Mapinduzi ya 23 yalimpa Mwanamke Faida Kadhaa

Imeandikwa na Esraa Ahmed
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili/ Mervat Sakr
Mapinduzi ya Julai mageuko makubwa katika nafasi ya mwanamke, ambapo yana faidi kadhaa, na miongoni mwa maarufu zaidi haki ya mwanamke katika elimu, ambayo milango yake ilifunguliwa na mapinduzi, na wasichana wengi waliweza kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu bila hata malipo, na hii liliwanufaisha watu wa tabaka la kati ,ambapo wamenufaisha elimu bure inayofaa na uwezo wao wa kifedha, Nehad Abu-Al-Qumsan, Rais wa kituo cha Haki za Wanawake cha Kimisri, ameonesha kwamba kama sio mapinduzi ya 23, hangeingia chuo kikuu, akisema: " Najivunia kuwa mimi ni kutoka kizazi cha pili kilichonufaisha urithi wa Mapinduzi Julai 23."
Waziri wa Kwanza wa kike Mmisri alikuwa "Hekmat Abu-Zeid, aliyepewa lakabu"Moyo wa Mapinduzi mwenye huruma na Rais Gamal Abd-Elnaser, na alipewa pia Waziri wa kiroho" na Wanahabari, kwa sababu shughuli yake inayoendelea, na labda Waziri wa Kwanza ambaye mamlaka ya nchi ilikataa kutoa pasipoti yake. Ambaye alikuwa Dk. Hekmat Abh-Zid, Waziri wa masuala wa kijamii , na aliyeaga dunia kwenye Julai 30, 2011
Amezaliwa mnamo mwaka 1922 na kulelewa katika kijiji cha El-sheikh Daoud huko Assiut, Baba yake alifanya kazi kama Mwangalizi wa Reli, na alimpa fursa za uwezo wa kusafuri kila siku kutoka kijijini kwao hadi Bandari Dayrut, kwa ajili ya kujiunga shule za msingi na za kati, hadi alipofika shule ya sekondari huko Kairo aliendelea shule ya sekondari Helwan. Ama wakati wa masomo yake, aliongoza uasi wa wanafunzi wa kike ndani ya shule dhidi ya Waingereza, uliomkasirisha sana mamlaka ambao inamfukuza shuleni, na alilazimika kumaliza elimu yake shuleni Princess Fayza huko Alexandria.
Hekmat Abu-Zeid alijiunga sehemu ya historia katika kitivo cha Fasihi, Chuo Kikuu cha Fouad wa kwanza mnamo mwaka 1940 baadaye, na kupata shahda ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Sant Andrews huko Scotland mnamo mwaka 1950, na Shahda ya Uzamivu ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha London, mnamo mwaka 1955, baada ya kurudi huko nchini Misri, aliteuliwa katika Kitivo cha Wasichana katika Chuo Kikuu cha Ain Shams, kujiunga na timu maarufu za upinzani hadi kipindi cha Uvamizi wa 1956.
Moyo wa Mapinduzi mwenye huruma.. ni lakabu iliyompewa na Rais Gamal Abdel Nasser, baada ya kutoa uamuzi wa umma, ili kumteua kama Waziri wa Masuala ya Kijamii, kwa hiyo anakuwa Mmisri wa kwanza kuchukua nafasi Waziri mwaka 1962.
Mnamo mwaka wa 1962, aliteuliwa katika kamati ya watu 100 kuandaa mkutano wa kitaifa na kujadili mkataba ya kitaifa itakayotolewa mawazo yake yaliwavutia washiriki wote, na aliombwa kuzungumza katika kikao cha Maandalizi ambacho Rais Gamal Abdel Nasser atakihudhuria, ambapo Hekmat alikosoa uwepo mchache wa wanawake katika mkataba huo, na akapinga vikali kukataa kwa kibinafsi kwa Gamal Abdel Nasser kwa kile alichokiita ujana wa kiakili kwa kuzingatia shauku, ambayo aliiona kama mshiriki muhimu katika kujenga, na ilikuwa mazungumzo ya televisheni moja kwa moja, baadaye alichukua uangalifu na kupendeza kwa Rais mwenyewe, hivi alimchagua katika mwaka uleule kama Waziri wa Masuala ya Kijamii, kulingana na kile mwandishi wa habari Omar Taher aliitaja katika Kitabu chake Industrial Egypt.
Mnamo mwaka 1970, Hekmat alirudi chuo kikuu cha Kairo kufundisha Sosholojia baadaye, alikufa baada ya kuhangaika kwa muda mrefu na ugonjwa mnamo 2011 akiwa na umri wa miaka 90.
Marajeleo:
Gazeti la Al- Ahram
Al-Jazerah Net
Al-Youm El- Saba