Siku ya Kazi ya kibinadamu Duniani 

Siku ya Kazi ya kibinadamu Duniani 

Siku ya kazi ya kibinadamu Duniani ni kampeni inaandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya  kuratibu Masuala ya Kibinadamu, kulingana na  ilivyoainishwa na Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa, ikizingatia siku ya Agosti 19, Siku ya kazi ya kibinadamu Duniani tangu 2008, Siku hiyo ni kama kumbukumbu ya wahanga wa shambulio la Mkusanyiko wa Umoja wa Mataifa huko Baghdad mnamo Agosti 19, 2003,  lililosababisha kifo cha "Sergio Vieira de Mello, Kaimu" Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa niaba  huko Iraq na wengine ishirini na mbili,  wakati ambapo, karibu na wafanyakazi 5,000 katika uwanja wa kibinadamu waliuawa, kujeruhiwa, au kutekwa nyara.

 Umoja wa Mataifa na Taasisi shirikishi zalenga kusaidia takriban watu milioni 160 katika nchi 56, ambazo ziko na haja kubwa la misaada , pamoja na kusaidia wale wote wanaofanya kazi kwa ajili ya heshima na haki za binadamu na watetezi wake Duniani, ili kukuza ufahamu wa umuhimu wa haraka wa misaada ya kibinadamu Duniani kote. 

Maudhui ya mwaka huu inakuja pamoja na kauli mbiu "Mkono mmoja haupigi makofi," ikisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja na kuimarisha muungano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto za kimataifa, mahitaji, na migogoro inayowakabili wanadamu, hivyo tushirikiane pamoja kupunguza mateso na kuleta matumaini.