Mnamo Julai iliyopita, Mitandao ya kijamii ilikuwa na picha inayosikitisha ya watoto kutoka Nigeria wakiwa wameshika kifaa cha Tablet ikiwa na bendera ya Israeli nyuma yake, kama jaribio la kuipamba sura yake mbaya kwa kufanya unyanyasaji dhidi ya watu wa Palestina wasio na ulinzi, na kama kupenya kupya kwa bara la Afrika, ubalozi wa Israeli nchini Nigeria ulinunua na ulieneza Tablet 70 kwa watoto waliohamisha makazi yao karibu na mji mkuu Abuja, wenye umri wa miaka 6-9 kujifunza Lugha na Hisabati, na ubalozi uliweka bendera ya Israeli kama kifuniko cha nyuma kama aina ya propaganda.
Jambo hilo limenisikitisha sana ni jinsi tulivyokuwa na jinsi gani tukawa barani Afrika? ... ambalo nchi zake nyingi zilikuwa zinatusaidia katika upande mmoja dhidi ya ubeberu na Uzayuni, likithamini mchango wa Misri karibu nayo katika mapambano yake ya kitaifa hadi kupata uhuru wake na Misri haikuacha jukumu lake la kuhifadhi Umoja na Utawala wa nchi zake hata katika hali yake ngumu zaidi baada ya kushindwa mnamo 1967, na jambo hili lilisababisha faida kadhaa kwa Misri kama kisiasa, kiuchumi, na ya kimkakati, na lilihifadhi Usalama wake wa kitaifa unaoenda hadi kusini, ambapo msingi wa maisha hupatikana.
Enzi ya Abd El Nasser imeisha pamoja na kifo cha mmiliki wake, ikiacha hazina ya kimkakati barani Afrika, lakini nyuma yake – El Sadat - alipoteza hazina hiyo, akafukuza Misri kutoka Afrika na akaacha mchango wake wa kihistoria hapo, akiacha nafasi kwa adui wa Kizayuni kushika nafasi yake na kudhoofisha Usalama wake wa kitaifa, haswa katika nchi za Bonde la Mto Nile.
Nasi tunasimama hapa mbele ya tukio la kihistoria la kimisri huko Nigeria, ambapo ilipotokea mnamo 1967, wakati ambapo ulijibu ombi la msaada kutoka huko licha ya maumivu ya kushindwa, na tukio hili linasimuliwa kwetu kutoka kwa Bwana - Muhammad Fayek - Mhandisi wa mahusiano ya kimisri -kiafrika wakati wa Rais Gamal Abd El Nasser katika kitabu chake muhimu – Abd El Nasser na Mapinduzi ya Afrika-.
Mnamo Agosti 1967, yaani wiki chache baada ya kushindwa, Rais Gamal Abd El Nasser alipokea barua kutoka kwa Kanali - Yaakub Juan - Rais wa Nigeria na Kamanda mkuu wa Kijeshi, ambapo alionesha hatari zinazokabili nchi yake kutokana na uvamizi wa ndege zikawa miliki ya - Ajoku - kiongozi wa kutengwa katika mkoa wa - Biafra – ambao ukawa ukipiga mji mkuu Lagos kila siku bila upinzani wowote, lililoleta hali ya hofu na wasiwasi iliyoeneza kati ya watu na haswa wakazi wa mji mkuu .
Na katika barua yake, Joan alielezea kwamba aliweza kupata ndege kadhaa za MiG-17 zilizotolewa na Umoja wa Kisovyeti, lakini hakupata wanahewa wanaoweza kuziendesha ndege hizo. Joan aliendelea kusema kuwa anajua hali ngumu ya kijeshi ya Misri, pia anajua kwamba inahitaji kila mpiganaji, lakini anatumai tu Rais Gamal Abd El Nasser atumie nguvu yake kumshawishi Rais wa Algeria Houari Boumediene ampatie wanahewa wengi wa Algeria wanaopata mafunzo ya ndege za MiG-17 alizokuwa nazo. Barua hiyo ilionesha kuwa Suala la kupata wanahewa hawa limekuwa suala la maisha na kifo.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Nigeria vilizuka tangu Kanali Agoku, Mtawala wa kijeshi wa mashariki mwa Nigeria, alipotangaza uhuru wa eneo hilo kwa jina la Jamhuri ya Biafra mnamo Juni 30, 1967, na aliweza kupata ndege kadhaa zenye wanahewa mamluki wa Ulaya, wengi wao walioajiriwa na Chumbi wakati alipojaribu kujitenga katika mkoa wa Katanga (pale Congo) na hatari kwa Nigeria kwa kujaribu kujitenga na mkoa wa utajiri wa mafuta wa Biafra ikawa ni sawa na ile ambayo Congo hapo awali iliyopatia na majaribio ya kutenganisha Mkoa wa Katanga wa utajiri wa madini.
Hiyo ilikuwa ikimaanisha kukata Nigeria vipande vipande kutoka mikoa mingine, inayokabiliwa na shida nyingi za kidini, kikabila, kiutamaduni na kisiasa, haswa kati ya Kaskazini na Waislamu wengi, na Mashariki na Wakristo wengi. Hali hiyo ilikuwa hatari , ambapo Marekani ilikuwa ikihimiza mgawanyiko kudhibiti mafuta yanayolengwa kutoka kwake kwa uwekezaji wake, pamoja na taasisi za Kiingereza na Ujerumani ambazo pia hupata masilahi yao katika kujitenga kwa mkoa tajiri - na kwa hivyo silaha ziliongezeka kwa Jenerali Agoku, na ndege za kivita zilikuja na mamluki wa Ulaya, na ilionekana wazi kuwa Nigeria ilikuwa imegawanyika,na imeisha.
Licha ya hali ngumu ambayo Misri ilikuwa ikipitia siku hizo na kushughulika kwa Abd El Nasser kwa kujenga upya vikosi vya jeshi vya kimisri katika maandalizi ya vita vya Ushindi, hakupuuza ujumbe wa Rais wa Nigeria, na haraka ilimwita mhusika wa masuala ya kiafrika-Mohamed Faik- akimwambia" Hatutaki kushindwa kwa Afrika kama tunavyo, akimfahamisha kuwa Nigeria haitapata wanahewa kutoka mahali pengine popote, na Misri yenyewe, wakati ilipopata kushindwa mnamo Juni, hakuna mtu aliyeitikia wito kama huo, basi kupeleka wanahewa ni jambo tofauti na kupeleka vifaa vya kijeshi, akimwonya kwamba serikali nchini Nigeria haitaweza kuvumilia na inaweza kushindwa na vikosi vya kujitenga, na huu ndio utakuwa mwisho wa serikali ya Muungano, basi Uhuru wa Biafra kwa njia hii ni kuunda taasisi mpya katika mkoa huo inayoweza kuchangia sawa na linalofanyikwa na Israeli huko Mashariki ya Kati.
akiongeza .. Marekani, kwa msaada wake kwa kujitenga, inataka kuzitisha serikali za Kiafrika ili ziwe chini ya udhibiti na utawala wa taasisi kuu za kibepari na kampuni. Silaha za Israeli zinaingia huko Biafra, na huenda hiyo ni mpango wa Marekani. lakini, Israeli yenyewe ina masilahi ya kugawanyika Nigeria, inayojumuisha kundi kubwa zaidi la Kiislamu barani Afrika, pamoja na faida za kiuchumi ambazo Israeli inataka kutimiza huko .. Misri haipaswi kuiruhusu liweke Afrika hivyo kwa sababu ya kile kilichotokea mnamo Juni 1967, na hiyo lazima iwe msingi wazi wa mkakati wetu. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa uamuzi: kusaidia serikali ya Muungano kupinga harakati za kujitenga huko Biafra na kudumisha Muungano wa Nigeria, kuitika ombi la Rais wake, na kupeleka wanahewa wanaohitajika.
Kwa kuzingatia kwamba hali wakati huo haikuruhusu Jeshi la Anga la Misri kuacha mwanahewa yeyote wa mapigano, Abd El Nasser alinipa jukumu la kuwa jambo hilo litatokea kupitia wanahewa wastaafu walioacha huduma ya jeshi la anga.Ofisi ya Masuala ya Kiafrika huko Misri iliwakusanya maafisa hawa na kuwaita kwa vikundi na ilikubaliwa na mamlaka za Nigeria kwamba shughuli hiyo ingefanyika kama aina ya itifaki kibinafsi kati ya watu binafsi na serikali ya Nigeria, ili kuepusha shida za kimataifa zinazotokana na uingiliaji wa moja kwa moja wa Misri. inayomaanisha ilikuwa kama aina ya mamluki wa Ulaya, lakini kwa kweli walikuwa mbali na kuelezewa kama hivyo.Ilikuwa serikali ya Misri iliyowapa kazi, kuandaa mkataba huu nao, na kumwita yeyote inayemtaka.
Kulikuwa na afisa wa mawasiliano wa Misri huko Lagos ambaye alikuwa akiwasiliana moja kwa moja na Ofisi ya Masuala ya Kiafrika huko Misri kupitia kila kinachohusiana na mambo ya watu hawa na akipanga kila kitu pamoja na mamlaka za Nigeria.nia ya maafisa hawa ilikuwa hasa kuhudumia malengo ya kitaifa ya Misri, malengo hayo ambayo yalikuwa sawa na maslahi ya Nigeria.
Muhammad Faik anaendelea na maneno yake, akisema: Bado nakumbuka mkutano wangu na kundi la kwanza la wanahewa niliowapokea kuwapa kazi hiyo na jinsi umakini wao ulilenga juu ya hamu ya kujua kiwango na jinsi matokeo ya vita hivi vya Nigeria yanavyotuathiri sisi na umuhimu wa hiyo kwa vita vyetu vikuu pamoja na Israeli bila mtu yeyote kuuliza mshahara au manufaa na faida watakayopata. Wengi wa wanahewa hao walirejeshwa katika Jeshi la Anga la Misri tena kama tuzo kwa kazi yao huko Nigeria.
Kundi la kwanza la wanahewa wa Misri, wakiongozwa na Luteni Kanali Taliaoui, walifika Lagos siku chache baadaye. Siku hiyo hiyo walipofika,walitumia pole pole ndege ya MiG, kwenye mji mkuu wa Nigeria. Na hiyo iliashiria mwisho wa utawala wa anga wa Agoku kikamilifu, kwani aina za ndege ilizotumia hazikuweza kukabiliana na MiG za Urusi ambazo zilitumiwa na wanahewa wa Misri. Wakazi wa mji mkuu, Lagos, walifurahi kuonekana kwa MiG angani mwao kwa furaha vigelegele, ambapo walikuwa wakiishi kwa hofu kutoka kwa uvamizi wa Agoku na mgomo wa anga ambao ulikuwa umeongezeka kwa kasi mnamo kipindi cha hivi karibuni.
Kazi iliyotolewa kwa wanahewa wa Misri ilikuwa kulinda anga za Nigeria katika maeneo yaliyoainishwa kwao, na vile vile kupiga uwanja wa ndege uliomiliki Biafra, na kuuharibu kikamilifu. iliyomaanisha kuzuia vifaa vya kijeshi kwa Biafra, ambavyo mara nyingi vilifika kwa ndege. Idadi ya wanahewa wa Misri nchini Nigeria iliongezeka na maendeleo ya vita na kuanzishwa kwa Kitivo cha ndege huko Lagos kuwafundisha maafisa wa Nigeria, na tulilazimika kupata wanahewa kutoka Jeshi la Anga la Misri kukamilisha idadi zinazohitajika, pamoja na wafanyikazi wa matengenezo, huduma ya ardhini na mawasiliano ya waya.
Wakati huo, haikuwa rahisi kumshawishi Luteni Jenerali Mohamed Fawzi, Waziri wa Vita, kukubali jambo hilo ila baada ya kukubali masharti yake kwamba wafanyikazi watabadilika baada ya miezi 3 na kuwa na haki ya kuwaita wafanyikazi wote wa Jeshi la Anga la Misri kwenye ujumbe huo ndani ya masaa 48. Na kweli Luteni Jenerali Mohamed Fawzi alitumia haki yake ya wito huo wakati vita vya uchochezi vilipoongezeka.
Kwa upande wa wanahewa , wale walio nje ya Jeshi la Anga la Misri walibaki, na ilibidi wafanye bidii maradufu. Na kudumu kuwepo kwa wanahewa wale hadi ushindi ulipopatikana na vikosi vya Muungano wa Nigeria, Agoku alikimbilia Ivory Coast, na vikosi vyake vikasalimu amri, na jaribio la kujitenga huko Biafra liliondolewa. bila shaka kwamba uamuzi wa Rais Gamal Abd El Nasser wa mapinduzi wa kuwapeleka wanahewa wa Misri huko Nigeria ulikuwa na ufadhili mkubwa katika kukata amri ya vita kwa upande wa vikosi vya Muungano.
Misri haikugharimia chochote kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono serikali ya Muungano wakati huo, ambapo serikali ya Nigeria ilikuwa ikilipia vifaa ambavyo ilipata kutoka Misri kwa sarafu ngumu, na vifaa hivyo vilikuwa sehemu za vipuri na ndege zingine ambazo zilitolewa na Jeshi la Anga la Misri, risasi, mabomu ya ndege na Vifaa vingine ambavyo vilikuwa rahisi kupatia tena kutoka Umoja wa Kisovieti.
Bei ilikuwa ililipwa wakati wa kupokea kwa Wizara ya Vita ya Misri, iliyokuwa ikitumia mapato haya kununua vifaa vyake kutoka kwa masoko ya Ulaya yanayohitaji sarafu ngumu, kama vile minyororo inayohitajika kwa utengenezaji wa gari la kivita lililotengenezwa na Misri na kununuliwa kutoka Uhispania. Serikali ya Nigeria ililipa mishahara ya wanahewa na mafundi wote wa Misri walioshiriki katika ujumbe huo, pamoja na mshahara wa usafiri wa anga uliohitajika kwa shughuli za kufufua haraka, na hiyo ilikuwa ikilipwa kwa sarafu ngumu .. ukiongezea kuwa, Misri ilisaini makubaliano ya kiuchumi pamoja na Nigeria yaliyotuletea faida kubwa.
Basi makubaliano pamoja na serikali ya Nigeria yalikuwa kubeba mzigo wote wa kifedha wa misaada ya kimisri, kwa kuzingatia hali ambayo Misri ilikuwa ikipitia suala la kujenga tena jeshi lake na hitaji lake la kukusanya rasilimali zake zote kwa vita vyake pamoja na Israeli, na kwa sababu Nigeria iliweza kulipa hilo halikuwa shida yake. Shida muhimu zaidi za Nigeria katika vita hivyo vilikuwa kwanza katika kupata ndege, silaha na vifaa muhimu, na vile vyote ilivipata kutoka Umoja wa Kisovyeti.
Hivyo ndivyo maoni yalikuwa wazi katika sera yake kuelekea Afrika,basi katika hali ngumu zaidi, Misri haikuacha kulisaidia Afrika, na ilikuwa inajua vizuri kuwa kile kilichokuwa ikifanya huko haikutenganishwa na vita vyake na vya Waarabu wote dhidi ya ukoloni na dhidi ya Israeli.
Picha nadra kadhaa zinaoneshwa kwa mara ya kwanza wakati wa ziara ya Rais Gamal Abd El Nasser huko nchi ndugu ya Nigeria mnamo Novemba 25, 1965.