Maadhimisho ya Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Leo, watanzania wanaadhimisha sikukuu ya Uhuru wake, ambapo Tanganika ilipata uhuru wake kutoka kwa utawala wa Uingereza mnamo tarehe Desemba 9, 1961, kisha baadaye nchi ya Zanzibar lilipata uhuru wake, Tanganika na Zanzibar zikiungana, kuundana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumbukumbu hiyo huadhimishwa kila mwaka kupitia neno la urais, maonesho ya kijeshi, na maonesho ya makundi ya kimuziki kwenye uwanja wa kitaifa huko Dar es Salaam.
Kwa upande wa mahusiano ya pamoja, Misri na Tanzania yana mahusiano yenye nguvu ya kihistoria, ambapo kabla ya kuanzisha Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 1964 na pia kabla ya uhuru wa Tanganika mnamo mwaka 1961, mnamo mwaka 1954 , Waafrika waliunda Umoja wa Afrika wa Tanganika ya kitaifa ukiongozwa na "Julius Nyerere" na wengine, ili Kuomba uhuru kamili mbali na Uingereza, na mapambano makubwa hayo kwa ajili ya kupata Uhuru, yameungwa mkono na kiongozi wa Misri Gamal Abdel Nasser, hadi Muungano huo kwa wingi umepatia Uhuru wa Tanganika mnamo mwaka 1961, na baada ya mwaka mmoja Nyerere alichaguliwa kama Rais wa nchi hii, kisha Zanzibar imejitenga na Uingereza mnamo mwaka 1963, na mnamo mwaka 1964, Tanganika na Zanzibar zimeunguana, na Misri ilikuwa miongo mwa nchi za kwanza zilizotambulika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na imeiunga mkono.
Mnamo mwaka 1964, wakati wa Muungano kati ya Tanganika na Zanzibar, Balozi Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi huru za Afrika alishika nafasi ya balozi wa kwanza wa Tanzania huko Misri, na kuna mahusiano mazito kati ya Viongozi wawili Gamal Abdel Nasser na Julius Nyerere na miongoni mwa dalili za kihistoria zinazobainisha mahusiano hayo ni ziara ya kihistoria ya Rais wa Tanzania Nyerere kwa Misri, ambapo Rais Gamal Abdel Nasser alikuwa naye hadi baraza la umma "Bunge" nchini Misri.
Mahusiano kati ya nchi hizo mbili zilichukua sura mbalimbali kwenye nyanja maalumu haswa kwenye uwanja wa maji ya Mto Nile, na pia ushirikiano kwenye nyanja za kiutamaduni, mafunzo, ushirikiano kifani, na utaratibu wa kisiasa kuhusu michakato ya kujenga usalama na kuunga mkono njia za utulivu na amani kwenye eneo la Afrika mashariki na pia ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara unaozingatia vipaumbele vya juu kwa hatua ya pamoja kati ya nchi hizo mbili, licha ya uanachama wa pamoja kati ya nchi hizo mbili kwenye makundi na mashirika kadhaa ya kikanda na Barani.