Siku ya kupamba Biashara Haramu ya Binadamu Duniani

Siku ya kupamba Biashara Haramu ya Binadamu Duniani

Imetafsiriwa na/ Neema Ibrahim
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 
 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza kuwa, Julai 30, ili kuadhimisha "Siku ya kupamba Biashara Haramu wa Binadamu Duniani"  ili kuimarisha ufahamu wa hali ya wateswa wa Biashara haramu wa binadamu na kukuza haki na ulinzi wao, Biashara haramu ya binadamu ni uhalifu mbaya na ukiukwaji wazi wa haki za binadamu, unaoathiri maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wanaokuwa wateswa wa wasafirishaji haramu katika nchi zao na nje.

Biashara haramu wa binadamu unafafanuliwa kama "kuajiri, kusafirisha, kuhamisha,  kuhifadhi au kupokea watu kwa njia ya tishio ya nguvu au kuitumika au aina zingine za kulazimisha, unyakuaji, udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka au hali ya udhaifu, au ya kutoa au kupokea malipo au manufaa ili kupata kubali kwa Mtu anaye udhibiti juu ya mtu mwingine kwa ajili ya unyonyaji, Unyonyaji unajumuisha, kwa uchache, unyonyaji wa ukahaba  wa wengine au aina zengine za unyonyaji wa kingono, kazi ya kulazimishwa, utumwa au vitendo vinaendana na utumwa, au kuibia vitungo. 


Kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Kazi Duniani, idadi ya wateswa wa biashara haramu ya binadamu inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 40 duniani kote, ikiwemo watu milioni 25  wanalazimishwa kazi bila nia, na takribani watu milioni 5 walio ni wateswa wa unyonyaji wa kingono, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa  Wanawake na wasichana wanawasilisha zaidi ya 70% ya wateswa wa biashara haramu ya binadamu ambao hugunduliwa.

Ripoti ya Kimataifa ya Biashara Haramu ya Binadamu iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuambatana na Dawa za Kulevya na Uhalifu kwa mwaka 2019, inaonyesha kuwa 51% ya wateswa ni wanawake, 21% ni wanaume, 20% ni wasichana, na 8% ni wavulana na kati ya hao. Wateswa waliouzwa kwa ajili ya unyonyaji wa kingono ilifikia 54%, na 38% kwa kazi ya kulazimishwa.  Katika miaka michache iliyopita, biashara haramu ya binadamu pia imeongezeka miongoni mwa watu wanaoishi au wanaokimbia mazingira ya migogoro.

Ni vyema kutambua kwamba Misri imetia saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kupamba Uhalifu uliopangwa, na protokali ya Kuzuia, Kukandamiza na Kuadhibu Biashara Haramu wa Binadamu, Hasa Wanawake na Watoto. Mnamo  mwaka wa 2018, hapo awali Misri pia ilitangaza kujiunga na kampeni ya kimataifa ya " moyo bluu " yenye lengo la kuwalinda wateswa wa uhalifu wa biashara ya binadamu, yanayoendana na maadhimisho ya Siku ya Dunia ya Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, ambapo Kamati ya Kitaifa ya kiuratibuya  Kupambana na Kuzuia Uhamiaji Haramu. na Biashara Haramu ya Binadamu, na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa na Uhalifu, na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, walifanya sherehe kubwa katika Ngome ya Salah Al-Din, ambapo nembo ya moyo bluu ilionyeshwa kwenye kuta za zamani za Ngome hiyo baada ya jua kutua.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy