Utaifa wa Kiarabu utaendelea imara, wa nguvu na thabiti

Utaifa wa Kiarabu utaendelea imara, wa nguvu na thabiti

Imefasiriwa na / Ali Mahmoud

Enyi Wananchi:

Hisia hii inayoenea katika taifa lote la kiarabu.. Hisia hiyo inayoonesha kujali kwa Utaifa wa Kiarabu, ni silaha yetu na ngome yetu katika kutetea utaifa wetu dhidi ya maadui zetu, utaifa wa kiarabu ulikabiliwa na ugaidi, mateso na unyanyasaji katika siku za nyuma, lakini haijafifia au kufa, lakini imebaki imara, wenye nguvu na thabiti.

Leo, -Enyi ndugu- licha ya ugaidi, licha ya unyanyasaji, licha ya njama za maadui wa utaifa wa kiarabu na mawakala, utaifa wa kiarabu utabaki imara, wenye nguvu na thabiti. (shangwe).

Enyi Wananchi:

Mmepinga sana na mlihangaika sana kwa ajili ya kuanzisha na kutetea utaifa wenu na kwa ajili ya kulinda nchi yenu isitegemewe na kwa ajili ya kuwaondoa wasaidizi wa ukoloni na mawakala, na hivyo mmeshinda siku zote kwa sababu mlipata uhuru na kujitegemea kwa nchi yenu, na mliwashinda wasaidizi wa ukoloni na mawakala na hakuna nchi, hata iwe kubwa kiasi gani, ambayo haijaweza kutumika kwetu kanuni ya utegemezi; kwa sababu sote tuliungana kulinda nchi yetu, na kauli mbiu yetu, siku zote, imekuwa si mpingamaendeleo wala utegemezi; kwa sababu nchi iliyopigana kwa ajili ya uhuru, ambayo ilipigania kuondoa mpingamaendeleo na wasaidizi wa ukoloni, kwa hali yoyote haiwezi kukubali mawakala wapya au kukubali utegemezi.

Kwa hiliy, Enyi ndugu, tumehifadhi uhuru wetu, tumehifadhi nchi yetu na tumehifadhi utaifa wetu, njama zikianza kutoka nje ya nchi, na wakomunisti wakitoka Damascus kwenda Baghdad kupanga njama dhidi ya ardhi yao na dhidi ya nchi yao, Sisi -Enyi Ndugu- tunajua kuwa njama hizo zinazopangwa.. Njama zilizopangwa na Wakomunisti dhidi ya nchi yetu hazitafanikiwa, kwa sababu hawatapata kati ya pembe za ardhi hii nzuri mtu yeyote anayeuza nchi yake na kukubali utegemezi, au anayesaliti nchi yake na kukubali kuwa wakala wa kigeni. Walitoka katika nchi hii nzuri, na mzee wao akatoka na kukusanyika nje ya nchi kuichafua nchi yake, taifa lake, watu wa nchi yake na watu wa taifa lake. 
Na hiyo, Enyi ndugu, si chochote ila ni asili ya mawakala ambao hawajisikii kwa nchi yao kwa thamani yoyote, hawana hisia kwa nchi yao kwa haki yoyote, lakini waliamini katika utegemezi, na waliamini kuwa mawakala wa mgeni kuvuta nchi yao katika maeneo ya ushawishi. Wakati hawakupata mtu yeyote kuwasikiliza kati yenu hapa katika nchi hiyo tukufu na katika nchi hiyo nzuri, walikwenda Baghdad; kwa sababu walipata makazi na msaidizi huko Baghdad, kwa sababu Qasim Al Iraq aliwafungulia Baghdad, na alikuwa akiamini kwa hii kwamba -kupitia mawakala hawa ambao waliamini utii na walikanusha utaifa- angeweza kukata viungo vya Jamhuri yetu, au angeweza kuzima mwanga ambao utaifa wa kiarabu ulizinduliwa na badala yake kuweka sera mpya aliyoifuata; sera ya utegemezi na sera ya upendeleo.

Qasim Al Iraq aliweza kukusanya maadui zetu kutoka kwa wakomunisti na mawakala huko Damascus ili kuwaelekeza dhidi ya Syria, na alifikiri kwamba kwa hili anaweza kufifisha utaifa wa kiarabu nchini Syria, au angeweza kufifisha utaifa wa kiarabu nchini Iraq, je, aliweza kufifisha utaifa wa kiarabu au kuzima utaifa wa kiarabu nchini Iraq? je, aliweza kukwaruza utaifa wa kiarabu nchini Syria? hajaweza kuzima utaifa wa kiarabu nchini Iraq, lakini aligawanya tu watu wa Iraq; watu wenye fahari ambao waliteseka na kupigana na Nuri Al-Saeed kuondokana na utegemezi, kuondokana na Mkataba wa Baghdad, na leo bado yuko katika Mkataba wa Baghdad, na leo bado anapigana tena ili kuondokana na utegemezi. Hataweza kuzima mwanga wa utaifa wa kiarabu nchini Iraq, na mawakala wa Kikomunisti hawataweza, chochote wanachoandika, hata wakihujumu, chochote wanachosema, hata wakidanganya kiasi gani, chochote wanachosema kwa watu wa Iraq, hawataweza kuzima moto wa utaifa wa kiarabu, wangeweza kwa muda kutegemea mambo ya watu wengi ambao wamechukia utaifa wa kiarabu kwa mamia ya miaka, lakini hawataweza kuua roho ya utaifa wa kiarabu katika nafsi za waarabu halisi. (Makofi).

Hili -Enyi Ndugu- ni suala letu, na Qassem Al Iraq alifuata njia zile zile alizofuata Nuri Al-Saeed kabla yake. Wakati mapinduzi yalipofanyika Mosul, na Qasim Al Iraq hakujua kinachoendelea Mosul, jambo la kwanza alilofuata ni kuwashtaki nyinyi na kuishutumu Jamhuri yenu; na alikuwa kwa hili, Enyi ndugu, alifuata njia ile ile ya Nuri Al-Saeed, na njia ile ile ya maadui wa utaifa wa kiarabu. Qasim Al-Iraq alikuwa akiamini kwamba hii inaweza kuzalisha tabia ya kitaifa ya kujitenga nchini Iraq ambayo ingemtenga na utaifa wa kiarabu, ili yeye na wakomunisti, watu wanaofuata mfumo huo, wafanyabiashara wa fursa na wajitenga waweze  katika hilo. Sera hiyo hiyo inayofuatwa na Nuri Al-Saeed na Fadel Al-Jamali inafuatwa leo na Qasim Al Iraq na wanyongaji wake, ikifuatiwa na Qasim Al Iraq na wafuasi wa Qasim Al Iraq dhidi ya Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu. Nao kwa hili, Enyi Ndugu, wanamaanisha wawe dhidi ya utaifa wa kiarabu, kwa sababu Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu ambayo imejitolea kubeba ujumbe wa utaifa wa Kiarabu.

Qasim Al Iraq, Leo, baada ya Mapinduzi Matukufu ya Iraq yaliyofanywa na Jeshi tukufu la Iraq, Qasim Al Iraq Leo, anakanusha utambulisho wake wa Kiarabu.. Anakanusha utaifa wake, pia alifuata njia za Nuri Al-Saeed, kwa nini mapinduzi yalifanyika huko Mosul? alisema: mapinduzi yaliyotokea Mosul ni hatua ya mgeni, na hatua ya Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu, na Qasim Al Iraq hakuwa na uwezo wakati huu kufikia Mosul, au kujua nini kinachoendelea huko Mosul.

Mapinduzi ya Iraq yalifanyika huko Mosul dhidi ya utawala wa ugaidi nchini Iraq; dhidi ya ugaidi wa wakomunisti nchini Iraq.. Dhidi ya ugaidi na unyanyasaji nchini Iraq, dhidi ya unyanyasaji wa Maafisa Huru nchini Iraq, sote tunajua hili, na kila mtu ulimwenguni anajua hili, na Mapinduzi ya Shawaf nchini Iraq hayakufanywa na kitendo cha serikali ya kigeni au kwa kitendo cha Jamhuri. Wakati Qasim Al Iraq alipowashtaki nyinyi, Enyi Ndugu, aliwashtaki nyinyi tu kuhalalisha msimamo wake juu ya unyanyasaji wa raia huru na wazalendo wa kiarabu.

Wakati Qasim Al Iraq alipowashtaki nyinyi kwa mashtaka haya -hakujua kinachoendelea Mosul- alikuwa akifuata sera ambayo ilikuwa ikigawanya watu wa Iraq na watu wa Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu. Qasim Al Iraq anaamini kwamba kwa kufanya hivyo -baada ya kugawanya Iraq katika makundi na mgawanyiko- ataligawanya taifa la kiarabu dhidi yake ili Ukomunisti uenee na kulidhibiti, na ili ugaidi utatawala katika nchi yetu kama ugaidi umeenea leo huko Iraq.

Enyi Ndugu:

Qasim Al Iraq alitoa ndege zake na akashambulia Jamhuri yetu; alishambulia kijiji kimoja katika Jamhuri yetu, na alibomoa baadhi ya nyumba ndani yake, na tulikuwa tukiweza kupigana na uchokozi huo mara mbili, lakini -Enyi Ndugu- hatukufanya hivyo, kwa sababu vijiji ambavyo tungeweza kupiga ni vijiji asilia vya kiarabu.. vinavyokusanywa na utaifa wa kiarabu navyo, wakati huo huo, pia vinakabiliwa na uchokozi wa ndege za Qasim Al Iraq na mabomu ya Qasim Al Iraq. Wakati Qasim Al Iraq aliposhambulia moja ya vijiji vyetu kwa ndege zake, alitaka turudishe uchokozi huu kwake, na hakujali kuwa baadhi ya watu wa Iraq watauawa, lakini alitaka kutumia hii kueneza ugomvi na chuki kati ya watu wa kiarabu nchini Iraq na Syria.

Sisi -Enyi Ndugu-  tulipokubali uchokozi, tuliukubali kwa sababu haturidhiki kamwe kushambulia kijiji cha waarabu nchini Iraq na kuua maisha ya Waarabu nchini Iraq, na Qasim Al Iraq na mabwana zake -Mabwana wa Qasim Al Iraq, mawakala wa ukoloni, mawakala na wakomunisti -hawataweza kutokomeza utaifa wa kiarabu katika eneo hili la ulimwengu.. Katika nchi za kiarabu, kwa sababu utaifa wa kiarabu umepigana kwa mamia ya miaka kwa uwepo wake, madhalimu wameshindwa, mawakala wameshindwa, washambuliaji wameshindwa, wavamizi wameshindwa, na utaifa wa kiarabu umeendelea ukiinua bendera yake baada ya kumwaga damu kwa hili.

Na tutatembea -Enyi Ndugu- njiani mwetu, hakuna mtu atakayetuvuruga, hakuna wakala atakayetuathiri, na bendera ya utaifa wa Kiarabu itafufuka kila mahali licha ya kutoridhika kwa wengi waovu.

Waasalam Alaikum warahmat Allah 
ــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Uwanja wa Al-Galaa huko Damascus

Mnamo Machi 12, 1959.