Siku ya Kimataifa ya Kulinda Elimu

Imetafsiriwa na/ Toka Ashraf
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Mei iliyopita, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikubali uamuzi wa kufanya septemba 9 ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Kulinda Elimu kutoka kwa mashambulizi yanayotokea katika maeneo haya ya mapigano, ambapo zaidi ya watoto milioni 75 duniani kote wanateseka kutoka mapigano yanayotokea huko nchini.
Siku hii ilikuja kama hatua ya kusitisha vurugu linalofanywa dhidi ya watoto hao na taasisi zao za kielimu zinazoshambuliwa na mashambulizi ya kigaidi na zinazotumiwa kwa malengo ya kijeshi. Siku hii inaangazia umuhimu wa kuhakikisha mazingira yenye usalama kwa elimu wakati wa dharura ya kibinadamu na migogoro inayokabiliwa na nchi.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy