Sera ya Serikali ya Kimisri ni Ushirikiano na Nchi zote

Sera ya Serikali ya Kimisri ni Ushirikiano na Nchi zote

Imetafsiriwa na/ Rahma Ragab 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

Swali la mhoji: mnaweza kuainisha nafasi ya Msiri kuelekea nchi za bahari ya Mediterania? Vipi muungano wa kiarabu na mradi wa kuanzisha mkutano wa kiislamu unaweza kuingia kwa nchi za eneo hilo?

Rais Nasser: sera  ya Serikali ya Kimisri ni Ushirikiano na nchi zote zinazotaka kushiriki naye ili kutimiza maslahi ya pamoja, na kwa kuzingatia nafasi pekee ya Misri kwenye bahari ya Mediterania; ambayo inakuza mahusiano na nchi zote za bahari hiyo, na kuhakikisha usalama, utulivu na ushirikiano wa pamoja.

Kuhusu mahusiano ya nchi za bahari nyeupe na chuo cha nchi za kiarabu, au nchi za kikundi cha kiarabu cha kiislamu, kwa upande wa kanuni hayapiti yaliyotajwa wakati wa nyuma, na kinachojulikana kwamba nchi hizo zitaelekea wakati wote ili kujenga mahusiano ya marafiki pamoja na nchi zote zinazo amza ya kukuza amani, kuhakikisha Usalama na Maendeleo ulimwenguni.

Swali la mhoji: mheshimiwa je, unadhani kwamba Italia inaweza kuchangia mchango makini kwenye maendeleo ya kiuchumi yaliyopatikana wakati huo huko  nchini Misri? Na pande gani zinazoweza kushirikiwa na Italia? Kulingana na tukio hilo unaweza kuzungumza juu ya ziara ya Waziri wa Biashara ya Kimisri, Mhe. Mohamed Abu Noseir nchini Italia na ziara ya ujumbe wa kitaliano huko nchini Misri Oktoba ijayo?

Rais Nasser: Serikali ya Kimisri inakaribisha wakati wote msaada wowote, sawa ya ni wa kiufundi au wa kushiriki kwa upande wa kifedha unaisaidia kutekeleza mpango wake wa kiuchumi unaolenga kuongeza kiwango cha maisha nchini pasipo na vikwazo vinaathiri utawala wake, kwa hivyo serikali ya Kimisri imechukua hatua zinaweza kuhimiza mtaji wa kigeni kuingia nchi, juu yake kutoa sheria ya uwekezaji wa mitaji ya kigeni, na taasisi mpya zote za utengenezaji hazilipi kodi kwa miaka saba, mashine, vifaa na zana zinazohitajika ili kuanzisha viwanda vipya hazitoi kodi ya forodha. Hayo yote pamoja na sheria mpya inayopanga kazi ya kampuni zinazochangia ili kulinda mtaji na wadau, na sheria zingine zilizohimiza sana kuvuta mtaji wa kigeni kwa Nchi, waitaliano  wenye mitaji wameshachangania kwa kiasi kikubwa.

Kuhusu ujumbe wa Dkt. Mohamed Abu Noseir nchini Italia , ni mfululizo kutoka jumbe zetu za kiuchumi kwa nchi mbalimbali; ili kujadili mambo yote yanayotuwezesha kukuza na kuendelea mahusiano yetu ya kiuchumi, ya kifedha na ya kibiashara na ulimwenguni kote. 

Swali la mhoji: serikali yenu inatarajia jukumu nini linaloweza kufanywa na wahamiaji wa kigeni hapa nchini Misri kwenye mchakato wa kufufua Uchumi wa kimisri? Na ni dhamana gani tunaozitarajiwa kulingana na nafasi yao nchini Misri kwa upande wa umma, na upande wa ushiriki wao kwenye nyanja za maisha nchini?
Rais Nasser: wahamiaji wa kigeni nchini Misri walikuwa na jukumu kubwa kwenye nyanja tofauti, serikali iliyopo ilikuwa inashughulikia zaidi kwa kukuza uchumi wa taifa, kuongeza Pato la mtu , kuongeza kiwango cha maisha, na kutekeleza adili na usawa kwa wote, jambo ambalo linawezesha kufikia Ustawi na Utulivu, wahamiaji wa kigeni – bila shaka- zitakuta nafasi nyingi zaidi ili kuongeza shughuli n ushiriki wake kwenye shughuli tofautitofauti huko nchini. Na naona wahamiaji wote wa kigeni wanaona kwamba Nchi hiyo ni nchi ya pili kwao, na hiyo kwa sababu  serikali na nchi wanawaheshima, na kuwatunza.

Swali la mhoji: je, Mhe. Unaweza kutuambia nafasi ya msingi wa mfereji wa Suez kulinganisha na mipango ya kimataifa, na baada ya kuondoka kwa vikosi vya Uingereza kutoka kwake, na wakati vikosi vya Kimisri viliuendesha?

Rais Nasser: Msingi wa Suez utarejesha nafasi yake kama msingi wa kijeshi baada ya kurejeshwa kwake kwa Misri, na vikosi vya Kimisri vitaukalia wakati wa kuondoka kwa vikosi vya Uingereza, hadi vitaunyang’anya kufuatia kuondoka kwa vikosi vya Uingereza mwishoni mwa muda wa mkataba.

Swali la mhoji: makubaliano ya kuondoka yaliyosainiwa mnamo julai 27,1954 yalijumuisha masisitizo kwamba serikali ya Kimisri ina nia ya kuheshimu mkataba wa 1888, unayohusu uhuru wa urambazaji kwenye mfereji wa Suez kama mpito wa kimataifa, je, serikali yenu inawaza kukariri masisitizo hayo yaliyoainishwa na mkataba wa pande mbili kati ya Misri na Uingereza kwa serikali nyingine ulimwenguni?
Na ikiwa umeamua hiyo, masisitizo hayo yatakuwa na aina gani? Yatakuwa tangazo la umma kwa wote au kupitia mawasiliano ya binafsi kwa nchi husika?

Rais Nasser:  kuashiria kwamba nchi mbili zilizosaini mkataba wa julai 27, 1954 zinaheshimu uhuru wa urambazaji kwenye mfereji wa Suez kama ilivyotajwa kwenye mkataba wa 1888, ni msisitizo wa sehemu iliotajwa kwenye mkataba huo, na unatekelezwa kwa nchi zote zilizousaini pasipo na upendeleo au ubaguzi wowote, kulingana na hiyo,hakuna haja ya kuwasiliana na Nchi zilizobaki zilizosaini mkataba huo; ili kusisitiza jambo lililopitishwa na kuheshimiwa na pande zote zilizosainiwa.

Swali la mhoji: ulimwengu unaona ustawi uliofikiwa na Misri mnamo Enzi ya Mapinduzi, na mnamo muda zaidi kidogo ya miaka mbili, je, Mhe. Unaweza kuongea kuhusu nyanja zilizokuwa na ustawi zaidi hadi sasa?

Rais Nasser: mojawapo ya malengo muhimu zaidi ya Mapinduzi ya julai 23,1952 ilikuwa ni kuondoa nguvu ya kikoloni, kueneza uadilifu na usawa baina ya watu wote, kuongeza kiwango cha maisha, kulinda hayo yote kutoka maslahi ya kimwinyi na unyonyaji haramu.

Kwa ajili ya hiyo, mapinduzi yalielekea hatua zake za kwanza ili kuongeza kiwango cha maisha ya mtu, kuporesha kituo chake cha kijamii kupitia kukuza nguvu ya kuzalisha itakayoongeza Pato la taifa, hayo yote yatakuwa kupitia mpango utagawanywa kwa sehemu tatu:

1- Kuendelea nguvu ya uzalishaji wa kilimo, inayotengwa kwa sehemu mbili kwa nguvu ya uzalishaji wa kilimo inayovunwa kwa kasi, na ile inayovunwa baadaye ya muda maalumu, kuhusu ya kwanza inalenga Eneo la ardhi iliyolimwa kwenye kijimbo cha delta na Misri ya juu, kubadilisha umwagiliaji wa msimu kwa umwagiliaji wa kudumu, kulima(kuporesha)ardhi mpya kwenye oasis kwa kutumia maji yaliyotolewa na pampu, kuporesha mfumo w kusafisha kwa kilimo na umwagiliaji wa pampu, pamoja na mpango wa kuporesha maeneo laki 3 ya ardhi, ya pili inalenga kujenga tanki la juu kwenye upande wa Kusini wa tanki la Aswani.

 Pamoja na hatua kubwa hizo zote zilipangwa na serikali ya Mapinduzi za kuongeza uzalishaji wa kilimo kupitia kueneza mibegu iliochaguliwa, kuongeza Eneo la ardhi iliyolimwa kwa mahindi, kuzalisha mchele kutumia maji ya visima, kuhifadhi mazao dhidi ya wadudu waharibifu wa kilimo, na mwishoni kuongeza uzalishaji wa matunda, tunapaswa kuongeza kwamba serikali ya Mapinduzi inaelekea juhudi yake kwa kufuga wanyama pamoja na kupambana na magonjwa ya wanyama, kuporesha malisho kwenye kijimbo cha jangwa, na kuendelea uvuvi.

Ukuaji wa utengenezaji: miradi ya utengenezaji wa chuma na shaba ilisomwa, na uamuzi wa kujenga kiwanda cha utengenezaji kinaweza kuzalisha laki 2 tani ya shaba na chuma kila mwaka umechukuliwa, na uzalishaji wa kwanza utaanza mnamo 1957, jambo ambalo litawezesha kuingiza viwanda vingi vya chuma na mitambo kama mabomba ya maji, vifaa vya kielektroniki, vipu vya chuma, na magari ya njia ya reli, na vipuri vya injini.

Uchanganuzi wa mradi wa kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea ambako gharama yake itaelekea kwa kiwango cha paundi millioni 25 umemaliza , na kuunda viwanda vingi vya kemikali vilivyohimiza viwanda vya bidhaa za kutibu na betri na tairi ya gari, na kilikuza viwanda vya nguo na ngozi kwa watumiaji wa ndani na pia viwanda vya hariri ya bandia na pamba.

Na jambo muhimu zaidi lililofanyika na Mapinduzi kwenye uwanja wa utengenezaji ni kuendelea utajiri wa chuma hasa petroli, maabara ya usafishaji wa petroli yamepanuka, uzalishaji wake umeongezeka kutoka tani laki 3 hadi tani millioni moja laki nne kila mwaka, serikali imefikia maendeleo mengine kama hayo kwenye uwanja wa kuunda na kutumia umeme.

Serikali hadi mwisho imeendelea ili kufanya mradi wa tanki la Aswani kuzalisha umeme ambao vitengo vyake vipya vya kwanza vitaendesha mwaka 1957, na imejenga kituo cha kiumeme kaskazini mwa Kairo kinachoweza kuzalisha kilo Watt laki 6 kwa saa, na kazi inaendelea ili kujenga kituo kingine cha umeme kusini mwa Kairo kinazalisha kilo watt laki moja na elfu ishirini kwa saa, na kitavipa(toa) viwanda vyote vya Eneo la kati kwa mkondo wa umeme , hiyo pamoja na sera ya umeme itamaliza kutekeleza mradi wa kutoa umeme kwa Tanki la Aswani.

2- Miradi ya ujenzi juu yake ni mradi wa kujenga barabara, sasa serikali ina azama ya kujenga makundi ya barabara yenye gharama ya paundi milioni 30, na yatamalizika mnamo miaka 10 ijayo, na pia kuna miradi mengine itakayotekelezwa inahusishwa na urambazaji wa ndani.

Kuhusu urambazaji wa bahari, Serikali ya Mapinduzi imeamua kuunda meli za kibiashara za Kimisri, pia kupanuza bandari ya Kimisri, ilitaja pia masuala ya kurefusha mtandao wa simu, na sasa inaangalia pia miradi ya kujenga makazi kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, na kurefusha urefu wa njia za reli kwa kilometa elfu moja, kufanya upyaji wa treni, na kukuza uhamasishaji wa reli kwa magari mapya.

Sasa hivi, vitengo vyenye teknolojia vinajengwa kwenye vijiji vinapatikana hospitalini, kilinikini, shule ya msingi na shule ya kilimo , vitafaidisha wanakijiji elfu 15, vinalenga kuongeza kiwango chao cha maisha, kuwatoa mafunzo ya utumiaji wa mbinu za utengenezaji kuanzia kipindi chake cha Kwanza (kutoka kwanza) na kuongeza mifugo yao, kuboresha hali ya kiafya ya watoto na mama, na bajeti maalumu ya kiwango cha milioni 14 na laki 5 imeainishwa kwa miradi hiyo pamoja na bajeti ya wizara ya mambo ya kijamii.

Kuhusu wakulima kwa ujumla, tunaelekea kutekeleza mpango wa makundi ya kiushirikiano yatakayowaongoza ili kutumia zana mpya za kilimo, kuwatoa mikopo, na kuwaongeza kwa mibegu safi na mbolea, jambo ambalo litaongeza uzalishaji wao kwa asilimia 16.

Ongezeko hili la uzalishaji limekuza kituo chetu cha kifedha, limesisitiza imani yetu, na pia ongezeko la kubadilishana na uagizaji limefuata na ongezeko la salio la malipo, ambalo limepata nchi hifadhi badala ya salio la deni.

Swali la mhoji: je, serikali yenu inafikiri kufanya mawasiliano ili kujenga mahusiano ya kina zaidi pamoja na nchi za Amerika ya kilatino (kusini)? Na njia gani ya kukuza mahusiano na nchi hizo kwa upande wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni?

Rais Nasser: uhusiano wetu na Marekani ya Kusini ulikuwa na unakuwa na tabia ya heshima na ushirikiano, na kuna mahusiano mengi yanayotufungamana na Nchi hizo, licha ya kuna wahamiaji wengi wa kiarabu huko wanatufungamana zaidi, na natamani uhusiano wa Misri na Uimwengu wa Kiarabu utakuwa n kina zaidi pamoja na Marekani ya Kusini, hasa kwenye nyanja za uchumi, biashara, utamaduni na mahusiano ya kimataifa ambazo zitanufaisha kwa heri.


Vyanzo:

Mazungumzo ya Rais Gamal Abdu El-Nasser pamoja na vyombo vya habari vya kitaliano 

Mnamo Desemba 17, 1954

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy