Siku ya kimataifa ya Ardhi
Leo Aprili 22 Dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ardhi, nayo ni siku inayolenga kueneza ufahamu na kujali mazingira ya asili ya sayari ya Ardhi. Siku hiyo inakuja kutukumbusha umuhimu wa mazingira yetu na uhifadhi wake na viumbe hai ndani yake, haswa katika hali hizi ambazo Ardhi yetu inapitia, na kujitahidi kuimarisha mazingira yenye Afya, Usalama na Utulivu.
Historia ya Siku ya Ardhi Duniani ilianza mwaka 1969, wakati wazo hilo lilipoanzishwa na Seneta wa Marekani Gaylord Nelson, mwanasiasa na mwanamazingira wa Marekani, kisha msaidizi wake, Denis Hayes, mtetezi wa mazingira, alianzisha Shirika la The Bullit Foundation, lililoanza kuadhimisha siku hii kwa mara ya kwanza mnamo 1970, na kuifanya siku hii kimataifa na liliifanyikwa mnamo 1990 katika nchi 141.