Sambamba na Siku ya Diplomasia ya Misri..Waziri wa zamani sana wa Mambo ya Nje atoa Shukurani kwa Wizara ya Vijana na Michezo ya Kimisri kwa kutekeleza Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa
Waziri wa zamani sana wa Mambo ya Nje,Balozi Mohamed Al-Orabi alitoa Shukrani zake kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa kutekeleza Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kimataifa, uliotoa sura nzuri na chanya na Misri kwa Vijana tofauti kutoka nchi mbalimbali za Dunia, na hiyo ndiyo inayozingatiwa miongoni mwa aina za Diplomasia na Nguvu Laini ambazo pande na taasisi mbalimbali za Misri zinazishughulikia.
Kauli hiyo imekuja sanjari na maadhimisho ya Misri ya Siku ya Diplomasia ya Kimisri, ambayo ni siku ya kushukuru na kukadiria kwa juhudi na kukiri misaada yote inayotolewa na wanachama wa sekta ya kidiplomasia ya Misri.
Waziri huyo alitoa hotuba yake wakati wa shughuli za Udhamini wa marehemu Kiongozi Gamal Abdel Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa - kundi la tatu, unaopangwa na Wizara ya Vijana na Michezo pamoja na uangalizi wa Rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, kwa kushirikisha viongozi vijana 150 wanaowakilisha takriban nchi 73 kutoka nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, mwaka jana, huko Kairo, ukiwa na kauli mbiu ya "Vijana wa kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini."
Na kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy, alisisitizia Jukumu la Udhamini huo, ukiwa na uangalizi wa Mheshimiwa Rais wa Misri, umuhimu wake kama nguvu laini na kidiplomasia yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zote na pia uwezo wa kuimarisha mifumo ya Usalama na Amani Duniani, akiashiria kwamba kutegemea historia kunaweza kutusaidia kupata suluhisho mbalimbali kwa matatizo ya kisasa.