Enzi mpya

Enzi mpya

Imeandikwa na Menna Abdullah Mohamed 

Mratibu wa Lugha ya Kiswahili/ Mervat Sakr

Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ni nchi kubwa na muhimu sana katika bara la Afrika, lakini mfumo wa utawala ni mfumo muhimu sana kwa kila nchi.

Je, mfumo wa utawala wa kimisri ilikuwa jamhuri tangu mwanzo? Ama lini mfumo huo wa utawala umebadilika? Matukio gani ya mapinduzi ya Julai 23?  kwani Rais Gamal Abdel Nasser alipewa lakabu Baba wa Afrika? Hivi ndivyo tutavyojibu….

Tangu mwaka 1805 Utawala wa Muhammad Ali Pasha ulianza na uliendelea hadi mwaka 1848, na watoto wake na wajukuu kutoka familia ya El-Alwaya walimfuatilia katika Utawala wa Misri, mmoja hadi mmoja, ama mnamo mwaka 1936, Mfalme Mkuu aliye muhimu zaidi na wa mwisho ameshika utawala, ikiwa ni sahihi, alikuwa Mfalme Farouk wa 1, katika enzi yake pia, rushwa kwa aina zake zote ilisambaza katika nchi nzima na hasara ya utawala wa kifalme huko nchini Misri ikawa wazi, mpaka kundi la maafisa katika jeshi. iliamua kutendeka dhidi ya mfalme na kufanya mapinduzi ya kijeshi ambayo baadaye wananchi walijiunga na kuyaunga mkono Inadai mapinduzi ya Julai 23, 1952, mojawapo ya malengo yake muhimu lilikuwa ni kubadilisha Utawala wa Mfalme na kuitangaza Misri kwa mara ya kwanza mwaka wa 1953 kama Jamhuri ya Kiarabu.

  Maafisa Huru ni  nani?                                                
 Ni kundi la Maafisa wamisri walioanzisha Harakati la Siri kwa sababu Askari wa Jeshi hawakuruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa kamwe. Harakati hiyo ilianzishwa kutoka kikundi la maafisa wa jeshi kwa uongozi wa Mohamed Najiub. Usiku wa manane katika tarehe Julai 23, 1952, waliteka jengo la Maafisa Huru waliokuwemo ndani yake walikamatwa  kisha wakatangaza hotuba ya kwanza ya mapinduzi,  ambayo( Anwar Sadat) aliitangaza kwenye redio ya Misri kwa jina la (Harakati iliibarikiwa)


Maafisa wa kwanza na walio muhimu zaidi walioanzisha harakati hilo walikuwa: Gamal Abdel Nasser, Abdel Hakim Amer, Youssef Siddiq, Muhammad Naguib, Mustafa Kamal Sidqi.

   Ama Gamal Abdel Nasser ni nani? 


 Gamal amezaliwa mnamo mwaka 1918. Alikuwa afisa wa kijeshi na kisiasa mmisri ambaye aliwahi kuwa Rais wa Pili kuanzia mwaka 1956 hadi kifo chake mnamo mwaka 1970. Alikuwa mmojawapo wa viongozi wa Mapinduzi ya Julai 23 na alikuwa kiongozi katika Umoja wa Kisoshalisti wa Kiarabu, ulioita Umoja wa Waarabu.

      Je, michango ya Gamal Abdel Nasser kwa Afrika ni ipi?

 Gamal Abdel Nasser alikuwa mojawapo wa Marais walio Kwanza waliotilia manani bara la Afrika, na alijitahidi sana kuimarisha mahusiano pamoja na nchi za kiafrika, kwa hivyo aliitwa Baba wa Afrika kwa ajili ya harakati za ukombozi wa kitaifa katika Afrika, na kuchangia katika kuunga mkono uhuru wa nchi 34 za kiafrika, na vilevile kufungua mawimbi ya redio yaliyoelekezwa Afrika, yakitangaza kwa lahaja za Umoja wa Afrika ili kuelimisha raia waafrika kuhusu hatari ya ukoloni, ili Kairo iwe mtaji wa kwanza duniani kuzungumza kwa jina la mapinduzi ya Afrika dhidi ya ukoloni. 

Historia ndefu ya Misri imekuwa na vipindi vigumu, na bila shaka Misiri imepitia watawala wengi dhalimu na hawa wote walifikiri kwamba wangeweka matakwa yao na sera zao za dhulma kwa watu, lakini watu wamethibitisha katika zama zote kwamba utashi wa watu watu hauwezi kushindwa kamwe  na kuwa ulimwengu hautakosa watu huru.