Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye Lebanon, Kutoka Ikulu ya Jamhuri Huko Mjini Kairo, mnamo Mwaka 1959

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye Lebanon,  Kutoka Ikulu ya Jamhuri Huko Mjini Kairo, mnamo Mwaka 1959

Imetafsiriwa na/ Amira Roshdy 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

Kwa kweli, kipindi nilichokaa na nyinyi kinachukuliwa kuwa mojawapo ya vipindi vya furaha zaidi ninavyoweza kuhisi; kwa sababu daima kilionesha hisia nzuri, kilionesha udugu na upendo ambao ni desturi ya Umoja wa Kitaifa wa Kiarabu, bila desturi.. udugu baina ya watu wa kiarabu nchini zote za kiarabu, na upendo baina ya waarabu wa nchi  zote za kiarabu. Tunashauri kwa uamini mkubwa wakati ujao, kwa msaada wa Mungu; kwa sababu tunatembea katika njia yetu kwa ajili ya fahari ya nchi yetu na fahari ya uarabu wote, tunaitegemea roho hii inayotoka kutoka kila nchi ya kiarabu na kila kijiji cha kiarabu; bila kukabiliana na watoto wake isipokuwa mkutano wa hisia, isipokuwa mkutano katika upendo wa taifa letu la kiarabu, katika uhuru wa nchi zetu za kiarabu, na katika kufanya kwa ajili ya fahari ya nchi ya kiarabu.

Maadui ya taifa ya kiarabu walijaribu wakati wote na kwa njia yoyote  kugawanya kati ya watoto wake kwa kila njia iwezekanavyo, na kugawanya kati ya wana wa nchi hizo za kiarabu, na kuzukia kampeni za chuki baina ya watu wa kiarabu nchini zote za kiarabu. Ndugu Lebanon imekabiliwa na kampeni hizi kwa muda mrefu, kampeni za chuki bado zinaeneza Lebanon na ulimwengu wa kiarabu. Wakati wa nyuma, kampeni hizi zimefanywa na duara za kiukoloni wa magharibi, leo zimefanywa na duara za kiukoloni na wasadizi wa ukoloni, na mawakala wa komunisti; Kwa kufanya hivyo, wanajaribu kuusambaratisha Umoja  wa Kiarabu ili wapate udhibiti juu yetu na kututiisha.

Lakini roho hii na ufahamu huo.. ufahamu mkubwa niliogusia katika kila tukio, ambao wakati wote unaniongezea Imani kwamba Taifa la Kiarabu lilidhamiria kujizatiti na ufahamu ili kusimama dhidi ya maadui zake baada ya kuteseka kwa kipindi kirefu Wakati wa nyuma; ufahamu huu ni silaha yetu dhidi ya wanaotaka kututawala, dhidi ya wanaoeneza chuki na fitina baina ya wetu, na dhidi ya wale wanaotutamani, wawe ni wakoloni au mawakala wa kikomunisti. Ndio maana tunaelekea siku za usoni kwa Dhamira na Imani, kwa udugu, upendo na mshikamano. Tunaelekea siku za usoni tukiwa tumeunganishwa na umoja.. umoja wa mioyo, umoja ulioudhihirisha leo kwa hisia hizi nzuri zinazodhihirisha upendo safi, mapenzi ambayo hayatafuti thamani, wala hayatafuti chochote isipokuwa Imani yake juu ya haki yake ya uhuru na haki zake.Katika maisha, bega kwa bega na ndugu zake wa Kiarabu katika kila nchi ya Kiarabu.

Roho hii na hisia hizi nilizoziona leo; Bali ni silaha yetu ya msingi katika vita vyetu vikubwa vya uhuru na mshikamano wa taifa la Kiarabu, umoja wa Waarabu dhidi ya maadui wa Waarabu, kwa mshikamano wa Waarabu dhidi ya maadui wa Waarabu, kwa uumbaji. ya nchi ya Waarabu wapendwa na wakarimu katika kila nchi ya Kiarabu, na kwa ajili ya umoja wa Waarabu unaotuleta pamoja sasa katika Mahali hapa hakuna umoja wa kikatiba au umoja wa kisheria, kwa sababu ni umoja wa hisia.. na umoja ambao tunadhihirisha kwa njia ya kubadilishana hisia, kubadilishana mapenzi, kubadilishana udugu, na kubadilishana matumaini kwa ajili ya mema kwa kila mmoja wetu katika nchi yoyote ya Kiarabu. 

Hakika huu ndio umoja wa kweli unaotuunganisha; Kila kitu kinachotokea kwa Lebanon kinatokea kwetu, kila kitu kinachotokea kwetu kinaathiri Lebanon, na kila kitu kinachotokea kwa nchi yoyote ya Kiarabu huathiri sisi sote. Huu ndio umoja wetu, na huu ndio usemi wetu wa umoja wa Waarabu. Umoja wa kushikana mikono dhidi ya maadui zetu si umoja unaoegemezwa kwenye uchoyo, wala umoja unaojikita katika kufanya kazi kwa ajili ya wageni, mawakala wa ukoloni, au kwa ajili ya wageni wa kuwa chini yao, bali ni umoja safi usio na malengo na bila kuungwa mkono na katiba. Ndilo linalotuleta pamoja sasa mahali hapa, sisi ni wana wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu na wana wa Lebanon, na sote tunahisi upendo ukiruka juu ya vichwa vyetu, udugu unatuunganisha, na hisia nzuri na matakwa mema yanayotokana na hisia zetu. na kutoka katika nafsi zetu.

Katika roho hii tunatumai kwa siku zijazo, na katika roho hii tunahisi kwamba kuna nguvu kubwa nchini Lebanon dhidi ya kampeni za chuki ambazo zinalenga Lebanon na Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, na dhidi ya kampeni za chuki ambazo zinalenga kutuvuta sote. kutii udhibiti wa wakoloni, na dhidi ya kampeni za chuki zinazofanywa na wakomunisti ili kutufungamanisha na gurudumu la utegemezi.

Kwa imani hii, roho hii nzuri, upendo huu, na udugu huu;  Sikuzote tutakuwa washindi, Mungu akipenda, katika siku zijazo, kama vile tulivyokuwa washindi zamani.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy