Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser Kuhusu Suala la Mfereji wa Suez Baada ya Kutaifishwa Kwa Maoni ya Umma wa Kiarabu Huko Kairo, Mwaka wa 1956
Imetafsiriwa na/ Alaa Zaki
Imeharirwa na/ Mervat Sakr
Wananchi:
Assalamu Alaikum
Leo, saa ya tano, Misri ilitangaza jibu lake kwa mwaliko ulioelekezwa kwake ili kushiriki katika mkutano wa London, unaofanyika siku ya 16, mwezi wa Agosti, jibu hili lilikabidhiwa kwa balozi za nchi zote huko Kairo, na wakati huo huo nilifanya mkutano wa waandishi wa habari kwa waandishi wa habari wote wa kigeni na Wamisri niliosoma taarifa hii na kujibu maswali waliyouliza.
Sitaki kuzungumza kuhusu shida kutoka kwa mwanzoni, lakini nataka kuzungumza kuhusu sehemu ya mwisho ya tatizo, mnaijua tatizo hilo kabisa, kutoka wakati wa "delespes" hadi tarehe ya 26, mwezi wa julai, tangu haki za Misri zilichukuliwa, na haki za Misri zilbakwa na vikosi vya kikatili, na tangu wakasema mfereji huu ulikuwa kwa kutumikia Misri, na kisha sisi sote, baba, na babu wetu tunahisi kuwa Misri ilikuwa katika huduma ya mfereji huu, tatizo ni kuwa kila mtu miongoni mwenu anajua kilichotokea katika siku hizi.
Leo, ninataka kuzungumza na nyinyi tangu wakati wa mwisho wa hotuba yangu, ambayo nyote mlisikia katika tarehe 26, mwezi wa julai, katika tarehe 26, mwezi wa julai iliamuliwa kutaifisha Kampuni ya Mfereji wa Suez, na napenda kuwaambia kila mmoja wenu kuwa kutaifisha kulikuwa kwa kampuni - Kampuni ya Mfereji wa Suez - sio Mfereji wa Suez, kwa sababu Mfereji wa Suez ni ardhi yetu, ardhi ya Misri, hakuna mtu anayeweza kusema kuwa tulitaifisha Mfereji wa Suez kwa sababu Mfereji wa Suez ni sehemu muhimu ya Misri, tulitaifisha Kampuni ya Mfereji wa Suez, na kisha kuna majibu ya nje ya nchi, hasa kutoka nchi za kikoloni, majibu hayo yalikuwa mzozo kubwa, na iliwakilisha vichwa vya habari katika magazeti akisema: kukamatwa kwa Mfereji wa Suez! Misri ilikamata Mfereji wa Suez, Misri ilikamata mfereji huo kwa msaada wetu, kwa Msaada wa Uingereza, Misri iliiba Mfereji wa Suez, Abdel Nasser Al-Khattak, Abdel Nasser aliiba mfereji huo, ni nini mzozo uliotokea nje ya nchi, sababu yake ni nini? Ninachoelewa kuwa Uingereza ilikuwa na asilimia 44 ya hisa na ilikuwa ikipata faida kila mwaka inakadiriwa kuwa karibu million 5 au milioni 6 pauni, ilikuwa mzozo uliopata ni kwa sababu Uingereza ilipoteza milioni 5 au million 6 pauni ? Au mzozo uliotokana kwa sababu Uingereza haikuridhika na fidia ya asilimia 44 iliyopokea ya hisa ? Hisa hizi ambazo walichukua kutoka kwetu wakati wa Ishmaeli, kwa bure, walichukua kutoka kwetu kwa bure na walichukua pesa, ndiyo, bila shaka, kitu kinachohitaji kuuliza na kitu kinachohitaji kustaajabu ni lazima kuwa kitu fulani kusababisha mzozo huu, kuna kusudi kubwa sana, Uingereza hafanyi mzozo huu kwa sababu ilinyimwa pauni milioni 5, lakini Uingereza inafanya mzozo huu kwa sababu inaangalia Kampuni ya Mfereji kwa msingi kuwa ni athari ya ukoloni, athari za ushawishi tuliosema kila wakati kuwa tunapinga, tulisema kuwa hatutakubali, kwa hali yoyote ile kuwa tunakuwa nyanja ya ushawishi wa mtu yeyote... Tunataka kuwa nchi huru inayodumisha uhuru wake, inayohifadhi enzi yake, na inayohifadhi heshima yake, lakini hatutakubali kuwa nyanja ya ushawishi kwa mtu yeyote chini ya jina lolote, au chini ya kampuni yoyote.
Baadaye, mkutano ulifanyika London, ambapo Uingereza, Ufaransa na Marekani zilikusanyika ili kujadili suala la Mfereji wa Suez, hatua zilizochukuliwa na Misri kuhusu Mfereji wa Suez, na kuamua, kuangalia kitu kutoka kwa msingi wa biashara ya Uhuru wetu, kuangalia kitu kutoka kwa msingi wa Uwezo wetu, walikutana na kisha walianza kwa uamuzi wa shinikizo la kiuchumi, kufungia fedha za Misri nchini Uingereza na Ufaransa, na wakati huo huo kufungia fedha za Misri huko Marekani... Aina ya shinikizo kwa kufuata nchi hizi kubwa zinazosema wao ni kiongozi wa ulimwengu huru kutishia Watu wa Misri, kulazimisha utashi wao kwa Misri, kuhusu nini?, kuhusu kitu ambacho ni chetu, kuhusu kitu tunachozingatia sehemu muhimu ya nchi yetu, kuhusu kitu kinachoingia katika msingi wa Uhuru wetu, kuhusu kitu kinachoingia katika msingi wa Uhuru wetu.
Shinikizo hili la kiuchumi lilichukuliwa kwa nia ya kuwapa njaa watu wa Misri kama walivyofikiria, au kushawishi watu wa Misri, na vitendo hivi viliomba maajabu kutoka kwa viongozi wa ulimwengu huru, walioomba uhuru, walioomba kujitawala, walioomba Uhuru wa watu, na walioficha Urithi wa Ukoloni huu na ngozi ya damu ya watu, walionekana kwa kweli na kufunua siri.
Tulikuwa tunatarajia shinikizo hili la kiuchumi kwa miaka miwili iliyopita, na tulikuwa tukipanga mambo yetu kwa msingi kuwa nchi yoyote ya nchi zote haijikuta kudhibiti Uchumi wetu, au kudhibiti pesa zetu, tulikuwa tunategemea kabisa kambi ya Sterling, tulikuwa tunategemea Benki ya London, hakukuwa na njia nyingine kwetu, katika miaka miwili iliyokuwa na pesa zote tunazotuma Uingereza kwa mwaka kwa pound milioni 8.
Shinikizo hili linaweza kutuathiri, lakini halitatuumiza, halitatusababisha kukata tamaa kamwe.
Tulikabiliwa shinikizo hili, na watu walikabiliwa shinikizo hili kwa Ujasiri, watu hawa waliokuwa wanakabiliwa na shida zote kwa Ujasiri, walikabiliwa shinikizo hili kwa Ujasiri.
Baada ya hilo nini kinachotokea? Hawakuacha na hii, lakini vitisho vya kijeshi vilianza, Mfereji ni kwenu! Waingereza wanasema Mfereji ni kwao! Chini ya sheria gani mfereji ni kwao, na chini ya sheria gani mfereji kwao, mfereji ni kwenu ulikamatwa na Wamisri, na tunahitaji kurudisha mfereji huu, shinikizo za kijeshi zilianza uhamasishaji, kuhamasisha meli za majini kwa njia ya karne ya kumi na tisa, harakati, Ufaransa pia ilianza, ambayo ina askari nusu milioni nchini Algeria inasema kuwa itahamasisha, itahamasisha anasema kuwa atahamasisha meli zake, atatoa askari kutoka Algeria ili kurejesha mfereji wao, ikiwa Wamisri walikamata kutoka kwao, na ikiwa Nasser alimwiba.
Kisha taarifa hii ya pande tatu, iliyosainiwa na Uingereza, Marekani na Ufaransa, ilionekana...Taarifa hii ilitangaza ulimwengu wote. Wakati huo huo, taarifa hii inawasiliwa kwa Misiri ili kuonesha siri, na taarifa hii inaonesha Ukweli, sio kwenu tu, bali maoni ya Umma duniani kote, maoni yote ya umma ya dunia yanaweza kufunua siri na kujua ukweli na nia, inafundisha kuwa Ukoloni una aina nyingi na ina majina tofauti, lakini katika majina haya yote, na katika fomu zote hizi ni Ukoloni.
Jibu lililotangazwa na Misri leo linaonesha makosa haya yote, walijaribu kwa kila njia kudanganya maoni ya Umma ya Ulimwengu, na kudanganya maoni ya umma peke yao, wakisema kuwa mfereji huu una tabia ya kimataifa na kwa mfereji huu ni wa Kimataifa, Waingereza wanasema hivi, Waingereza katika mwaka wa 1939 katika kesi inayohusiana na Kampuni ya Mfereji mbele ya mahakama za mchanganyiko, wakasimama hapo na kutetea kwa heshima kuwa mfereji huo hauna mamlaka ya Kimataifa bali Mfereji wa Misri.
Kampuni ya Mfereji ni Kampuni ya Hisa ya Misri, iliyochukua idhini yake kwa kipindi cha miaka 69 kutoka kwa serikali ya Misri.
Ibara ya 16 ya makubaliano yaliyohitimishwa kati ya serikali ya misri na kampuni kwa mwaka, inasema kuwa: Kampuni ya Mfereji wa Suez ni Kampuni ya Misiri chini ya sheria za nchi, kupuuza hotuba hii, hotuba hii yote: Ukweli huu ni ujinga, na walianza kuchanganya uhuru wa urambazaji katika Mfereji na Kampuni ya Mfereji wa Suez... Walianza kuuambia ulimwengu na kuuambia ulimwengu maoni ya umma kuwa uhuru wa urambazaji katika Mfereji wa Suez unaweza kupatikana tu na kuishi kwa kampuni hii ya kimataifa, kampuni hii inayo tabia ya kimataifa, maneno haya yatakuwa na jibu, misri walimjibu leo...Mkataba wa 88 uliitwa Mkataba wa tarehe 29, Oktoba, mwaka wa 1888, kuhusu kudhamini uhuru wa kutumia Mfereji wa Bahari wa Suez. Hii ina maana kuwa makubaliano haya yanahusika na kuhakikisha Uhuru wa kutumia Mfereji wa Bahari wa Suez.
Tulisema kuwa bado tunahifadhi neno letu kwenye makubaliano ya 1888, inayosikitisha pia kuwa taarifa iliyotolewa na viongozi wa Ulimwengu huru, ilitaja Ukweli fulani na kuachana na wengine, ilipuuza Ukweli wote kuwa misri ilipewa haki zake zozote.
Walisema katika taarifa kuwa Misri ilifanya makubaliano na Uingereza kwa mwaka mmoja, ambapo ilisema kuwa Mfereji wa Suez ni njia ya maji ya umuhimu wa kimataifa kutoka kwa mtazamo wa kiuchumi, kibiashara na kimkakati... Taarifa ya nchi hizo tatu iliondoa taarifa iliyotangazwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa, iliondoa sehemu ya kwanza ya kifungu hiki, kifungu cha nane cha makubaliano ya 1954, inayosema kuwa nchi hizo mbili zinaona kuwa mfereji ni sehemu muhimu ya misri, maneno haya yana shaka na tuhuma, ikiwa watajulisha nakala hii kuwa Uingereza ulisaini na Misri, kwa sababu wana nia ya kuingilia kati, wanataka kunyakua sehemu ya ardhi yetu waliyokuwa nayo kwa mwaka mmoja, kuwa ni sehemu muhimu ya Misri.
Ni wazi kabisa kuwa serikali za nchi hizo tatu zilikuwa zikisisitiza kutegemea madai hayo, na kupotosha maoni ya Umma ya Ulimwengu, kuwa Kampuni ya Mfereji wa Suez ni shirika la Kimataifa, na kuwa serikali ya Misri haiwezi kubadilisha hadhi yake.
Maneno hili ni Upungufu wa mikataba yote, Upungufu wa mikataba yote, maneno hili linaonesha nia iliyokusudiwa.
Mkutano walioalikwa, na walioalikwa, masharti yake, wakati na mahali... Nchi hizo tatu, zinazochukuliwa kuwa nchi au baadhi ya nchi zinazotumia Mfereji wa Suez, na kupuuza Uzembe wote unaohusika, walipuuza Misri na kuamua kuwa walikuwa wakifanya kazi kwenye mkutano wa kutafiti Mfereji wa Suez, na wakati huo huo, hii iliambatana na kile nilichokuambia juu ya tishio, tishio la kiuchumi, shinikizo la kiuchumi, na tishio la kijeshi, na walisema kuwa mkutano huo uko London, na waliamua kuwa wanaalika nchi zingine kushiriki kwa msingi wowote, ninajua nini kwa msingi gani katika zaidi ya nchi yetu ambayo hutumia Mfereji wa Suez, waliamua kuwa wao ni kuitwa nchi 24.
Walipuuza mkataba huo waliotegemea, unaotaja mfumo wa mwaliko, unaotaja walioalikwa, unaotaja kuwa mahali pa mkutano ni Kairo...Walisema kuwa nchi hizo tatu, viongozi wa ulimwengu huru, wanaamini kuwa hatua lazima zichukuliwe kuanzisha aina ya utawala chini ya usimamizi wa kimataifa ili kupata kazi ya mfereji kabisa kama ilivyoainishwa katika makubaliano ya 88, kwa kuzingatia haki halali za Misri.
Aya iliyosemwa katika taarifa yao, aya hii inaonesha wazi -wazi kabisa- kwanini serikali tatu za azimio hilo zilijaribu kuipatia Kampuni ya Mfereji wa Suez sifa ya kimataifa zikipuuza maandishi ya makubaliano na sheria zote ilikuwa wazi kuwa wanataka kukiuka haki wazi za Misri, wanataka kuchukua Utawala wake kuhusu mfereji, unaochukuliwa kuwa sehemu muhimu ya eneo lake.
Mnajua Usimamizi wa kimataifa unamaanisha nini ? ninawaona waangalizi wa kimataifa wanaosema hii kuwa aina mpya ya Ukoloni... Ukoloni wa pamoja, mara tu tuliamini kuwa tuliondoa ulinzi wa kawaida, unaowakilisha moja ya aina za Ukoloni, aina mpya ya Ukoloni ilianza kuonekana kwetu leo, Ukoloni wa pamoja chini ya jina la mkataba wa kimataifa.
Watu hawa, nchi zilizotia saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa, uliotangaza uhuru wa watu, uliotangaza utatuzi wa amani wa mizozo ya kimataifa, iliyounda Umoja wa Mataifa, ilipuuza mkataba huu, ilipuuza kwa kiwango ambacho nchi zote zinazoshiriki Umoja wa Mataifa zilishangaa, na baada ya kusema kuwa Misri ilikiuka makubaliano yake ya kimataifa, ninawapinga wale wanaosema kuwa hii inaonesha makubaliano ya kimataifa yaliyokiukwa na Misri.
Misri daima ilihifadhi ahadi zake zote, lakini ilisumbuliwa na kukiuka makubaliano yanayotokea leo, makubaliano wanayopuuza katika tamko la pande tatu na makubaliano wanayojaribu kuficha kutoka kwao haki zote za Misri ambazo ni wazi kabisa.
Ikiwa wanaweza wanashambulia mawazo ya watu wao, wanaweza, wanashambulia mawazo yetu? Mfereji wa Suez ni kwenu, haki zetu tunajua maarifa yote, walizungumza juu ya mfumo wa urambazaji ndani yake na urambazaji haukuwa wa kawaida na ulitishiwa, urambazaji ulikuwa wa kawaida, na wa kawaida zaidi kuliko wa kwanza, zaidi ya 766, meli iliyopita kupitia Mfereji wa Suez kutoka wakati wa kutaifisha hadi sasa, kile mtu alilalamika, walisema kuwa walichukua pesa za Mfereji wa Suez kuitumia kwenye Bwawa la juu, vinginevyo haingewezesha maendeleo na mageuzi katika mfereji, kuzungumza na kudanganya watu wao, na kushambulia mawazo ya watu wao.
Ninataka kukuambia kuhusu ripoti ya 1955 kuhusu Mfereji wa Suez, Usambazaji wa bajeti, mapato ya Jumla yalifikia paundi milioni 34 na nusu, jumla ya gharama, ikiwa ni pamoja na Utumiaji wa rasilimali ya kampuni ilifikia paundi milioni 18 na elfu 300, faida halisi ya kampuni ni paundi milioni 16 na elfu 300, Ufadhilii unatoa- kutoa kwa nani? - Milioni 5 paundi na nusu, na kisha kubaki salio halisi pauni milioni 10 na elfu 800... Pauni milioni 10 na dola elfu 800 zinagawiwa kwa wenyehisa... Hii ni ripoti ya mwaka wa 1955.
Leo, katika mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa saa 5, mmoja wa waandishi wa habari wa kigeni aliniuliza, ni kweli kuwa hautaelekeza kiasi chochote cha jumla ya utashi kwa mageuzi ya mfereji na maendeleo ya mfereji kulingana na nyakati? - Nilimwambia kuwa tulichofanya ni kuwa tulikuwa pauni milioni tano walizoweza kutoa, pauni milioni tano na nusu, pauni milioni 10 na elfu 700 zinazosambazwa kwa wanahisa baada ya wanahisa kudai fidia kamili, ambapo bado tuna karibu pauni milioni 16, nchi sawa na dola milioni 30 kwa mwaka, tulikuwa tukipata msaada dola milioni 12 kwa mwaka kwa Bwawa la Juu, na wataalam wako walikuwa Wakisema kuwa Bwawa la Juu, lakini gharama zilizopo kwa kweli, gharama zilizopewa bodi ya wakurugenzi kwa maelfu ya pauni, na kwa washiriki wa bodi ya wakurugenzi kwa maelfu ya pauni, na ruzuku anuwai zilizopewa kwa gharama ya Mfereji wa Suez, ziliachwa kutoka kwake.
Niliwaambia: ni kwa Masilahi ya Misri kuwa inaendeleza Mfereji wa Suez na kuifanya iwe sawa kwa mahitaji ya wakati, na wakati huo huo ni kwa masilahi ya Misri kuwa inachukua faida iliyokuwa katika roho ya wanyonyaji waoliteka kampuni kutoka kwetu na kuiba kutoka kwetu katika siku za Ismail, ili tuongeze uzalishaji katika nchi yetu na pia kukidhi mahitaji ya wakati.
Kiwango cha juu cha maisha, kiwango cha maisha tunacholenga, kinahitaji juhudi kubwa, kwa sababu kiwango cha maisha nchini Misri, kwa sababu ya ukoloni wa muda mrefu, ongezeko la idadi ya watu inahitaji juhudi kubwa, inahitaji kazi inayoendelea, na inatuhitaji kufanya kazi, tunafanya kazi katika maendeleo ya mfereji ili tupate utashi mingi uwezekanavyo, na tunafanya kazi katika Ujenzi wa miradi mingine, haswa mradi wa Bwawa la Juu.
Hotuba hii tunayosikia inakusudiwa kuchanganya na inakusudiwa kupotosha maoni ya Umma Ulimwenguni... Hotuba hii inawakilisha sera iliyofuatwa hapo zamani.. Sera ya nguvu ya nchi kuu ni sera ya kutumia nguvu, kulazimisha Utashi wao kwa nguvu.
Suala hili -ndugu- sio suala la mfereji, bali ni suala la nchi zote huru Ulimwenguni, suala la nchi ndogo zilizopata Ukombozi wao kupitia mapambano yao, yanayotaka kupata ukombozi wao dhidi ya nguvu ya kikatili na inayotaka kupata ukombozi wao dhidi ya sera ya nguvu ya nchi kubwa, Je, njia waliyojaribu kuwadanganya watu walioonekana katika taarifa ya pande tatu, iliwadanganya watu? Je, ilitudanganya hapa Misri? Je, ilitujihisi roho ya kushindwa au ilifanya mtu yoyote miongoni mwenu kufikiri juu ya kuacha heshima yake, haki yake, na utawala wake?!
Kulikuwa na majibu huko Misri, kila mtu aliamua kuchukua haki yake, kila mtu alihisi kuwa kuna njama ya kunyakua haki zake, kila mtu alihisi kuwa kuna njama ya kushambulia Utawala wake na kushambulia heshima yake iliyopangwa na nchi na viongozi wa Ulimwengu huru.
Mwitikio katika nchi hizi ulikuwa nini? Mwitikio katika nchi hizi ulikuwa kwanza matokeo ya msisimko.. waliweza kufichua makosa, waliweza kufichua habari potofu iliyokuwa ikielekezwa kwao kwa sababu ilikiuka utakatifu wa maoni yao, na sauti katika nchi hizi hizo zilianza kuita kuwa hatuna haki ya kuchukua njia hii, na kuwa sisi, tulioanzisha Umoja wa Mataifa, na tulioita kanuni tulizoziita baada ya Vita vya Kidunia vya Pili, ni lazima tutoe mfano...Sauti zimeanza kusema kuwa nchi yoyote ndogo iliyopata ukombozi wao itahisi kuwa iko salama, kuwa heshima yao yuko salama, na kuwa utawala wao ni salama, ikiwa mbinu hizi zitachukuliwa kuwa njia ya kutatua matatizo au njia ya kutatua migogoro.
Mwitikio hapa Misri ulikuwa dhamira na uamuzi, uamuzi tunaopigana, mapambano yetu ni mwendelezo wa mapambano yaliyopita.
Katika mkutano na waandishi wa habari, mwandishi mmoja wa habari aliuliza, " je, Kuna hali ya dharura nchini Misri ?" nikamwambia: kwa Mwenyezi Mungu, namaanisha, maisha yangu yote huko Misri najua kuwa kuna dharura dhidi ya Ukoloni iliyokuwepo na dhidi ya Unyonyaji, dharura dhidi ya Utawala wa kigeni, dharura dhidi ya wenye tamaa, kila mtu miongoni myetu anajiona katika dharura, na nikamwambia juu yangu mwenyewe, mimi hujiona kila wakati katika dharura ili niweze kuokoa nchi yangu Ichoyo wa wenye tamaa.
Njama hizi zinatufanya tuamini zaidi haki yetu, hatutawahi kuwasilisha, lakini tutapigania haki zetu.
Leo, mwandishi mmoja wa habari aliniuliza kwenye mkutano na waandishi wa habari, aliniambia, "nadhani Uingereza na Ufaransa zilitumia nguvu, utafanya kazi...?" Nilimwambia atetee nchi yangu hadi tone la mwisho la damu yangu; hii ni wajibu wangu, wajibu wa kila mzalendo. Aliniambia wajitoleaji ni kiasi gani? Nikasema, Mwenyezi Mungu anajua wajitolea wanajua nini, lakini tulianza kuamini katika kitu kinachoitwa Vita Vya Jumla, vita vya jumla vilivyopo kila mahali vilitaka kukombolewa, ile iliyoshinda mizinga, ndege, meli na nguvu ya kikatili, vita vya jumla vilivyokuwepo Algeria na ile iliyokuwepo Indochina, vita vya jumla ambavyo watu wote walijihamasisha ili kupata Uhuru wao na kupata Ukombozi, kupata sera zao, maisha, na kuanzisha aina fulani ya maisha mazuri.
Nilitaka kukuambia hitaji, baada ya kusikia ghasia hii nilishangaa na wakati mmoja nilifikiria, nikifikiria -ndugu- tunakubali mwaliko huu? -... Hakuna Utambuzi na hakuna Udhaifu, kamwe ikiwa tunaonesha ulimwengu kuwa watu hawa wanaozungumza lugha hii walisahau amani ya Ulimwengu, walisahau usalama wa Ulimwengu na baada ya hapo kutokea nini ?.. Vitisho zaidi.. kutishia watu wa Misri na kuweka shinikizo kwa watu wa Misri.
Baada ya mkuu wa Wizara ya Uingereza alisimama, na kufuata njia ya ajabu, alisema: Hatumwamini Nasser, ni wito gani, sisi hatuamini Nasser, Hatuna mahusiano...Tunamtaka Abdel Nasser... Ni busara kuwa kelele zote hizi ni kwa sababu tunamtaka mmoja wa watu binafsi! Wanataka mamlaka ya Misri, wanataka Udhibiti na Unyonyaji, na kuwa katika eneo la ushawishi....Bila shaka, baada ya maneno haya, mwitikio wa mwito huu ulikuwa dhidi ya utu wetu na dhidi ya mamlaka yetu, kwa sababu nia zilidhihirika na Ukweli ukadhihirika.
Mwitikio katika ulimwengu wote ulikuwa? "Kwa maoni ya umma huru, moja kweli bure alikuwa? Baada ya kutaifisha kwa Mfereji wa Suez siku moja baada ya tishio, sauti kutoka ulimwengu wa Kiarabu ilianza, na sauti kutoka ulimwengu wa Kiarabu zilianza kusema: jina lake sio Mfereji wa Suez, jina lake ni mfereji wa Kiarabu... Utaifa wa kiarabu tayari ulianza kuonekana katika maana yake halisi na katika hali yake bora; msaada kwa Misri na msaada kwa Misri kutoka kwa wafalme wa Kiarabu na marais wa Kiarabu wote walianza.. watu wa Kiarabu na taifa la Kiarabu walianza kuhisi Uwepo wake na kuhisi uhai wake, na ilionekana juu ya ukweli wake, ni nini yenyewe na moyoni mwake, Utaifa wa Kiarabu ulianza kuonekana kwa ulimwengu wote.
Kesho -ndugu- nilikuwa kusoma gazeti, na baada ya kusoma makala katika magazeti ya nje nikisema kuwa utaifa wa Kiarabu ulibaki kuwa ukweli, na kuwa utaifa wa Kiarabu unaweza kubaki kuwa hatari zaidi kuliko hatari ya kikomunisti.
Mnamo wa mwaka wa 1952 baada ya mapinduzi, nilipoandika kitabu cha "falsafa ya mapinduzi" nilikuwa nikiutazama utaifa wa Waarabu kuwa ndio sababu ya kwanza ya nguvu zetu... kuwa na Utaifa mmoja, kila mmoja wetu anahisi jinsi anavyohisi kama ndugu, sote kila mmoja wetu anahisi jinsi ndugu anavyohisi. Kila mmoja wetu anapigana kwa ajili ya suala hili ambalo ndugu wake analipigana.
Leo, kwenye mkutano wa waandishi wa habari saa tano, mmoja wa waandishi wa habari wa kigeni aliniuliza, na akaniambia: kuna mpango uliowekwa, uliopangwa, kwa hivyo ni nini kilitokea katika nchi za Kiarabu za majibu? Nilishangaa! Nilimwambia: kwa Mwenyezi Mungu, hauelewi hitaji, ni mtu gani mwerevu sana, asiye na kifani ambaye ana nguvu ya shirika awezalo, anafanya mpango huu, nikamwambia: Utaifa wa Kiarabu ulikuwa Ukweli halisia, Utaifa wa Kiarabu uko moyoni mwa kila mwarabu, Utaifa wa Kiarabu leo kila Mwarabu anahisi kuwa ni njia ya amani yake, njia ya usalama wake, njia ya Uwepo wake, njia ya kiburi chake, njia ya heshima yake, nikamwambia: leo, baada ya Misri kutishia, Utaifa wa Kiarabu ulionekana kila mahali, katika kila nchi ya Kiarabu mtu yeyote Ulimwenguni anaweza kupanga hisia hizi au kupanga kazi hii inayoonesha kuwa hisia ni moja, na malengo ni moja!
Mnahitaji kuelewa kuwa Waarabu wa leo sio Waarabu wa wakati huo, Waarabu walihisi kuwepo kwao, walihisi utaifa wao, na wakaanza kujisikia hisia kamili kuwa nguvu zao ni katika utaifa wao.
Katika Ulimwengu wote , kilichotokea nini, kila nchi ya uUimwengu ilihisi kuwa hatua hii ilikuwa tishio kwake, nchi huru zinazo uwezo wa kutoa maoni yao na utashi wake - nchi zote za Asia - kila nchi ya Asia ilitangaza kuwa hatua hii iliyochukuliwa na nchi tatu kubwa inachukuliwa kuwa tishio kwa amani, inachukuliwa kuwa kitendo cha karne ya kumi na tisa, maoni ya Umma ya bure, mkutano wa dhamiri Ulimwenguni karibu na suala hili, kwa sababu ni suala la haki, na suala la haki linalotetewa na nchi ndogo mbele ya nchi kubwa, zinazotaka kufuata sera ya nguvu.
Leo,ndugu, maoni ya Umma Ulimwenguni, dhamiri ya Ulimwengu inakusanyika karibu na suala la Mfereji wa Suez, suala la Misri, Uingereza, Ufaransa na Marekani halijawahi kubaki, suala la ulimwengu kutetea Ukombozi wake, uliopigania, suala la matumizi ya nguvu ya kikatili, au sera ya nguvu inayofuatwa na nchi kuu.
Leo, sisi, kama serikali, kwa kutumia haki zake, na kutumia utawala wake, hatuwezi kuwa chini ya kitu chochote kinachoathiri heshima yetu, na hatuwezi kuwa chini ya shinikizo lolote linaloathiri utawala wake, kwa sababu sisi ni mfano kwa ulimwengu, kwa kusema kuwa haki inaweza kushinda, na kwa kusema kuwa Ulimwengu una maoni ya bure ya umma, na kuwa dhamiri ya ulimwengu wote ni dhamiri huru, licha ya njia za taarifa tatu zilizotangazwa, na licha ya habari potofu ya taarifa hizo tatu.
Sisi, ndugu, tulisema kuwa tuko tayari kuelewa kuhusu Uhuru wa kutumia Mfereji wa Suez, mkutano wa nchi zilizosaini unakutana na 88, na wito kwa nchi zote zinazotumia Mfereji wa Suez, ambao ni zaidi ya nchi, kujadili kuhakikisha Uhuru wa matumizi ya Mfereji wa Suez katika Urambazaji, kitu kinachotuvutia sisi na nchi za Ulimwengu wote.
Mfereji wa Suez ni muhimu sana kwa biashara ya Ulimwengu, haswa kwa Uingereza, ni muhimu kwa nchi za Asia kwa sababu husafirisha bidhaa kutoka nchi za Asia hadi Ulimwengu wote, wakati nchi za Asia ni muhimu kwa sababu husafirisha mafuta kutoka kwao...Tuna wasiwasi sana, hatuna nia ya kuharibu nchi yoyote ya dunia, lakini kuchangia ustawi wake, kuchangia kuwezesha kazi yake, na kuchangia kuimarisha biashara yake, lakini mchakato sio mchakato wa uhuru wa kutumia Mfereji wa Suez, mchakato ni mchakato ya nguvu ya kikatili, Udhibiti, Unyonyaji, Utawala, nyanja za ushawishi.
Tulipotangaza maoni yetu leo, tulikuwa tukifanya kila kitu kwa ajili ya amani, tulikubali kanuni hizi, tulisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa, uliopuuzwa na nchi tatu za taarifa hiyo, na tukasema: tutafanya kila kitu katika uwezo wetu kutatua matatizo ya kimataifa kwa njia za amani, tulisaini taarifa ya pande tatu, na tukasema: tutatumia njia zote za amani kutatua matatizo ya kimataifa, kile kinachohitajika, ndugu, tunachofanya kwa ajili ya amani.
Nilikuambia: nilikuwa tayari kusafiri kwenda London, kwa hili, lakini ikiwa tunahitaji amani, lazima kuhifadhiwa kwetu na tunahifadhi hadhi yetu, ambayo ni mji mkuu wetu, tunaoanza kuhisi leo, na Uhuru wetu.
Swali ambalo mtu anajiuliza leo ni: Je, nchi hizi kweli wanataka amani ? Nchi hizi wanataka amani ? Au nchi hizi walikataa tamaa na walitaka kutatua matatizo yao.. Je, serikali ya Ufaransa inataka amani ? Ikiwa inataka amani, haikutatua matatizo ya Algeria, bali ilikubali uamuzi wa kibinafsi uliowekwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, lakini ilitaka kutatua matatizo yake ya ndani, inataka kutatua matatizo ya Algeria, ilitaka kutatua matatizo ya utawala na wizara zilizokuwa na wizara kila miezi 6. Je, serikali ya Uingereza inataka, au inataka kutulia kuwa ni Uingereza mkuu?! Nilisoma katika moja ya magazeti kuwa Uingereza haitakuwa tena mkuu, ni mchakato wa kiburi badala ya mchakato wa Upendo kwa amani.
Tulisema kuwa tutajaribu kwa njia zote za amani kutatua matatizo kwa njia ya kuhifadhi uhuru wetu na kuhifadhi heshima yetu, suluhisho zilizowatoliwa leo zinaonesha na kuonesha Ulimwengu wote kuwa Misri inataka amani, lakini pia inahifadhi Uhuru na heshima yake, inataka kutatua matatizo ya kimataifa kwa njia za amani, lakini haitakuwa chini ya nguvu ya kikatili, wala haitakuwa chini ya tishio la kiuchumi au tishio la kijeshi.
Maneno tuliosema leo -ndugu- yanaonesha kuwa Misri nzima inapambana na inajitahidi ili kuimarisha utawala wake, na kuimarisha Ukombozi wake, au Ufunuo huu uliotokea hautakuwa na faida, ikiwa Ufunuo ni kama uongo, kwa msingi kuwa Mfereji wa Suez hauhusiani na Misri, au chini ya Udhibiti au Ushawishi wa serikali au nchi za kigeni, hayo ni maneno ambayo akili haiwezi kukubali.
Ninataka kukuambia: ikiwa kulikuwa na njama za kila wakati kwa ajili ya Mfereji wa Suez, na tulizifahamu, kulikuwa na njama za kuifanya Mfereji wa Suez kuwa wa Kimataifa, na kulikuwa na njama za kupanua makubaliano ya Mfereji wa Suez, Kampuni ya Ndege ya Mfereji wa Suez ilituambia: panua makubaliano kwetu ili tuweze kuendelea na programu ya mageuzi, tuliwaambia: hatutapanua makubaliano, "Monsieur picoul" ndiye mkurugenzi - mkurugenzi wa kampuni - alisafiri kutoka miezi kadhaa hadi washington, na kujaribu kwa njia zote channel, zaidi ya hii -enyi ndugu - "Mheshimiwa Black", na ninyi nyote mnajua, yeye ni" Mheshimiwa Black", ambaye ni mkurugenzi wa Benki ya Dunia, aliponiambia, " tuko tayari ili kukupa dola bilioni kama mkopo ili kupanua Mfereji wa Suez na kuifanya kufaa kwa kifungu cha meli kubwa, tu kwa sharti; kuwa unatazama hali Ya Mfereji wa Suez, au kuanzisha mfereji mengine, nilimjibu, nikamwambia: mfereji mengine kwake: siwezi kamwe kutoa neno juu ya suala hili kabla ya kuhitimisha hali ya sasa katika Mfereji wa Suez, tunatafuta amani, na watu wote waliokombolewa, wanaojisikia huru, wanatusaidia katika hili.
Tutajaribu kwa njia zote kufikiri suluhisho nzuri, lakini ili kutetea heshima na Ukombozi wetu , tutapigana, mimi mwenyewe nitapigania kushuka kwa mwisho kwa damu yangu, hii ni njia yetu, na hii ndio tatizo letu, tunasonga mbele kwa nguvu, Uamuzi, dhamira na imani katika haki yetu ya uhuru, na haki yetu ya maisha.
Kusonga mbele, Mwenyezi Mungu atatusaidia, aliyetusaidia katika mapambano yetu yote, aliyetupa Ushindi katika mapambano yetu kwa miaka mingi, tutashinda nguvu ya kikatili, tutashinda nguvu za Unyonyaji, nguvu za Utawala, nguvu za Udhibiti, tutasonga mbele na imani katika haki yetu ya uhuru, haki yetu ya kuishi, imani ndani yetu wenyewe, imani katika Uwepo wetu, imani katika nchi yetu, imani katika nchi yetu...Imani kuwa Mfereji wa Suez ni sehemu muhimu ya Misri, hii ndiyo njia yetu... Mwenyezi Mungu akusaidie.
Wasslamu alaikum warahmtu Allah
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy