Malengo ambayo hayafikishwi na heshima na hadhi hayalingani na shida ya kupambana kwake
Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
Enyi Wananchi:
Mwenyezi Mungu asifiwe, maana hilo ndilo Bwawa la Juu; Bwawa lenu refu, ambalo mmelisubiri tangu muda mrefu na kulifanyia kazi.Hilo ndilo bwawa refu ambalo taifa zima la kiarabu, ikiwemo watu wa taifa mbalimbali, limefanya juu chini ili kuliona likifikiwa. jambo ambalo linanifurahisha na kutufuraisha sisi sote Katika hafla hii, Mheshimiwa Mfalme wa tano Mohammed " Mashangilio" . katika maadhimisho hayo anashirikiana nasi , Mheshimiwa mfalme Muhammed wa Ufalme wa Morocco; Ambayo ilihangaika pamoja na uongozi wake kwa ajili ya uhuru wake, hadhi yake , na iliweza kupata, na mwishowe iliweza kuzipata.
Enyi Ndugu :
Hili ni Bwawa la Juu , ambalo vita vilifanyika karibu nalo, na ambalo mashujaa walipigania kwa ajili yake ، hili ni Bwawa la Juu ambalo limeshuhudia juhudi hizi zote na kilistahili juhudi hizo siyo kwa sababu uthamini binafsi wake tu , bali kwa sababu ya maana yake kama mfano wa kutilia mkazo kwa taifa ya kiarabu zima ili kuendeleza nchi mkubwa zake zilizopata uhuru .
Wale ambao walipigana - enyi ndugu - ili kufikia tumaini, na wale ambao walijitahidi kugeuza tumaini kuwa ukweli, na wale ambao hawakutishwa na moto na chuma, hawakufanya yote hayo ili kuchomoa ekari milioni au milioni mbili kutoka kwa makucha ya jangwani tu , wala kupata tu kilowati milioni 10 za umeme , bali walifanya hivyo ili kutimiza nia yao ya kujitegemea, ambayo waliipokonya kutoka katika mtego wa dhuluma, Ukoloni , unyanyasaji, na udhibiti. Hakuna shaka- enyi ndugu - kwamba ardhi mpya ambayo tutapata kutoka Bwawa la Juu ni lengo muhimu sana, kama vile hakuna shaka kwamba umeme tutakaopata kutoka Bwawa hilo ni lengo lingine muhimu sana, lakini Thamani kubwa ya Bwawa hilo ni thamani yake kama dhamira, nia na utashi mzito , uthamini mkubwa wake ni dhamira ambayo wenyeji wake walisisitiza baada ya kuwa wameiweka wazi njia yao na kuitambua na kuiazimia , na wakaazimia kwamba heshima na hadhi ziwe njia yao kwake , si udhaifu, uchovu, wala kuachwa.
Na nakumbuka - wananchi wenzangu - nilipotaifisha mfereji mnamo mwaka wa 56, na wakati kulikuwa na matatizo makubwa yaliyotukumba wakati wa kujenga Bwawa la Juu, na nilipozungumza nanyi kutoka Alexandria wakati wa tukio hili, nakumbuka kwamba nilikuambieni kuwa tutajenga Bwawa la Juu, lakini kabla hatujajenga Bwawa ni lazima tujenge Bwawa la heshima , Uhuru na hadhi na tutapojenga Bwawa la heshima , Uhuru na hadhi inapaswa basi tumaini litimie, na lazima tujenge Bwawa la Juu .. Mmesha jenga - enyi raia ndugu - bwawa la heshima , Uhuru na hadhi kwa juhudi , mapingano , subira , azimio , nia yenu na kutohofia .. kutohofia kutoka nchi kubwa na vitisho vyote ,na mlishinda vita vya kujenga Bwawa la heshima , Uhuru na hadhi.. na Leo - ndugu - mmeshinda kujenga Bwawa la Juu.
Malengo - Enyi ndugu - ambayo hayatekelezwi kwa heshima na hadhi hayalingani na shida ya juhudi ya kuyafikia kwani njia tunayofuata kuelekea lengo letu lazima ilingane katika umuhimu wake na malengo hayo, na jambo kubwa ambalo lilikuwa ni dhamira kuu la kufanikiwa kwa waarabu wetu kufanikiwa ni kuchagua njia ngumu zaidi, si kwa sababu ndiyo njia ngumu zaidi, ila kwa sababu ndiyo njia bora zaidi, iliyo sahihi zaidi, na inayoendana zaidi na lengo tunalotafuta ,Thamani yake kubwa ni kwamba nia ambayo wamiliki wake waliyokomboa, kisha wakauheshimu, kisha wakaazimia kutembea katika njia yake, kisha wakaazimia kuufanya uhuru huu kuwa hai.. endelevu.. nishati inayowaka. hawakuisitishwa baada ya kupata uhuru bali waongozwa nayo na iliongozwa nao kwa ajili kuandika karatasi nzuri mno katika historia ya juhudi zao , Wanakabiliwa na zama ya ujenzi ili kurekebisha maisha yao kwa msingi wanaoukubali hivyo baada ya kuishi kwa muda mrefu katika maisha illiwalazimisha kwa kuweka masharti ya udhibiti wa ndani na nje.. udhibiti wa ndani na wa nje .. udhibiti wa ndani unaotumiwa vibaya na udhibiti wa nje wa kidhalimu. Thamani yake kuu - ndugu - ni kwamba muundo ambao uliangaza uwezo wetu wa kupinga, na tukashinda, na tukathibitisha kwamba tunaweza kustahimili machangamoto, na tukastahimili mbele ya machangamoto, tukaishi wakati wake, kisha tukaishi baada yao; Tulistahimili uchokozi na kuishi kipindi cha uchokozi, kisha tukaishi baada ya uchokozi ili kufikia lengo ambalo tuliazimia, na ili kujenga nchi zetu katika nusu ya pili ya karne ya ishirini kwa njia ya nusu ya pili ya karne ya ishirini.
Hiyo - Ndugu - ndiyo Thamani kubwa kwa Bwawa la Juu kwa taifa zima la Kiarabu. raia huweka sanamu ya kumbukumbu kwa kuhifadhi tukio la ushindi wao mkubwa, na tunazingatia kuwa bwawa kuu ni ukumbusho wa Vita vya Waarabu, na uzinduzi wa utaifa wa Kiarabu ili kufikia jukumu lake la kihistoria na kibinadamu.. Ni ukumbusho-ndugu- Inalingana katika ukubwa wake, katika manufaa yake, na athari zake, pamoja na kadiri ya taifa lililoiunda.Ni ukumbusho hai na wenye ubunifu na sio tu jiwe kiziwi ambalo maua hutupwa pembezoni mwake mnamo maadhimisho , Ni maisha mapya yaliyofanywa upya, Ni nguvu inayohimiza maendeleo , msaidizi , nguvu na uundaji mkono Katika vita vikubwa na njia ndefu ili kufikia malengo makubwa ya Kiarabu, pia ni motisha inayoendelea ambayo inakumbusha taifa letu kwamba hakuna jambo gumu la kulifikia au haliwezi kulitarajia, iwapo litaamua, kutaka na kuazimia, bali tuna imani kwamba Bwawa hilo kuu litakuwa kichocheo endelevu kwa mataifa mengi zaidi ya taifa letu la kiarabu . Mataifa mengi Barani Afrika, ambayo mto huu mkubwa unatoka moyoni mwao, na huko Asia, ambako Jamhuri yetu ya Muungano wa Kiarabu yenye ushindi inaenea.
Na nakumbuka – wananchi wenzangu – tulipokumbana na vikwazo kwa ajili ya kujenga bwawa hilo kuu , na ilipoonekana kwa ulimwengu wote kwamba hatuna njia ya kulijenga bwawa hili kuu ambalo tulitangaza azimio letu la kujenga, na. nilipokuambeni hivyo, na nilipokuombeni nyote tutoe jasho , damu na roho kwa ajili ya kufikia lengo hili, na nilipokuombeni tujitegemee sisi wenyewe, azimio letu na nguvu zetu, na wakati picha ilionekana mbele yetu picha ya giza tupu ; Matumaini yalijaa mioyoni mwa watu hawa, na nilipotoka baada ya kutoa hotuba hii, palikuwa na kelele kubwa ikaenea baina ya hadhira katika Alexandria kote, na kisha kati ya maeneo ya Kairo na Sehemu zote za nchi ambazo nilizifika au kuzitembelea wakati wa safari yangu kutoka Alexandria hadi Kairo, na kelele hii kuu ilikuwa ni onesho la matumaini na onesho la kuazimia na nia; Kila mtu alikuwa yupo kila mahali, na umati katika kila mahali walikuwa wakiimba kutoka ndani ya mioyo yao kwamba tutajenga bwawa hili. na imekuwa neno la umma balu imekuwa wimbo wa kitaifa.. " tutajenga Bwawa .. tutajenga Bwawa kwa juhudi zetu na miyoyo yetu " .
Na leo - ndugu - matumaini haya yanaonekana, leo - ndugu - nami ninaposema kubwa Jamhuri ya Kiarabu iliyoshinda; Ninamaanisha tu kwamba matumaini yenu yameshinda, azimio lenu limeshinda, juhudi zenu zimeshinda, na roho ya juu ambayo mlikabiliana nayo siku hizi ngumu, na roho ya juu ambayo mlikabiliana nayo tishio na kuzingirwa, roho hii inavuna matunda yake leo, hupata leo kwenye mahali hapa - kusini mwa mbali kutoka eneo la kusini la Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu - unapata ishara ya utambuzi wake, unapata ishara ya utekelezaji wake, na unapata ishara ya nia yake , unapata ishara hii ya kuanza kujenga Bwawa hilo kuu .
Enyi Ndugu wananchi:
Kazi hii - kama nilivyokuambeni - ina maana kubwa, ina maana muhimu nayo ni kwamba mataifa, hata yawe madogo kiasi gani, yanaweza kufanya matendo makuu... yanaweza kuyafanya matendo hayo , ikiwa nia yao ikiungana , yakichukua maamuzi mazito , yakaazimia na yakifanya juu chini kwa ajili ya kuyafanya malengo yake yatekelezwe. Na ninyi - ndugu - kwa kazi hii kubwa; Kwa subira hii, kazi, azimio na juhudi , mlitoa mfano kwa Dunia nzima kwamba mataifa madogo yanaweza kutekeleza nia yao licha ya utashi wa mataifa makubwa na licha ya nia ya wanyanyasaji na dhulma ya nje. nchi zinazoendelea zikiandaa , kuazimia na zikiazimia kujitolea kwa roho na damu yake kwa ajili ya malengo makubwa yake ; zitaweza kufikia malengo yake makubwa licha ya meli, licha ya ndege, licha ya uchokozi, licha ya tishio, licha ya kizuizi, na licha ya kurasa za giza zinazotuzunguka.tuliweza Kwa subira na juhudi zetu , tuliweza kwa dhamira yetu ya kuweka nia yetu katika njia ya kuondoa giza hili, kusitisha uchokozi huo, na kuendelea na safari yetu ili kuona lengo kubwa ambalo tulilifanyia kazi linaibuka na kutekelezwa.
Huu - Enyi ndugu- ni mfano kwa nchi zote ulimwenguni kote .Bwawa Kuu tunaloanza kulifanyia kazi leo ni kichocheo endelevu kwa mataifa yote Barani Afrika na Asia. linakumbusha daima kwamba raia wadogo, bila kujali kiwango cha vifaa vya uharibifu wa atomiki wanachokimiliki ni kidogo kiasi gani , wanaweza daima kufanya kazi kubwa zaidi za ujenzi, na wanaweza - ikiwa ni lazima - kuchimba njia yao wenyewe, hata kwa kucha zao.. wanaweza kuchimba njia hili hata kwa kucha zake , na kwa damu yake kati ya mawe.
Raia wetu- enyi ndugu-wameweza, na wao si watu wenye nguvu zaidi ya kwa silaha, na wala sio matajiri wenye pesa ... waliweza kujenga Bwawa kubwa zaidi Duniani na katika historia na kufanya hivyo wakati wa kipindi kigumu mno na kati ya hatari iliyopelekea vita vye ukatili mkali wakati ambapo walibeba silaha na kujiandaa kupambana na walishinda . Baada ya hayo, -enyi ndugu-, majaribio mengi yalifanywa ili kulishinda, majaribio ya kuuzunguka. Kuuzunguka mpaka kufikia kile ambacho silaha hazikuweza kufikia, labda njaa - Enyi ndugu - ingevunja azimio lake, na labda njaa ingefikia kile ambacho silaha hazikuweza kufikia. Lakini watu wenye idadi ndogo..watu wenye idadi ndogo ndogo waliweza kushinda katika vita vya silaha na kulazimisha nguvu za uchokozi kurudi nyuma kwa kushindwa, na kushushwa bendera chini, basi waliweza pia kushinda katika vita vya njaa, bali waanza mnamo kipindi kigumu chake zaidi hatua zake za kwanza katika njia ya viwanda.
Na sote tunajua - Enyi wananchi wenzetu - kwamba tuliamua wakati tunakabiliwa na kuzingirwa, na tunapokabiliwa na vita vya njaa, kuanzisha mradi wa miaka mitano wa viwanda, na tuliamua kuwekeza Paundi milioni 303 kwa ajili ya viwanda, kisha tuliamua licha ya hali hizi zilizotuzunguka, na ambazo zilikuwa zikitokea pembezoni mwetu; hali ya kizuizi cha kiuchumi na kufungia kwa fedha zetu - hali ya njaa na hali ya shinikizo - kwamba tunapunguza muda wa miaka mitano ili kukamilisha mradi wa miaka mitano katika miaka miwili, na tuliweza ingawa haya yote kushinda na kutekeleza nia yetu ; kwa sababu nia yetu imekombolewa, na kwa sababu tumejenga Bwawa kuu kwa heshima , uhuru na hadhi. tuliweza mnamo siku hizi kusonga mbele katika maendeleo ya viwanda, na vitisho havikutishi, kuzingirwa hakukutisha, na njaa haikututisha, na tuliweza mnamo kipindi hiki kilichopita, ambacho kilikuwa moja ya nyakati ngumu zaidi kwa taifa letu; kufikia kazi kubwa zaidi , na kuendelea katika njia yetu ili kufikia lengo kubwa ambalo tuliazimia kufikia.. Lengo hili ni Bwawa Kuu.
Na tulitembea- Enyi ndugu-pia katika njia ya kuanzisha uchumi uliokombolewa kwa upande wa misingi yake katika misingi mikuu na imara zaidi.Hatukutishika na tishio hilo, wala uchokozi huo haukututisha kwa kuamua tutekeleze nia na utashi wetu kwa vitendo. kwa uchumi wetu uwe huru, wa kizalendo, na wa Kiarabu ulio huru; kwa hiyo tuligeuza makampuni ya kigeni yaliyokuwa yanadhibiti uchumi wetu yawe ya kiarabu, tukayafanya mabenki yawe ya kiarabu na hata tuliyataifisha, na tukayafanya makampuni ya bima kuwa ya kiarabu na kuyataifisha, kisha uchumi wa taifa katika nyakati hizi ngumu - uchumi uliokuwa unatawaliwa na mgeni. ukawa uchumi wa taifa unaotokana na utashi wa watu hawa, na tulipitia nyakati hizi ngumu na nyakati hizi ambazo tulikuwa tunapigania kwa ajili ya uhuru wetu; Tulitembea bega kwa bega ili kupigania uhuru na ukombozi, kisha kuzuia uchokozi na kuwashinda wavamizi, kisha kujenga uchumi uliokombolewa wa taifa la kiarabu, basi tulikuwa tunatazamia mbele mpaka tulione bwawa hili ambalo vita vilianza kwa ajili yake .. Tunaliona. kama ukweli uliopo katika hali halisi .
Leo - enyi ndugu - tuna haki ya kujivunia; kwani tuliweza kupata uhuru, kisha tukaweza kuthibitisha uhuru huu, halafu tukaweza pia wakati huo huo kuangamiza uchokozi; Uchokozi wa mataifa makubwa, ndipo tulipoweza pia kuendelea katika mipango ya maendeleo ya viwanda, na tukaweza kuanzisha uchumi wa taifa uliokombolewa wa taifa la Kiarabu, kisha tukaweza pia kutembea katika njia yetu ya kuiendeleza nchi yetu, basi leo - enyi ndugu - tunaona kwamba tunafikia lengo ambalo tulitarajia kufikia mwaka wa 56; Tunaona kwamba tunafanikisha Bwawa kuu , jengo hilo kubwa, jengo kubwa, jengo ambalo ni onesho la ushindi wa dhamira yenu na ushindi wa utashi wenu.
Hivyo - Enyi ndugu - raia walishinda; walishinda kwa ajili yake wenyewe na kwa ajili ya taifa lake, kisha akashinda kwa mataifa mengine mengi katika Afrika na Asia ambayo yanakabiliwa na vita vikubwa vya uhuru, na kukabiliwa na vita vya baada ya uhuru kwa ajili ya kujenga, vilevile, walishinda katika vita vingi vinavyofanyika katika ulimwengu wa Kiarabu kote ili kuhifadhi utaifa wake, na ili kuhifadhi haki yake ya maisha ya uhuru; Vita hivi vinavyoanzia Ghuba ya Uarabuni hadi Magharibi ya kiarabu.. Vita hivi vinavyoanzia Oman kwenye Ghuba ya Uarabuni hadi Algeria katika Magharibi ya kiarabu. vita hivi mlivyopambana kwa ajili yake , ambavyo mlibeba daima bendera yake, na ambayo nyinyi nyote mmetangaza kwamba mnawaunga mkono wanawe Waarabu , kwa damu zenu, fedha zenu, na nafsi zenu, vita hivi vinavyoenea katika Palestina ya kiarabu ili kuhifadhi utaifa wa kiarabu kutoka hasara na kuporomoka, vita hivi ambavyo kila mwananchi wa raia hawa anajua ni vita yake; Vita vyovyote katika sehemu yoyote katika taifa la Waarabu ni vita vyetu na vita vya kila mmoja wetu.
Kwa mshikamano huu na kwa umoja huu - enyi ndugu - tunaweza kushinda na hatuwezi kusahau kwamba watu wa Kiarabu katika Sehemu zote za Kiarabu, kutoka Ghuba ya kiarabu hadi Bahari ya Atlantiki, wametuunga mkono katika vita vyetu na kusimama nasi katika vita vyetu. Kila mwananchi wa taifa la Kiarabu alihisi kwamba hii Vita ni vita vyake. Nami naamini moyoni mwangu - wananchi wenzangu - kwamba kila mtu mmoja wa wana wa taifa la Kiarabu katika sehemu zote za taifa la Kiarabu anahisi leo kwamba kujenga bwawa hilo ni ushindi kwake, ushindi kwa utashi wake , ushindi wa juhudi zake . na ushindi kwa uungaji mkono wake kwa wana wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu wakati walipopigana uchokozi, na walipopambana na kizuizi cha kiuchumi, na walipoazimia kuendelea katika vita vyao hadi ushindi.
enyi ndugu wananchi:
Hii ndiyo thamani kubwa kwa Bwawa Kuu. Thamani yake kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, thamani yake kwa taifa zima la Kiarabu, thamani yake kwa mataifa ya Afrika na Asia. Na sisi hapa leo, tunasherehekea kuanzisha kwa ujenzi wa Bwawa kuu, na tunasherehekea kwa kuridhika ambayo haijachoshwa kwa majivuno au kiburi.. tunasherehekea kwa ridhaa inayotusukuma kwa hatua pana na haituathiriki kwa udanganyifu au kiburi, tunaisherehekea sisi wenyewe na tunaisherehekea kwa ajili yetu tulioijenga na kwa wale ambao Bwawa Kuu litabaki mbele yao Mfano wa kudumu tunausherehekea - enyi ndugu- na dhamira inatujaza miyoyo yetu kwa heshima kwa wale walitusaidia Kwa sababu walitusaidia kujenga, na tunaisherehekea bila chuki dhidi ya wale waliopigana nasi; hii ni kwa sababu walitupa fursa ya kushinda, na ushindi wetu utujitegemee sisi wenyewe. Azma yetu ya kuijenga sisi wenyewe katika nchi yetu iliyokombolewa, azma yetu ya kufuata njia tuliyoitaka kwetu wenyewe.
Sisi - enyi Ndugu, tunaposherehekea ujenzi wa Bwawa Kuu, lazima tuitaje nchi iliyokubali kutusaidia katika kazi hii. ilitusaidia kwa mkopo ili tujenge, halafu ikatusaidia kwa msaada wa kiufundi ili kujenga.. Hiyo ni Umoja wa Soviet . Na msaada wa Umoja wa Kisovyeti kwetu kwa kutupa mkopo wa kujenga awamu ya kwanza ya Bwawa Kuu, na msaada wa kiufundi katika ujenzi wa Bwawa Kuu, ulikuwa msaada wa dhati na usio na masharti, msaada unao urafiki na mapenzi ambayo yanaunganisha watu wa Kiarabu na Watu wa Sovieti, na msaada wao kwetu ulikuwa wa dhati isio wa kifani , bila vizuizi vyovyote wala sharti, tena hakuna shida au uchovu, nami nachukua fursa hii ili kutoa,- kwa niaba yenu - kwa jina la serikali na katika jina langu mwenyewe - shukrani kwa watu wa Umoja wa Kisovyeti na Serikali ya Umoja wa Kisovyeti kwa msaada huu. Pia natoa Shukrani zangu kwa mafundi wanaofanya kazi nasi kutoka Umoja wa Kisovieti ili kazi hii iendelee, na kwa ushirikiano wao pamoja na wahandisi waarabu wenzao kwa misingi ya urafiki, upendo, na azimio la kukamilisha kazi hii kwa haraka kadri iwezekanavyo.
Pia nachukua fursa hii ili kutoa shukurani zetu kwa wahandisi wote waarabu na wafanyikazi waarabu ambao walianza kazi ya bwawa hili na ambao watalifanyia kazi kwenye bwawa hili hadi litakapotekelezwa na hadi kukamilika, na raia waarabu wote . Sisi sote tunawatazama kwa shukrani, uaminifu na shukrani, vilevile , nachukua fursa hii ili kuwapa na shukrani na heshima zetu za dhati.
Enyi ndugu wananchi:
kipindi hiki , ulimwengu unapitia awamu muhimu katika historia yake.. unaelekea kwenye amani na maelewano, na unaelekea kuangalia nchi zilizokosa fursa zamani, nasi tumechangia katika kuunda anga hii; kwa sababu tulithibitisha kwa dhamira, azimio na utashi wetu kwamba sera ya madaraka iliyofuatwa katika karne ya kumi na tisa haiwezi kamwe kufanikiwa katika karne ya ishirini, na tulithibitisha kwa ujasiri wetu wakati wa uchokozi wa pande tatu ulioikumba nchi yetu, na kisha tukathibitisha kwa dhamira yetu halafu kwa kutekeleza muundo huu katika ujenzi wa Bwawa kuu, kwamba nchi ndogo haziwezi kushindwa ikiwa nia yao yameunganishwa na ikiwa dhamira yao ni ya kweli, na nia yao na dhamira yao yameunganishwa ili unatetea uhuru. wa nchi yako, na unatetea uhuru wa nchi yako dhidi ya uchokozi na uvamizi, nanyi mlishinda na neno lenu limekuwa moja na azimio lenu limeunganishwa kujenga Bwawa Kuu ambalo tulikabiliana na vikwazo vyote Ili kulijenga, azimio lenu lilishinda na kutekelezwa..na mlijenga Bwawa kuu.
Kwa hili - enyi wananchi wenzako - mliwekeni kanuni mpya katika karne ya ishirini; Kanuni hii ni kwamba mataifa madogo hayawezi kwa hali yoyote kuacha utashi wao wa uhuru au kuacha azimio lao , ikiwa yakiazimia, yatakwenda katika njia yao hadi mwisho ili kufikia lengo wanalotamani, na kwamba njia zilizofuatwa katika karne ya kumi na tisa kwa udhibiti wa nchi kwa nchi nyingine - Nchi kubwa juu ya nchi ndogo - lakini hizi ni mbinu hazina faida na haiwezekani kwa watu kuzikubali, bila kujali silaha zao ndogo.
Mlithibitisha - enyi ndugu - kwa ajili ya kutetea uhuru wenu jinsi mataifa madogo yanatetea uhuru wao, basi mlithibitisha - enyi ndugu - kwa ajili ya azma yenu ya kujenga bwawa hili jinsi mataifa yanaweza kutekeleza nia yao kwa vitendo. Leo, tunapokabiliana na hatua hii mpya katika historia ya ubinadamu na ulimwengu kwa ujumla, na leo tunaposubiri viongozi wa mataifa makubwa duniani kukutana, tunajua kwamba tumeweka na kuanzisha kanuni kuu na ya hali ya juu. ; nayo Ni kwamba nchi ndogo zitaenda katika njia zao wenyewe, ambayo ni kwamba nchi ndogo zitafanya kazi kwa ajili ya kuendeleza uchumi wao.
Leo - enyi ndugu - tunajisikia fahari kwamba mataifa makubwa yameanza kuhisi na kuona kwamba mataifa hayawezi kunyenyekea, hayawezi kukubali udhibiti au dhuluma, hayawezi kuwa ndani ya maeneo ya ukoloni na hayawezi kuwa mashamba ya malighafi, lakini yanataka kuchukua jukumu lao ulimwenguni kote kisha jukumu lao maishani. Leo tumethibitisha hili na tukahisi kwamba nchi zote zilichukua hili.. Walichukua somo hili ambalo tulithibitisha kwa ulimwengu wote katika mapambano yetu ya uhuru wetu na kwa ajili ya kujenga Bwawa kuu, somo hili ambalo tupoteza kwa ajili ya kulifanikisha na kuonyesha mashahidi na damu, lakini tunahisi kwamba somo hili tumehudumia wanadamu wote. Ubinadamu huwa unaunganishwa na unategemeana, na hauwezi kutenganisha watu hauwezi kubagulia, na haiwezekani kwa baadhi ya watu kuwa na haki ya maendeleo na maisha ya ustawi, na kwa wengine haki hii inachukuliwa kutoka kwao. na hawana haki ya maendeleo na hawana haki ya kuishi katika jamii ya ustawi. leo tunajivunia kubwa tulipambana na tulithibitisha ulimwenguni kote somo kubwa hilt na tutaendelea katika njia yetu , tunategemea mwenyezi Mungu , juu ya umoja wetu, na juu yetu wenyewe, na mwenyezi Mungu ndiye mpatanishi.
Amani na rehema za Mungu zikufikeni.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser mjini Aswan wakati wa kuanzisha kwa ujenzi wa Bwawa la Juu.
Mnamo Januari 9, 1960.