Maafisa Huru...Miaka 71 ya Mapinduzi ya Julai 23

Maafisa Huru...Miaka 71 ya Mapinduzi ya Julai 23

Imefasiriwa na / Aya Nabil

Kutoka kwenye ngome hadi Anga mpana, Wamisri waliandika historia kwa herufi za dhahabu, na walifanya mambo mengi sana.Ili kuondoa dhulma kuelekea kilele cha uhuru kwa utashi na dhamira isiyo na kikomo, watu wa kweli ambao hawatii mtu yeyote, kwa neno moja, na kila wakati kwa mkono mmoja katika shida.

Mapinduzi makubwa katika Historia ya ubinadamu na watu yamekuwa na jukumu muhimu katika kubadilisha mfumo uliopo unaotawala maisha ya kisiasa na kijamii, na uliyohitaji kuubadilishwa na mfumo mwingine unaotimiza matakwa na matarajio ya watu, kupitia Mapinduzi au Harakati ya watu inayotimiza lengo linalotakiwa, na Mapinduzi au Harakati hiyo inaungwa mkono kikamilifu na dhamira kali ya watu wake.

 Mwanzo wa mabadiliko katika maisha ya Wamisri ulikuwa tangu kuanza mapinduzi ya Julai 23, 1952, ambapo Maafisa Huru walikula yamini ya kuondoa utawala uliopo na kuanzisha utawala wa kidemokrasia.

 *Harakati ya Maafisa Huru:

 Ni kundi lililoandaliwa na Maafisa Huru ilifanyika mnamo Julai 23, 1952, na walijiita wenyewe, " Kundi la Maafisa Huru" na kabla ya hapo iliitwa "Harakati ya jeshi" na Umri wao haukuzidi miaka 35, isipokuwa baadhi yao, na lengo la shirika halikuwa kuunda mahusiano  au ushawishi wa umati, na hii iliwatofautisha na harakati zingine za kijeshi.

  Kabla ya Mapinduzi ya Julai 23, 1952, Misri ilifikia kiwango kikubwa cha mvutano wa kisiasa. Kutokana na kuenea kwa ufisadi, hali mbaya; pamoja na Utawala wa ukabaila na uvamizi wa Waingereza, na hali hizo ndizo zilizochochea kufanya mapinduzi ya Julai 23, 1952.

  Kufikia alfajiri ya Julai 23,1952, Jeshi, likiongozwa na Maafisa Huru, liliweza kudhibiti maeneo muhimu, na kuzingira maeneo ya kimkakati kama vile majumba ya kifalme, Wizara ya Vita, na jengo la redio, na mfalme na Serikali yake wakati huo walikuwa katika jiji la Alexandria.

Saa moja kasoro robo asubuhi "Anwar El-Sadat" alifika kwenye jengo la redio ; ili kutangaza taarifa ya kwanza iliyowekwa na Meja Jenerali "Muhammad Najib" na kusoma yafuatayo: "Misri ilipitia kipindi kigumu katika historia yake ya hivi karibuni ya rushwa, ufisadi na ukosefu wa utulivu wa utawala, na sababu hizi zote zilikuwa na athari kubwa kwa jeshi, na watu wafisadi na wenye nia mbaya walisababisha kushindwa kwetu katika vita ya Palestina, na baada ya vita hiyo, sababu za ufisadi ziliungana na wasaliti walipanga njama dhidi ya jeshi na utawala wa jeshi ulichukuliwa na mjinga au mfisadi ..... Mungu akupe mafanikio".

 Alfajiri ya Julai 23, Wamisri waliamka kwa mapinduzi ya Maafisa Huru dhidi ya utawala wa kifalme. Maafisa walifanya mapinduzi ya kijeshi bila umwagaji damu, na wakafanikiwa kudhibiti hali hiyo; Mfalme alilazimika kuacha kiti cha enzi, na akahamishwa kwenda Italia mnamo Julai 26, na hiyo ilisababisha kuondolewa kwa ufalme, na mfumo wa Utawala ulibadilishwa ukawa Jamhuri.

 Watu wa Misri walionesha uungaji mkono wao kwa jeshi na tabaka zote za watu na madhehebu zake zilitoka kuunga mkono malengo ya mapinduzi, na kwa hivyo mapinduzi yalichukua uhalali wake kutoka kwa watu baada ya kuyaunga mkono. Watu wa Misri waliendelea na njia ya mapinduzi, bila kujali ugumu, na mapinduzi yalitangaza kanuni zake za kukomesha ukoloni, kupinga utawala wa kibebari, kuondoa ukabaila, kuanzisha haki ya kijamii, na kupinga njama zinazolenga jeshi.

Hali ya Misri ikabadilishwa sana baada ya mapinduzi, ambapo mapinduzi yaliunga mkono tabaka lililoteseka kutokana na dhuluma, na kunyimwa haki ya kijamii; kundi la Maafisa Huru halikuwa na mwelekeo mmoja wa kisiasa, lakini lilijumuisha mwelekeo tofauti; ambayo ilisababisha mabadiliko makubwa katika hali ya Misri, na mapinduzi katika akili za Wamisri yalihusishwa na picha ya Marehemu "Gamal Abdel Nasser" aliyekuwa ishara wazi ya harakati za ukombozi dhidi ya uvamizi, na picha hiyo imeendelea hadi leo.

 Misri ilifanikiwa kupata uhuru wa kisiasa kwa kuondoa utawala wa kifalme na kutangaza Jamhuri. Ardhi ya Misri ilipata uhuru wake kutoka kwa mkoloni aliyewaibia watu haki zao, na mapinduzi yalielekezwa kuhakikisha uhuru wa kiuchumi kwa kuondoa ukabaila, Hivyo yaliweza kuhakikishs kanuni ya haki ya kijamii, na kuboresha hali yake ya kiutamaduni na kielimu.

 Misri baada ya mapinduzi ya Julai 23 ilipanua jukumu lake Barani Afrika na eneo la Kiarabu, na harakati za ukombozi zilizoanza baadaye zilipata msaada wa kifedha na kimaadili kutoka Misri, ambapo Cairo ilifanikiwa kusaidia harakati za ukombozi huko Yemen na Algeria, na kuwasilisha kesi yao katika Umoja wa Mataifa na vikao vya kimataifa. Redio ya Sauti ya Kiarabu iliwakilisha msaada wa vyombo vya habari; kwa ajili ya mapinduzi ya Algeria, na redio siri ya Algeria ilianzishwa;ili kutangaza taarifa, vyombo vya habari vya Misri pia viliunga mkono mapinduzi ya Algeria.

 Mapinduzi hayo yalithibitishia kwa taifa la kiarabu kutoka Bahari hadi Ghuba kwamba nguvu za Waarabu ziko katika umoja wao, wameunganishwa na historia moja, lugha moja, na hatima moja, na hivyo mapinduzi hayo yalitoa mifano ya ajabu sana ya Upendeleo wa jeshi la Misri kwa matumaini na matarajio ya watu maishani. Msaada uliotolewa na mapinduzi pamoja na uongozi wa Gamal Abdel Nasser kwa Harakati za ukombozi, iwe katika ulimwengu wa Kiarabu au Kiafrika, na jukumu lake zuri katika kuibuka kwa Jumuiya ya Umoja wa kiafrika;iliipa Misri nafasi ya kimataifa, ya Asia na ya kiafrika.