Lugha ya Kiswahili.... Chimbuko na Usambazaji
Imetafsiriwa na/ Rahma Ragab
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Imeandikwa na/ Fatma Mahmoud
Umoja wa kimataifa umeamua kuainisha Siku ya Julai 7 kila mwaka kuwa Maadhimisho ya lugha ya Kiswahili Duniani, ambapo Lugha ya kiswahili inazingatiwa ni lugha ya kibantu inaeneza pwani za Afrika Mashariki na lugha ya kimawasiliano ya pamoja kati ya Nchi za Afrika Mashariki na miongoni mwa lugha inayotumiwa na Umoja wa Afrika, nchi zinazozungumzia kiswahili ni( Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), Somalia, visiwa vya Mwezi, Zambia, Madagascar, Msumbiji, Malawi na Oman). Inazingatiwa ni lugha iliyo rasmi huko nchini Tanzania na visiwa vya Mwezi na lugha ya pili huko nchini Kenya baada ya lugha ya kiingereza.
Idadi kamili ya wazungumzaji wa lugha ya kiswahili inatofautiana kati ya wakazi milioni 50 kufikia zaidi ya wakazi milioni 200. Misamiati mengi ya lugha ya kiswahili yametokana na lugha ya kiarabu na ya Sanskrit kutokana na kutendeana baina ya wafanyabishara na waarabu na wahindu kwenye pwani za Mashariki Kusini mwa Afrika. Ina pia maneno kutoka kireno, na ilikuwa iliandikwa kwa herufi ya kiarabu na sasa inaandikwa kwa herufi ya kilatino.
Umuhimu wa usambazaji zaidi lugha ya kiswahili kati ya wananchi wa Afrika unatokana na kwamba ni mojawapo ya kuimarisha utambulisho wa Kiafrika, na tayari juhudi za kuimarika kutumia lugha hiyo kama lugha ya Afrika yote zilianza kutokea tangu miaka 60 ya karne iliyopita, kupitia Julias Nyerere , Rais wa Kwanza wa Tanzania baada ya kupata Uhuru, aliyetumia lugha ya kiswahili ili kuunganisha Raia wake baada ya uhuru kutoka ukoloni wa waingereza.
Mnamo mwaka 2019, pia lugha ya kiswahili imekuwa lugha moja ya Afrika iliyopitishwa na kikundi cha maendeleo cha Afrika Kusini. Hivi majuzi, chuo kikuu cha Adis Ababa kilitangaza kuwa kitaanza kufundisha lugha ya kiswahili, Pamoja na jukumu la Misri la kuimarisha lugha za Afrika miongoni mwake ni lugha ya kiswahili, ambapo tangu mwaka 1967 kitengo cha lugha za Afrika kilianzishwa kwenye kitivo cha lugha na tafsiri kwenye chuo kikuu cha Al-azhr, baadaye vyuo vikuu vingi vya kimisri vilianza kuifundisha kama chuo kikuu cha Al-azhr, Kairo na Ain Shams na pia cha Aswani na hiyo kwa sababu ya umuhimu wa lugha ya kiswahili ili kuimarisha utambulisho wa kiafrika na mahusiano ya pamoja kati ya nchi za bara la Afrika.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy