Kila Mwaka, Septemba 10, China Huadhimisha Siku ya Mwalimu

Kila Mwaka, Septemba 10, China Huadhimisha Siku ya Mwalimu

Imetafsiriwa na/ Enas Abdelbassit 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

Leo, Septemba 10,  China inaadhimisha Siku ya Mwalimu, ambapo watu wanaonesha hisia zao za shukrani, upendo, urafiki na heshima  kwa walimu wao.  Ualimu huko nchini China unaheshimiwa sana, na unaonwa kuwa kazi ya heshima zaidi kuliko kazi nyingine. Siku ya Mwalimu ilianzishwa rasmi nchini China mnamo mwaka 1985, kwa lengo la kuinua kazi ya kiakili iliyopotea wakati wa miaka ya Mapinduzi ya Utamaduni.

 China ndiyo yenye mfumo mkongwe na mkubwa zaidi wa elimu duniani, ulioanzia takribani miaka 2,000. Idadi ya walimu nchini China ni takribani milioni 16, huku wanawake wakiwa ni asilimia 65 kati yao, mfumo wa elimu ya kisasa nchini China unategemea na toleo la Ulaya la elimu ya lazima, ambayo huchukua miaka sita hadi tisa, ikigawanywa katika miaka 6 kwa shule ya msingi, na miaka mitatu kwa elimu ya sekondari. 

Uwekezaji katika elimu huko unawakilisha takribani 4% ya pato la taifa la China, kulingana na kile kilichochapishwa na gazeti la China People’s Daily.

Jana, Xi Jinping, Rais wa China, aliwapongeza walimu wote wa nchi hiyo, pamoja na wawakilishi wa vitengo vya mfano vya kufundisha vilivyopewa jina la marehemu Huang Da nian, mtaalamu wa jiofizikia  aliyefanya kazi kama profesa katika Chuo Kikuu cha Jilin na kupitia utafiti wake, China ilifanya maendeleo makubwa katika uchunguzi wa kina kirefu cha dunia, na kwa heshima ya jina lake, shule kubwa zaidi duniani imepewa jina lake, na katika kumbukumbu yake, shule kubwa zaidi zilipewa jina lake, na akitoa pongezi kwa juhudi zao kubwa na kuwahimiza kuendelea kutoa ujumbe na mwongozo mzuri kwa wanafunzi wao, na kuimarisha ustadi wao wa kufikiri na ubunifu, akisisitiza umuhimu wa ujumbe wao katika kujenga kizazi bora, kinachoweza kujenga nchi yao.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy