Siku ya kimataifa ya mwanamke wa vijijini
Kulingana na Shirika la chakula na kilimo (FAO), imesema kuwa isiyopungua asilimia 70 ya watu maskini Duniani wanaishi katika maeneo ya vijijini, na wanawake ni kwa wastani karibu nusu ya wafanya kazi ya kilimo katika nchi zinazoendelea.
Uimwenguni, mwanamke mmoja miongoni mwa watatu anafanya kazi katika kilimo, wanawake na wasichana katika maeneo ya vijijini wanateseka umaskini mkubwa. Wakati kiwango cha umaskini Duniani kimepungua, watu bilioni moja Duniani bado wanaishi katika hali ngumu sana ya umaskini, inayomaanisha kwamba viwango vya umaskini katika maeneo ya vijijini ni zaidi kuliko mijini.
Leo, Oktoba 15, ni maadhimisho ya kimataifa kwa "Siku ya kimataifa ya mwanamke wa vijijini" kwami mwanamke wa vijijini ana mchango muhimu katika maendeleo ya kilimo na vijijini, kuboresha kiwango cha Usalama wa chakula, na kutokomeza umaskini vijijini.
Kwa sababu mchango wao ni muhimu sana katika kupunguza njaa, umaskini na mafanikio ya Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, ni lazima tukabiliane na ubaguzi na kunyimwa ambazo bado zinawashinda mwanamke wa vijijini, na pengine kuthaminiwa kidogo kwa jukumu lao ni kuchangia kueneza ufahamu na kubadilishana mawazo kwa maisha bora zaidi kwao.