Siku ya Shahidi …. Jenerali Abdel Moneim Riyad
Na Dkt / Khairat Dergham
Siku ya Shahidi nchini Misri ni siku ya tisa kutoka Machi kila mwaka, na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ilitangaza kusherehekea kwa siku hii mwaka 1969 kwa kumbukumbu ya kufariki kwa kiongozi mkuu Jenerali Mkuu Wafanyakazi wa Vita vya Misri , Luteni Jenerali Abdel Moneim Riyad na pia alipewa cheo cha Luteni wa kwanza na Nyota ya heshima .
Ikumbukwe kuwa Luteni Mohamed Abdel Moneim Riyad amezaliwa mnamo 1919 na aliaga Dunia mnamo Machi 9,1969 na alishikilia nafasi ya Mkuu wa Mamlaka ya Uendeshaji wa Jeshi mnamo mwaka wa 1964, akawa na nafasi ya Mkuu wa Majeshi wa Kamanda wa Umoja wa Kiarabu, pia aliteuliwa katika vita vya mwaka 1967 Kamanda mkuu wa upande wa Jordani, na pia Jenerali Mohamed Abdel Moneim Riyad alishiriki katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia , Vita vya Palestina , Uchokozi wa nchi tatu huko Misri na Vita vya Attrition.
Pia alisimamia mpango wa Misri wa kuharibu mstari wa Bar Lev, na Asubuhi ya Machi 8, Luteni Jenerali Abdel Monem Riyad aliamua kwenda mbele kuona kwa karibu matokeo na maeneo ya kijeshi. Na ghafla Katika eneo hilo hilo la uwepo wa Jenerali, moto na makombora ya mizinga ya Israeli yalianza kurushwa hata aliuawa kishihidi kati ya askari wake, kama mfano unaotoa Tathmini kwa majeshi ya kimisri, Jenerali hakuwa anafuatalia hali kutoka ofisi yake huko Kairo, bali alisisitizia kwamba awe kati ya wanawe. Ili kuwa kiongozi, mwalimu na mfano wa kuigwa. Na ili kuongeza ari ya askari, kuwahimiza na kuwahamasisha kupigana.
Mwenyezi Mungu amrehemu shahidi, na alipatwa heshima na marehemu kiongozi Gamal Abdel Nasser, na Machi 9 imechukuliwa kuwa siku ya Shahidi, na kumheshimu, jina lake lilipewa nyanja, shule na mitaa mikuu.
Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wa nchi na wote waliojitoa muhanga kwa ajili ya kuirejesha ardhi ya Misri mpendwa yetu na kuipigania kuihifadhi.
"Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi." [Ali- 'Imran: 169].
