Tendo Yoyote Yenye Jeuri Dhidi ya Misri Litaathari Ulimwengu kutoka Bahari ya Atlantiki mpaka Bahari ya Hindi
Imetafsiriwa na/ Amira Roshdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Swali la mhojiwa: maoni yenu nini kuhusu maandalizi ya vita vya kiingereza- kifaransa katika Bahari ya Mediterania? Mnaamini kuwa huo ni udanganyifu au ikiwa mazungumzo yatakatishwa kabisa, itatia Mashambulio?
Rais AbdelNasser: Kama navyokuwa Rais anayewajibikia watu walitayarisha kukabiliana na uwezekano mbaya zaidi, sijali hata kidogo hatua zinachukuliwa na wengine.
Swali la mhojiwa: Katika hali ya kukamata, mnadhani itakuwa mgogoro mdogo au mnatarajia kuwezekana Kutukia Vita vya Tatu ya Ulimwengu?
Rais AbdelNasser: Tendo yoyote yenye Jeuri dhidi ya Misri litaathari ulimwengu wote kutoka Bahari ya Atlantiki mpaka Bahari ya Hindi, na nchi zote za Kiarabu zitakuwa upande wetu moja kwa moja.
Swali la mhojiwa: maoni yenu ni nini kuhusu kuwasili vikosi vya Ufaransa Mashariki ya Kati?
Rais AbdelNasser: Ninadhani kwamba hatua hizi zina malengo mawili; Kwa upande zinasisitiza umuhimu wa eneo la kimkakati la Cyprus kama msingi wa vita kwa Magharibi, na kwa upande mwingine zinaashiria matayarisho ya kivita kumkamata Suez.
Swali kutoka mhojiwa: Katika siku hizi Ubalozi wa Ufaransa unaweka shinikizo kwa wafuasi wake ili kuondoka nchi hiyo , hata kwa kuweka meli ili zinawasafirisha ovyo wao, mnadhani vita vya mishipa au Ufaransa inakabiliana na mashambulizi ya kijeshi kwa ukweli?
Rais Nasser: Ninadhani kwamba vita vya mishipa hivi wanavyojaribu kuvipiga si lolote ila vita vya mishipa dhidi yao wenyewe. Ama sisi, tunatayari kuamini nia za dhati, na tunatayarisha kwa nguvu zetu zote kukabiliana nao. Kuhusu kinachotokea katika Ufaransa kwa sasa kinawatia hofu tu watu wa Ufaransa na wale wanaokaa katika Misri, sio wamisri.
Swali la mhojiwa: Unadhani kwamba hali hii ya matukio, kusafirisha meli katika Cyprus na tatizo la Suez itaweka wazi suala kuu la Cyprus la kitaifa kwenye matatizo?
Rais AbdelNasser: Kama unavyojua - wamisri, serikali, na mimi binafsi - daima tumeunga mkono upande wa Ugiriki kwenye tatizo la Cyprus, na tutaiunga mkono hadi ushindi wake wa mwisho, na ninaamini kwamba haki za kimataifa zitashinda mwishowe.
Swali la mhojiwa: mnadhani kwamba nchi za Kiarabu zitaiunga mkono Ugiriki katika kurejea kwake Umoja wa Mataifa?
Rais AbdelNasser: Ndiyo, nadhani hivyo.. aghalabu yao , labda hata zote.
Swali la mhojiwa: Kesho utapokea kamati ya watu watano ya Mkutano wa London, je mnaweza kunizungumzia kuhusu maelezo yake.
Rais AbdelNasser: Nitawapokea kwa sababu ninataka kuwaonesha Imani yangu nzuri, na ninataka kusikiliza maoni yao.
Swali la mhojiwa: Je, mtajadili mtazamo huu?
Rais AbdelNasser: Nataka kuwasikiliza, Unaelewa vizuri kwamba sitambui nia mbaya ya mataifa makubwa kuhusu suala la uhuru wa kusafiri kwenye Mfereji. Uingereza haijawahi kuheshimu maneno yake wakati sisi daima tumekuwa tukiyaheshimu maneno haya. Kwa haki gani wanatangaza: Tunafanya. huziamini ahadi za AbdelNasser?! Mfereji wa Suez ulikuwa kiungo cha mwisho cha uvamizi wa wakoloni huko nchini Misri, jambo ambalo hatulikubali. Hatuna nia ya kuondoka kwenye mfereji huo kwa manufaa ya uvamizi wa kimataifa wa pamoja, na tumetoa hakikisho zote za uhuru wa urambazaji. Mfereji wa Suez unapitia eneo la Misri, na ikiwa vita ni muhimu ili kuulinda, tuko tayari kuulinda.
Swali la mhojiwa: Unaonaje nafasi ya Uturuki kwa ujumla na hasa kuhusu tatizo la Ugiriki?
Rais AbdelNasser: turuki inaendelea kufuata sera ya ajabu. Hivi majuzi nimefahamu kutoka Waziri Mkuu wa Libya kwamba itaunga mkono maoni ya kimisri katika mkutano wa London, na alivunja ahadi yake dakika za mwisho. Nafasi ya Uturki imeachia athari kubwa kwenu.
Swali la mhojiwa: Uamuzi wa Ugiriki wa kukataa kuhudhuria mkutano wa London ulikuwa na athari gani kwako?
Rais AbdelNasser: Tumefurahishwa sana na msimamo wa Ugiriki, na kwa mara nyingine tena ni wazi kabisa kwamba tunakabiliwa na matatizo makubwa ya kimataifa na tumepewa shauku ileile ya kisiasa.
Swali la mhojiwa: Una jambo unalotaka kuwaambia Wagiriki wa Misri?
Rais Nasser: Ninawaona kati yetu.. kama Wamisri. Nadhani wana majivuno kama Wamisri na wanaipenda Misri, na watu wetu wanahisi vivyo hivyo. Watu hawa wawili wana mizizi kubwa ya zamani, na kipindi kipya cha shughuli sasa kinafunguliwa mbele yao. Nataka sana kwenda Ugiriki, na kwa ujumla nimealikwa na serikali ya Ugiriki.
Mazungumzo ya Rais Gamal AbdelNasser pamoja na jarida la Ugiriki "Catamireny".
Mnamo Septemba 10, 1956.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy