Gamal Abdel Nasser na Utamaduni

Gamal Abdel Nasser na Utamaduni

Imeandikwa na / Amr Sabeh

Imefasiriwa na / Osama Mostafa Mahmoud

Mnamo mwaka 1969 , vita vya ugomvi kati ya Misri na Israel vilikuwa vikiendelea.Sherehe ya kumbukumbu ya miaka elfu moja ya kuanzishwa kwa mji wa Kairo iliwadia, na licha ya vita hivyo, sherehe kubwa ya kiutamaduni ilifanyika kuadhimisha siku hiyo ambayo haitarudiwa tena hadi baada ya miaka elfu moja, na mwanzo wa sherehe ulikuwa ufunguzi wa Maonesho ya Vitabu ya Kimataifa ya Kairo kama maonesho ya kwanza ya vitabu ya Misri, Kiarabu na Kiafrika.

Wakati wa utawala wa Gamal Abdel Nasser, Wizara ya Utamaduni na Baraza Kuu la Sanaa na Fasihi zilianzishwa, ambalo jina lake lilibadilishwa kuwa "Baraza Kuu la Utamaduni."Na Mamlaka ya Vitabu vya Jumla ilianzishwa, na Nyumba ya Vitabu na Nyaraka za Kitaifa ilitengenezwa na kuhamishiwa kwenye jengo lake la kisasa kwenye Nile Corniche mjini Kairo.Chuo cha Sanaa pia kilianzishwa mnamo 1959 na taasisi zake maalum za kiufundi, na jumba la opera. vikundi kama vile Kairo Symphony Orchestra, vikundi vya muziki wa Kiarabu, na sarakasi, ukumbi wa michezo wa kitaifa na wa vikaragosi, na ukumbi wa Sayed Darwish katika chuo hicho kufanya matamasha, na msingi uliwekwa kwa kikundi cha makumbusho ambayo inachukuliwa kuwa moja ya makumbusho makubwa zaidi ya Misri hadi sasa, na maendeleo ya tambarare ya Piramidi ilianza na maonesho ya sauti na mwanga na boti za jua ziligunduliwa, na mahekalu ya Philae na Abu Simbel na mambo ya kale ya Misri huko Nubia yaliokolewa, Mamia ya majumba ya kiutamaduni yalianzishwa. miji, vituo, na vijiji, na mamlaka ya utamaduni wa watu wengi ilianzishwa.Maelfu ya vitabu vilichapishwa kwa bei nafuu chini ya jina la Mradi wa Vitabu Elfu sehemu ya kwanza, na kisha Mradi wa Vitabu Elfu sehemu ya Pili.

Hayo yote yameandikwa na tarehe, lakini si muhimu madamu  kurasa zilizofadhiliwa za  Hazoumbel mfuasi wa the Brotherhood, mwengine Shakshak wa kiliberali na Shawkat al-Shamasherji kwenye Facebook na Twitter zinapiga kelele mchana na usiku kwamba Gamal Abdel Nasser alikuwa adui wa utamaduni na wasomi, tena hata hakuwa msomi.