Taarifa za kushangaza kuhusu Uislamu safi wa Gamal Abdel Nasser

* Katika suala la kutaifisha alimfuata Omar bin Abdulaziz aliyetaifisha mali ya Bani Umayya, kama mfano bora.
* Alipopata nakala kuu iliyoandikwa pamoja na makosa ikisambazwa Barani Afrika Wakati wa utawala wake, Qur’ani Tukufu ilikusanywa katika mamilioni ya kanda na diski zenye sauti za wasomaji wakuu, na wakat alipopata kuwa Maskini wa Afrika hawawezi kununua mashine za CD, alianzisha Idhaa ya kwanza ya Quran Tukufu Duniani kote.
* Idadi ya misikiti nchini Misri iliongezwa kutoka elfu kumi na moja kabla ya mapinduzi hadi elfu ishirini na moja mwaka wa 1970, Hiyo ni wakati wa utawala wa miaka 18 wa Rais Gamal Abdel Nasser, idadi (misikiti elfu kumi) ilijengwa, Ambayo ni sawa na idadi ya misikiti iliyojengwa nchini Misri tangu ushindi wa Kiislamu hadi zama ya Abdel Nasser.
* Somo la elimu ya kidini limefanywa (somo la kulazimishwa) inategemea kufaulu au kufeli kama masomo mengine kwa mara ya kwanza katika historia ya Misri, wakati ilikuwa ya hiari katika ufalme.
* Al-Azhar Al-Sharif iliendelezwa na kugeuzwa kuwa Chuo Kikuu cha kisasa kinachosomesha Tiba na Uhandisi, ilipowakuta wachache wasio Waislamu, wanadhibiti taaluma hii Barani Afrika.
* Abdel Nasser alianzisha Jiji la Jumbe za kiislamu kwenye eneo la ekari thelathini, linalojumuisha wanafunzi wanaotoka nchi sabini za Kiislamu wanaosoma Al-Azhar bila malipo na malazi kikamilifu bure pia. Idadi ya wanafunzi Waislamu katika Al-Azhar kutoka nje ya Misri iliruka mara kumi kwa sababu ya shauku ya Abdel Nasser kwa Al-Azhar, aliiendeleza na kuigeuza kuwa Chuo Kikuu kikubwa chenye matawi katika nchi nyingine.
* Alisaidia sana ukombozi wa Algeria,Kairo ulikuwa mji mkuu wa mapinduzi na sauti ya Waarabu ilikuwa sauti ya mapinduzi ya Algeria na alipigana vita vya Uarabuni wake. Na tulikaribia kulilia kama Al-Andalus baada ya miaka 150 ya uvamizi wa Ufaransa na inabaki hadi leo katika aya ya 7 ya Crusader NATO, ambayo Erdogan ni mwanachama rasmi wa sehemu ya Algeria ya Ufaransa.
* Maana za Qur’ani Tukufu zilitafsiriwa kwa lugha kadhaa wakati wa utawala wake.
* Mashindano yaliandaliwa katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika ngazi ya Jamhuri, na ulimwengu wa Kiarabu, na ulimwengu wa Kiislamu, Rais Abdel Nasser binafsi alikuwa akisambaza zawadi kwa wahifadhi wa Qur'ani.
* Ensaiklopedia ya Gamal Abdel Nasser ya Fikhi ya kiislamu iliwekwa, ambayo iliyotia ndani sayansi na sheria zote za dini ya kweli katika majalada kadhaa na kusambazwa ulimwenguni pote.
* Maelfu ya Vyuo vya kidini vya Al-Azhar vilijengwa huko Misri, na matawi ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar yalifunguliwa katika nchi nyingi za Kiislamu.
* Gamal Abdel Nasser aliunga mkono nchi zote za Kiarabu na Kiislamu katika mapambano yao dhidi ya ukoloni.
* Alisali sala ya Ijumaa huko Moscow, akakatisha mazungumzo, akafungua Msikiti Mkuu wa Moscow, na kumpinga Khrushchev katika hotuba ya hadharani.
Akisema, “Sitawaruhusu kueneza ukomunisti katika nchi zetu za Kiarabu. Sisi ni waamini na nyinyi wasioamini .” Khrushchev alijibu, Mtu huyu anadhani anatawala Ulimwengu mzima, hotuba ya mwaka wa 1959 huko Damascus.
* Jumbe za Al-Azhar wakati wa utawala wake, zilikuwa na viwango vya juu zaidi vya kuingia katika dini ya Kiislamu katika historia,ambapo idadi ya waliochagua Uislamu kama dini kutokana na Jumbe za Al-Azhar wakati wa enzi ya Rais Gamal Abdel Nasser ilifikia watu 7 kati ya 10, kulingana na takwimu za Baraza la Makanisa Ulimwenguni.
* Sheria ilitolewa inayokataza kucheza kamari na ulikuwa mchezo anaoupenda zaidi Farouk.
*Abdel Nasser alitoa maamuzi ya kufunga yote nyumba za kulala wageni za Masonic, na Vilabu vya Rotary na nyumba za kulala wageni za Baha'i.
* Uamuzi ulitolewa wa kufuta idhini za ukahaba na alitoa sheria dhidi ya ukahaba, iliyoratibiwa katika enzi ya kifalme na enzi ya ukoloni wa Waingereza.
* Msichana huyo alifikia elimu ya kidini kwa mara ya kwanza kama Taasisi za Azhar kwa wasichana zilifunguliwa, Na mashindano mengi yalifanyika katika miji yote kuhifadhi Qur’ani, na Vitabu vyote vya turathi za Kiislamu vilichapishwa katika matoleo maarufu na vyombo vya habari vya serikali ili viweze kufikishwa na wote.
* Pia alikuwa na shauku ya kusali Sala ya Ijumaa pamoja na wananchi misikitini.
* Alisali Sala ya mwisho ya Ijumaa kabla ya kifo chake tarehe ishirini na tano Septemba huko Al-Azhar Al-Sharif.
* Na hitimisho la kazi zake ni kuwalinda Waislamu katika matukio ya Black September "mwezi mweusi wa Septemba" huko Jordan, tarehe ishirini na saba Septemba 1970.
* Gamal Abdel Nasser alifariki Dunia siku ya Jumatatu, Septemba 28, 1970, inayolingana na tarehe ya Hijri ya tarehe 27 Rajab 1390, kwa kumbukumbu ya Siku ya Isra na Mi'raj.