Ujasiri wa Nasser na Hekima ya Nkrumah: Kurudi tena asili (2)

Ujasiri wa Nasser na Hekima ya Nkrumah: Kurudi tena asili (2)

Na/ Dkt.Hamdi Abd El Rahman

Ni Hakika  kwamba Waziri Mkuu wa Ethiopia,Abi Ahmed, na wenzake hawajui ukweli kuhusu nafasi ya Misri katika harakati ya Umoja wa Afrika, mji mkuu wa nchi yake unalolishuhudia.

Pengine tutampa msamaha, ambapo yeye ni kutoka kwa kizazi kilichofungua macho yake kwa ukandamizaji na unyanyasaji wa utawala dhalimu wa kijeshi katika nchi yake. Hata hivyo, haikubaliki mtu kudanganya huku ana Uzamivu na hata Tuzo ya Nobel na kutilia shaka utambulisho wa kiafrika wa Misri.

 Anaongoza kampeni ya kiitikadi iliyopitwa na wakati inayobagua rangi nyeusi na dhana ya Kiafrika na kama muktadha wa mchakato wa usaliti wa kisiasa ili kupata uungaji mkono wa ndugu zetu Waafrika wasio Waarabu katika suala la Bwawa la Maendeleo.

Anaweza kurudia rekodi za ikulu yake ya serikali au kumbukumbu za makao makuu ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa nchi yake kujua jinsi alivyompokea Gamal Abd El Nasser akifuatana na Ahmed Ben Bella kwenye ndege moja hadi Addis Ababa kwa mahudhurio ya Mkutano wa Wakuu wa Afrika mwaka 1963. Nasser alikuwa akionyesha mwelekeo wa kipekee katika harakati za Umoja wa kiafrika, na yeye ndiye aliyeiita Mazrouei jina la Afrabia ili kupata nguvu ya viunganishi vya kihistoria na kiustaarabu kati ya Waarabu na Waafrika. Ubalozi wetu mjini Addis Ababa uliitwa Ubalozi wa Waarabu,na hapo ndipo Nasser alipokutana na viongozi wa harakati za ukombozi wa Afrika, waliotambulishwa kwake na Waziri Mohamed Faeq kutokana na kuwafahamu yeye binafsi.

 Miongoni mwa maamuzi ya mkutano huo ni kuundwa kwa kamati ya kusaidia harakati ya ukombozi wa taifa, huku Misri na Algeria zikiwa ndio wakuu wa wanachama wake.Je, damu za mashahidi wa Misri hazikuchanganyika na damu za ndugu zao kutoka Algeria katika kutetea ardhi na heshima na kumfukuza mkoloni? Labda kurudi kwa fuvu la shahidi wa Misri kutoka Ufaransa hadi Algeria kunatukumbusha uhusiano wa karibu uliotetewa na kizazi cha kwanza cha waanzilishi.

Wakati wa utawala wa Rais Thabo Mbeki, ambaye aliendeleza Mpango Mpya wa Maendeleo Barani Afrika, unaojulikana kwa ufupi NEPAD, nilialikwa kwenye warsha ya kujadili suala hilo kwa mahudhurio ya Rais mwenyewe. Nilipotoa hotuba yangu, mmoja wa waliohudhuria, kwa bahati mbaya kutoka nchi za Bonde la Mto Nile, aliniuliza kuhusu utambulisho wa Misri na iwapo ni Mwarabu au Mwafrika. Bila shaka, suala hili lilitatuliwa nchini Afrika Kusini yenyewe, kwa mazungumzo ya mwamko wa Afrika Na sio kuzingatia weusi tu kama jina la utambulisho, kwani Afrika Kusini mpya ni nchi ya makabila mengi. Nakumbuka mmoja wa waandishi wa habari wa kiafrika alimuuliza Rais Nasser iwapo Misri ni mwarabu au mwafrika. Jibu lake lilikuwa la busara sana na ni zote mbili. Misri, ambayo ina Egyptology kueleza historia yake na ustaarabu, haitilia shaka.

Mbinu ya Nasser ilikuwa ya kipekee katika vuguvugu la Umoja wa kiafrika, ambalo lilipingwa na pande kadhaa. Wapo kama James Baldwin, ambaye alizaliwa ughaibuni na kuishi baadhi ya maisha yake barani Afrika, aliamini katika hali isiyoepuka ya kurudi kwa jamii ya watu weusi barani Afrika, hata alipokuwa anaishi Paris. Alipenda kuelezewa kama mwandishi mweusi. Kwa upande mwingine, Ali Mazrouei aliyezaliwa barani Afrika na kuishi ughaibuni aliwasilisha dhana ya uamuzi wa kiutamaduni usiotegemea rangi kwani ni kiungo cha kijiografia, kidemografia, kisiasa na kiitikadi. Kwame Nkrumah alikuja kuchanganya mielekeo miwili, yaani umuhimu wa rangi na mahusiano mengine ya kiutamaduni na kiitikadi. Huo unakuja uhusiano kipekee kati yake na Nasser na hata msisitizo wake wa kuoa mwanamke mmisri. Hapa kuna dalili muhimu kuhusu ukweli wa dhana ya Umoja wa kiafrika.

Nkrumah alimpeleka rafiki yake Meja Salih Said Senari, ambaye alikuwa mmoja wa Waislamu wa kwanza wa Ghana kusoma Misri, kutafuta mke wa Misri.

 

Meja Senari, anayehudumu katika Jeshi la Ghana, kwa bahati nzuri alioa na mwanamke Mwislamu wa Misri aitwaye Souad El Roby, mwaka wa 1953.

Kwame Nkrumah alimtembelea Senari nyumbani nwake katika kitongoji cha Accra. Alibisha mlango mara kadhaa hadi Souad, mke wa Meja Sinnari, alipofungua mlango.Nkrumah aliunyoosha mkono wake kumpa mkono, lakini alichanganyikiwa kidogo na kuweka ncha ya shela iliyokuwa imefunika kichwa chake mkononi na kumsalimia Nkrumah. Hata hivyo, hakumruhusu kuingia sebuleni bila mumewe kuwepo.

Inaonekana kwamba tabia ya Souad kwa Nkrumah ilimpendeza na ikaongeza azimio lake la kuoa mwanamke mmisri.“Kaka yangu, nikioa mwanamke wa aina yako nitakuwa na usalama wa kutosha,” Nkrumah alimwambia rafiki yake. Fathia Halim Rizk, binti wa kitongoji cha Al-Zaytoun mjini Kairo, alichaguliwa kutoka miongoni mwa wanawake watano licha ya kukataa kwa mamake kwa sababu hakutaka kumpoteza binti yake katika nchi ya mbali.

Meja Senari aliashiria kuwa Rais Gamal Abd El Nasser alimshawishi mama yake Fathia na kulipa mahari kwa niaba ya Nkrumah. Kwa Hakika, Fathiya alisafiri kwenda Ghana pamoja na Meja Sinari na mkewe Souad.

Busara za Nkrumah zilidhihirika katika ndoa hii, Nasser aliyohimiza katika kufikia Umoja wa kiafrika kwa njia ya ndoa kwa kuunganisha ukanda wa Afrika Kaskazini na bara zima la Afrika. Kulikuwa na hasira na wasiwasi miongoni mwa safu za mgawanyiko wa wanawake katika chama cha Nkrumah, na hata mama yake Elizabeth alikasirishwa na wazo la kuolewa na mwanamke mweupe, lakini Nkrumah aliwaeleza kuwa yeye ni kitambulisho na mfuasi wa Kiafrika na hata ikiwa ni rangi nyepesi. Kwa ushirikiano wa Fethiya na utangulizi wa busara kwa utamaduni wa jamii ya Ghana, alishinda kupongezwa na wanawake wa soko walioandika juu ya mauzo yao: "Fethiya anastahili Nkrumah."

Pengine Nkrumah pia alikuwa anafikiria kushinda ukabila, kana kwamba alioa mwanamke wa kabila fulani, jambo hilo linaweza kuamsha wivu na hisia za makabila mengine.

 Hivyo basi, ujasiri wa Nasser na hekima ya Nkrumah vilichangia kutekelezwa kwa dhana ya Afrabia kuwa ukweli, na mwanamke wa Misri akawa mke wa Rais wa Ghana baada ya uhuru. Huo ni ukurasa mmoja tu kwa wale ambao hawakumbuki historia ya Afrika ya kisasa ya Misri.