Siku ya Usalama wa Wagonjwa Duniani

Imetafsiriwa na/ Amr Ashraf
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Kulingana na Shirika la Afya Duniani, angalau wagonjwa 4 kati ya 10 wanajeruhiwa wakati wa kupata huduma za afya, na angalau 80% ya madhara haya yanaweza kuzuiwa. Makosa mengi yanayodhuru yanatokana na utambuzi mbaya wa wagonjwa, maagizo yasiyo sahihi na matumizi yasiyo sahihi ya dawa.
Shirika la Afya Duniani huadhimisha Siku ya Usalama wa Wagonjwa Duniani kila tarehe 17 Septemba ya kila mwaka kwa lengo la kuongeza uelewa wa kimataifa kuhusu usalama wa mgonjwa, kuimarisha ushiriki katika kutoa huduma za afya salama, na kuendeleza hatua za haraka na endelevu za kimataifa ambazo zitaboresha usalama wa mgonjwa na kupunguza madhara kwa yao.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy