Siku ya Kimataifa ya Upinzani wa vita na Ukoloni
Imetafsiriwa na/ Rahma Ragab
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Historia ya mapambano ya watu imetufundisha kwamba hakuna mtu anayeweza kuheshimu utu wake na heshima yake, na kupenda familia yake, nyumba yake na nchi yake, anaweza kunyamaza na kusimama bila kujali mazoea ya ukali, vita vya mauaji ya kimbari, ugaidi na ukoloni wa makazi na kuyazingatia hayo yote ni sera rasmi. Kwa hivyo, ulimwengu unasherehekea Siku ya kimataifa ya Upinzani Vita na ukoloni kila Septemba 27. Utangulizi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa unasisitiza kutotumia nguvu za kijeshi, isipokuwa kwa manufaa ya pamoja, na Kifungu cha 2 kinataja kutatua matatizo ya kimataifa kwa njia za Amani na kuzuia nchi wanachama kutishia kwa nguvu au kuitumia. Kwa hivyo, mkataba huo unakataza vita na hautambui uhalali wa ukoloni.
Siku hii inakuja wakati kuna mvutano na msukosuko unaokua katika siasa za nchi nyingi duniani. Kwa hivyo, mashirika ya haki za binadamu yanajitahidi sana katika siku hii kuhimiza mshikamano kati ya vikundi tofauti vya jamii na kueneza misingi ya maisha ya pamoja kwa wote bila kujali Imani zao au asili yao. Pia inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi kwa ajili ya ustawi wa watu, kuchukua hatua dhidi ya ugaidi wa ndani na wa kimataifa kwa aina zake zote, na kupambana na uhalifu uliopangwa na uliokiuka njia zote.
Mashirika ya haki za binadamu pia yanajitahidi kupunguza kueneza silaha na kutafuta kukomesha silaha za maangamizi makubwa, hasa nyuklia, kemikali, na hata silaha ndogo ndogo. Pia inafanya kazi ili kulinda utoto na kukuza dhana za amani kati yao na kuzuia kutangaza aina yoyote ya ukali, ikiwa ni pamoja na silaha, na kuzibadilisha na vitu vyema na vya usalama zaidi vinavyoonesha upendo na Amani kama vile maua.
Kwa upande mwingine, sheria ya kimataifa imetambua harakati za ukombozi wa kitaifa na imezilazimisha nchi kuzilinda na kuzisaidia katika mapambano yake halali dhidi ya ukoloni. wakati vita vilikuwa halali kama njia ya kutatua migogoro ya kimataifa, Vita vya harakati za ukombozi wa kitaifa vimepitia hatua kadhaa kati ya marufuku na ruhusa, Lakini baada ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia (1939-1945), kuzuia vita na kuviharamisha na kuanzisha "Umoja wa Mataifa" ikawa moja ya sifa muhimu zaidi za karne ya 20.
Umoja wa Mataifa umepiga hatua kubwa katika suala hili, mnamo mwaka wa 1949, ulipitisha "Mikataba nne ya Geneva ," ambapo (mkataba wa nne) unashughulikia ulinzi wa raia, jambo ambalo limeupa umuhimu mkubwa katika sheria ya kimataifa ya uwanja wa kibinadamu.
Hatimaye, kila ukoloni unasababisha upinzani, na ukoloni unapoongezeka, upinzani unakuwa mkali na mpana zaidi. Kwani Kukataa ukoloni, kuupinga na kupigana nayo ni lazima ili kuadhibu mvamizi na kumlazimisha kulipa fidia kwa hasara alizozisababisha kwa watu waliokaliwa. Kuendelea kwa ukoloni hufanya upinzani ni jibu halali kwake, na hakuna njia mbadala isipokuwa kujiondoa kikamilifu, kulipa fidia kwa hasara, kuvunja makazi ya ukoloni, na kurejesha ardhi na haki zilizopotea. Kwa hivyo, Mkataba wa Umoja wa Mataifa una vifungu wazi na vya moja kwa moja vinavyoharamisha vita na kuzuia nchi wanachama kutumia nguvu au kutishia kuitumia katika mahusiano ya kimataifa.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy