi, 1962, Burundi ilitangazwa kama ufalme huru unaodhibitiwa na jamaa ya TUTSI, ikiwakilisha nusu ya kusini ya eneo hilo linalojulikana kama Rwanda-Urundi, wakati  ambapo nchi ya Rwanda ya kisasa inawakilisha nusu ya kaskazini ya eneo hilo.

Inatajwa kuwa Misri ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza, na inachukuliwa kuwa nchi ya kiarabu ya kwanza, iliyoanzisha mahusiano ya kidiplomasia  pamoja na Burundi baada ya uhuru wake mnamo 1962, wakati ambapo  ilianzisha ubalozi wake nchini Burundi mnamo Desemba 1964.