Viongozi wa Israeli Watafuta Faida Zao Wenyewe Bila ya Kujali Madhara kwa Wengine, Ilihali Hatusahau Majukumu Yetu ya Kitaifa na Kimataifa

Viongozi wa Israeli Watafuta Faida Zao Wenyewe Bila ya Kujali Madhara kwa Wengine, Ilihali Hatusahau Majukumu Yetu ya Kitaifa na Kimataifa

Imetafsiriwa na/ Ahmed Salama
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

Swali la msemaji: Je, Mheshimiwa una maoni gani juu ya wasiwasi wa Israel kwamba mkataba kati ya Misri na Uingereza kuhusu kuondolewa kutoka eneo la Mfereji wa Suez na msaada uliopendekezwa na Marekani humithilisha tishio kwa Israeli?              

Rais Nasser: Nadhani kuwa wasiwasi wa Israeli ni bandia tu, na lengo lake mara nyingi  linakuwa kupata pesa zaidi kutoka kwa serikali ya Marekani, watu wa Marekani, na kutoka duniani kote. Mkataba wa Misri- Uingereza  utaondoa mojawapo ya vizuizi vikuu vinavyozuia mahusiano kati ya nchi za Magharibi na nchi za Kiarabu. Israeli yenye ubinafsi sana hata inafikiri kwamba mawazo ya watu wote yanaelekea kwake, na kwamba tuna mambo ambayo ni makubwa zaidi, na makubaliano ya Misri- Uingereza ni tu maonesho ya maendeleo ya ujenzi nchini Misri.

 Kwa bahati mbaya, Israeli, inaonekana kuwa inashiriki msimamo wa Wakomunisti - kwa makusudi au bila makusudi - wakati inajitahidi kuzuia suluhu ya Amani ya shida ya miaka 72 ya Mfereji wa Suez. Wakomunisti na Wanazi wameazimia kuzuia suluhu ya Amani; hii ni kwa sababu ya kuzukia machafuko katika ulimwengu wa Kiarabu hutumikia tu vitu vya uharibifu, na hamu hii ya kuunda machafuko na machafuko katika ulimwengu wa Kiarabu ili kuunga mkono kile nilichotaja wakati wa nyuma kwamba Wanazi hutumikia Wakomunisti katika majaribio yao ya kusababisha machafuko, na kuzuia njia ya kuboresha mahusiano kati ya Magharibi na nchi za Kiarabu.

Swali la msemaji: Je, unaona juhudi za Mhe. Rais wa Sasa  Saleh Salem katika kuunga mkono nguvu za kijeshi za ulimwengu wa Kiarabu kuwa na athari kwa Israeli?

Rais Nasser: Juhudu za Rais Salah Salem katika ulimwengu wa Kiarabu hazikukamilika tu katika kuimarisha nguvu za kijeshi za Kiarabu; tunatafuta kuimarisha mahusiano yetu yote na nchi za Kiarabu, isitoshe kuratibu miradi yetu ya ulinzi, kwa hivyo umakini wetu unakwenda kwa ulinzi na sio kwa ari, na moja ya malengo yetu makubwa ni kutangaza Amani, na kutoa ustawi katika mkoa huu, na tunajali kuzuia uhasama wowote.

Na hatimaye ushahidi umefika kwa umma wa ulimwengu kuwa Israeli - sio Waarabu - wanafuata sera iliyowekwa na shambulio la kigaidi dhidi ya vijiji vya Waarabu.

Swali la msemaji: Taarifa ya hivi karibuni kutoka kwenu imetajwa kuwa Israeli inagawanya ulimwengu wa Kiarabu katika sehemu mbili, unaweza kufafanua ikiwa una suluhisho la hali hii? Suluhisho ni nini

Rais Nasser: Israeli imekatisha usafiri wa nchi kavu zote kati ya Misri na nchi za Kiarabu mashariki mwa Suez, na tunaamini kwamba Misri na nchi za Kiarabu zinapaswa kupata usafiri wa nchi kazi zinazokuwa   muhimu kwa biashara zao, ustawi wao na miradi yao ya ulinzi. Lakini kila mtu alifahamu kwamba ulinzi wa eneo hili ni wa watu wake kwanza; umuhimu wa kuunda njia hii ya ardhi kati ya Misri na nchi za Kiarabu kwa faida ya ulinzi wa Mashariki ya Kati ilionekana.

Ni wazi kuwa Waarabu wataendelea kuunga mkono miradi yao ya ulinzi bila kujali Israeli. Israeli imechukua eneo la kusini mwa Palestina, hadi Ghuba ya Aqaba, ingawa Umoja wa Mataifa na nchi za Kiarabu hazitambui haki ya Israeli katika eneo hilo. Na kwamba uvamizi huo ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano, na  unaendelea kupinga mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Sioni suluhisho la haraka kwa hali hii isipokuwa ikiwa maoni ya umma wa ulimwengu au shinikizo la kimataifa litalazimisha Israeli kuachana na eneo hili, ambalo halikuchukua kwa msingi wa mradi wa mgawanyiko, au kwa mujibu wa masharti yoyote ya makubaliano ya kusitisha mapigano; lakini ilivunjika kwa kukiuka makubaliano haya.

Swali la msemaji: Unaona inawezekana kuwa na mkataba wa amani kati ya Misri na Israeli wakati wowote? Ikiwa ndivyo, ni nini masharti ya Amani hiyo?

Rais Nasser: Viongozi wa Misri na wa Kiarabu wamesema mara kwa mara kwamba haitawezekana kufanya Amani na Israeli, isipokuwa Israeli itatii maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini Israeli haijaacha kupinga Umoja wa Mataifa, na inaendelea na mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya vijiji vya mbele ambavyo vimeibua hasira ya maoni ya umma wa ulimwengu, na kusukuma serikali ya Marekani kuelekeza lawama kwa Israeli. Hatua hii ya mwisho ina maana kubwa ikitukumbusha uwezo wa ushawishi wa Zionism katika Bunge na udhibiti wa vyombo vya habari vya Marekani.

Kwa kuongezea, Israel haijafanya chochote kuutuliza Waarabu, lakini kwa makusudi - wakati tulijaribu kusuluhisha tofauti zetu na nchi za kimagharibi - iliweka vizuizi, bila kuzingatia hamu ya viongozi wa Magharibi na nchi za Kiarabu kufikia kiwango cha juu cha utulivu, na ustawi unaofuata kwa Amani ya ulimwengu.

Viongozi wa Israeli wanatafuta faida zao tu bila kujali madhara kwa wengine, ikiwemo usalama wa mataifa ya magharibi ambayo wanadai kuwa ni marafiki wao. Waisraeli wamedai kuwa wao pekee ndio marafiki wa demokrasia katika Mashariki ya Kati, wakati matendo yao yanapinga madai hayo. Na ukweli ni kwamba Israel si rafiki ya mtu yeyote; ni rafiki yake mwenyewe, na inazunguka kati ya Mashariki na Magharibi kulingana na kile inachokiona kuwa ni faida kwa pande zote mbili. Israeli inatafuta faida yake tu, wakati sisi hatujawahi kupuuza majukumu yetu ya kitaifa na kimataifa. Na nadhani mafanikio ya mazungumzo yetu na Uingereza juu ya suala la Mfereji wa Suez ni ushahidi bora wa hili.

Mazungumzo ya Rais Nasser na Naibu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati wa Shirika la Habari la Umoja wa Mataifa .

Tarehe 13 Septemuhba 1954.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy