Siku bila ya Magari huko Kigali

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky
Rwanda ni maarufu kwa "Siku Bure ya Magari ya Kigali", ndilo tukio ambalo hufanyikwa mara mbili kwa mwezi huko mji mkuu, Kigali, mnamo Jumapili ya kwanza na ya tatu ya kila mwezi, tena mnamo siku hiyo barabara nyingi zafungwa na pikipiki au magari hayaruhusiwi kuvuka barabara hizo ili watu waweze kutembea, kukimbia au baiskeli kwa uhuru kamili.
Historia ya siku hiyo ilianza mwaka 2016, ilipoanza ikiwa ni sehemu ya juhudi za Rwanda kuhifadhi mazingira, huku madereva wa magari wakihimizwa kuacha magari yao siku hiyo ili kutumia njia nyinginezo ambazo ni rafiki kwa mazingira, mfano kuendesha baiskeli na kutembea kwa miguu.
Hapo mwanzo tukio hilo lilitekelezwa siku moja tu kwa mwezi mnamo mwaka 2016, na baada ya mwaka mmoja tu kupita, yaani mwaka 2017, likabadilishwa kufanyikwa mara maada ya wiki mbili kwa mwezi, hivyo lilifanyikwa Jumapili ya kwanza na ya tatu ya kila mwezi, kutokana na umaarufu wake mkubwa, huku ikihudhuriwa na viongozi wengi miongoni mwa viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais wa nchi mwenyewe, Mheshimiwa Paul Kagame, ambaye ndiye Rais wa sasa.
Kama tulivyoeleza hapo awali, lengo la tukio hilo lilikuwa kuhifadhi mazingira, lakini limebadilika na kuwa mwaliko wa maisha bora kwa mazoezi na uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu, kwani kliniki nyingi unazozitembea hutoa uchunguzi wa matibabu bure kwa njia maalum.
Ikumbukwe kuwa tukio hilo halifanyiki katika jiji zima, lakini linatekelezwa katika baadhi ya barabara zilizotengwa kwa jambo hilo, wakati barabara zingine ziko na maisha yao kama kawaida, na tukio hilo halifanyiki siku nzima lakini huendelea kwa masaa matatu tu, kwa hivyo huanza saa moja asubuhi na kumalizika saa nne asubuhi, baada ya hapo maisha hurudi kama ilivyo katika siku za wiki zilizobaki.
Hatimaye, ikiwa ungependa kushiriki katika tukio hilo unachotakiwa kufanya ni kujitokeza na kujiunga na utakuwa na siku ya kufurahisha na yenye afya.
Vyanzo:
https://livinginkigali.com/kigali-car-free-day/
https://www.climate-chance.org/en/best-pratices/kigali-car-free-day/
https://images.app.goo.gl/q6jZv4Ya7GWeFmfP6