Mapinduzi ya Misri ya Julai 23, 1952 ..Mwanzo wa Mabadiliko

Mapinduzi ya Misri ya Julai 23, 1952 ..Mwanzo wa Mabadiliko

Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud

Mapinduzi ya Julai 23 ,1952 ni  mapinduzi yaliyoandaliwa na maafisa wa Misri wakiongozwa na Gamal Abdel Nasser, yaliyopindua utawala wa kifalme yakaanzisha mfumo wa Jamhuri na pia kuikomboa Misri kutoka kwa uvamizi wa kijeshi na kiuchumi wa Uingereza, baada ya hapo ,makubaliano ya kuondoka yalitiwa saini baada ya miaka 74 ya ukoloni .

Sababu kuu za Mapinduzi hayo ni kama ifuatavyo:

- Ubadhirifu wa Mfalme Farouk na wafausi wake na kususa kwa umma , hilo Ndilo lililosababisha hali mbaya ya kiuchumi na kupoteza haki ya kijamii.

- Kufunga shule za kikosi cha majini na cha  jeshi.

- Kutotilia  mkazo kwa Baraza la Usalama kutoa azimio kwa  maslahi ya Misri baada ya kuwasilisha suala la kutupilia mbali kwa majeshi ya Uingereza kwa Umoja wa Mataifa.

- Kupunguza idadi ya vitengo vya jeshi la kitaifa

- Mfalme aliunganisha nchi katika vita vya Palestina bila maandalizi sahihi, lililosababisha kushindwa bila shaka.

Matokeo ya Mapinduzi hayo katika nyanja za kijamii na kielimu... yanachukuliwa kuwa hatua ya mabadiliko katika mustakabali wa Misri kama ifuatavyo:

Kwanza: Ukabaila ulikomeshwa kwa kuidhinishwa kwa sheria ya kwanza ya mageuzi ya kilimo mnamo Septemba 1952, iliyoainisha umiliki wa kilimo kwa kila mtu hadi ekari 200 na iligawanya sehemu  ardhi ya kilimo iliyobaki kwa wakulima ambao hawakumiliki ardhi.

Pili: kuidhinisha sheria za bima ya kijamii na pensheni kwa wafanyakazi, kuainisha saa za kazi na kuruhusu wafanyakazi kushiriki katika vikao vya mabosi  wa  makampuni na viwanda, pamoja na kuamua asilimia yao ya faida.

Tatu: Wanawake pia walipewa haki ya kupiga kura na kugombea uchaguzi wa Bunge. vilevile, elimu ikawa bure katika viwango vyote, na shule nyingi na vyuo vikuu vilianzishwa nchini kote. 

 Na mwishowe, Mamlaka  kuu ya  Majumba ya Utamaduni na Vituo vya Utamaduni na Chuo cha Taasisi za Juu za Tamthilia, Filamu, Wakosoaji, Ballet, Opera, Muziki na Ngano zilianzishwa.