Sikukuu ya Wafanyikazi nchini Uganda

Sikukuu ya wafanyikazi inajulikana kama Siku ya Wafanyikazi Duniani na sikukuu ya Mei. Nayo ni likizo rasmi katika nchi nyingi Duniani kwa wakazi , na shule na makupuni mengi hufungwa. Na kawaida yake inakuja mnamo Mei mosi, lakini nchi kadha husherehekea mnamo tarehe zingine,tena Sikukuu hiyo kawaida huhusishwa na kumbukumbu ya mafanikio ya Harakati za Wafanyikazi.
Maadhimisho ya kwanza ya Sikukuu ya Wafanyikazi yalifanyikwa Mei mosi, 1890, na hayo baada ya Kongamano la Kwanza la Kimataifa kwa Vyama vya Kiujama huko Ulaya mnamo Julai 14, 1889 huko Paris, lilipotangaza kuainisha Mei mosi ya kila mwaka kuwa "Siku ya Wafanyikazi kwa Umoja na Mshikamano wa kimataifa .”
Tarehe hiyo ilichaguliwa kwa sababu ya matukio ya upande wa mwingine wa Atlantiki, ambapo mnamo 1884, Umoja wa Marekani wa biashara iliyopangwa na Vyama vya Wafanyikazi zilidai siku ya kazi iwe masaa manane; kisha kuanza kuitekeleza kuanzia t Mei mosi, 1886.
Na hiyo ilisababisha mgomo wa umma na ghasia za Chicago Haymarket, lakini hatimaye imeshaidhinishwa rasmi kwa masaa manane kwa siku ya kazi .
kwa miaka mingi, wanawake wengi nchini Uganda wamenyimwa haki ya kupiga kura katika sekta rasmi ya kibiashara kutokana ukosefu wa fursa ya kupata mikopo nafuu, ukosefu wa ujuzi wa kiufundi unaohusiana na kupanga miradi ya biashara na usimamizi wake , na ukosefu wa kupatikana masoko pamoja na taarifa zinazohusiana na fursa za biashara, na kwa kutatua tatizo hilo, Serikali ya Uganda mnamo mwaka wa fedha wa 2015/2016, ilizindua Mpango wa Ujasiriamali wa Uganda kwa lengo kuu la wawezeshe wanawake wa Uganda kuboresha viwango vyao vya mapato na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.
Na hiyo pia ni kutokana na michango ya Umoja wa Wanawake Waafrika wanaotetea haki ya kupatikana Ajira kwa wanawake wa vijijini.
Hatimaye, Sikukuu ya Wafanyikazi nchini Uganda sio tu kumbukumbu ya kusherehekea, bali ni maadhimisho ya kimataifa ya kupata haki zao.