China ya Kikomunisti ni nchi ambayo ipo sasa kikweli, kwa hivyo Marekani inapaswa ikubali ukweli huo

China ya Kikomunisti ni nchi ambayo ipo sasa kikweli, kwa hivyo Marekani inapaswa ikubali ukweli huo

Rais Nasser: Waarabu wanaogopa kuanguka chini ya udhibiti wa nchi za kimagharibi, na hofu yao hii inafanya vyema kuwaachia hatua za nidhamu yoyote ya kulinda eneo wanaloishi.

Mara tu Waarabu wanapopata silaha zinazohitajika, wanaweza kuunda vikosi 12 vya kijeshi ndani ya muda fupi sana kuliko ile iliyochukuliwa na Ufaransa kuandaa vikosi vilivyopangwa kujiandaa kushiriki katika jeshi la Ulaya.

Nami nakataa mchango wa nchi yoyote ya kiarabu katika muungano wowote wa ulinzi; kama muungano baina ya Uturuki na Pakistan, basi ushiriki wa nchi yoyote ya kiarabu katika muungano wa Uturuki na Pakistan utaamsha hasira ya Waarabu.

Siwezi kukubali mradi wowote kutoka kwa miradi hii kwa sababu watu wetu wanapinga nidhamu yoyote kama hiyo; ambapo wanaizingatia aina ya ukoloni unaojificha.

Nilivyoeleza ukweli huo kwa  “Bwana Dallas”, na kulazimisha nidhamu yoyote vile kutoka aina hii kwenye Mashariki ya kati, italeta madhara kwa watu wote, kwa sababu itakuwa kujenga nafasi kwa wakomunisti kuchochea uchungu na chuki dhidi yake.. na wakomunisti wa Misri ni wachache.

Uwepo wa vituo vya jeshi vya Marekani nchini Libya hutoa Wakomunisti na fursa ya kueneza propaganda zao mbaya katika Mashariki ya kati na Ulimwengu wa Kiarabu. Wakomunisti walijaribu kuwashawishi wengi wa watu wa Misri kwamba mpango wa kipengele cha nne wa Marekani ni tendo la ukoloni tu, na mpango huo  hutoa nchi kwa kiasi kidogo cha misaada ya kiufundi, na hauna matokeo halisi ambapo umma unaweza kugusa, na umma wanataka matokeo halisi  yanayoweza kuona, ili utambue kwamba kuna misaada ya kweli.

Naamini kuwa serikali ya Marekani ya sasa yenye uelewa zaidi na ufahamu kwa matatizo haya, haswa tatizo la Israeli, kuliko serikali ya Rais “Truman”.

- Swali kutoka kwa Mhoji: Mnafikiri kwamba mambo lazima kusuluhishwa kati ya Waarabu na Israeli kabla ya mfumo wa ulinzi wa eneo la Nchi za Kiarabu?

Rais Nasser: Nadhani kwamba uwepo daima wa Israeli huathiri ulinzi wa eneo la Mashariki ya kati, kama ilivyo sasa, kwa sababu moja tu kwamba Israeli hugawanya Ulimwengu wa Kiarabu kwa sehemu mbili.

- Swali kutoka kwa Mhoji: Je, kuendelea kwa mgogoro wa Kiarabu - Israel kutazuia kulipa eneo la Mashariki ya Kati silaha na uimarishaji wake?

Rais Nasser: mgogoro huo hauna madhara juu ya hatua yoyote kwa upande wake, na ni kawaida kwamba Waisrael hutumia kila njia ya kuzuia misaada yoyote ya kijeshi kufikia kwetu; wao kwa tendo lao hilo, wataathiri masuala yanayohusiana na ulinzi wa Mashariki ya kati.

Sera ya “Mendes Frans” inapaswa kufuatiwa huko Marrakech na Algeria.

Naamini kwamba kutopendelea upande wowote kwa “Nehru” nchini India kutasaidia kumaliza Vita Baridi, na ninaamini kuwa India inapaswa kuwa kitovu cha nidhamu yoyote kwa ajili ya ulinzi wa Asia na Mashariki ya mbali, na Misri inapaswa kuchukua jukumu hilo hilo kuhusiana na ulinzi wa Mashariki ya kati; Misri inaweza kukusanya karibu naye timu ya nchi na watu.

Kuondolewa kwa Majeshi ya Uingereza kutoka Eneo la Mfereji wa Suez kutawafanya Wamisri kuzingatia mawazo na juhudi zao ili kuimarisha nchi yao.

China ya Kikomunisti ni nchi ambayo ipo sasa na ni ukweli uliokuwepo, Marekani inapaswa ikubali ukweli huo sio kukataa kuutambua, kwa sababu msimamo huu kwa upande wa Marekani unaashiria kutotenda na kupuuza kwa Wachina, na  kwa hilo uliwafanya mamilioni 400 au 500 kutoka kwa washupavu wachukue msimamo dhidi yenu. Nimekutana na watu ambao wametembelea China, na nilijua kutoka kwao kuwa Watu wa China wanapenda serikali yao ya kisasa, kwa hivyo, Marekani inapaswa kuitambua China ya Kikomunisti, kwa sababu kwa kutambua kwake kungemaliza Vita baridi.

ــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser na “John Law”, Mjumbe wa Gazeti la " The United  States News and World Report"

Mnamo Agosti 30, 1954.