Harakati ya Nasser kwa Vijana yazindua mfululizo wa kwanza wa mikutano kuhusu suala la Palestina

Imefasiriwa na/ Amr Ashraf
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Harakati ya Nasser kwa Vijana iliyofanyika Ijumaa jioni, Novemba 24, majadiliano ya jopo yenye kichwa "Mgogoro wa Kiarabu na Israeli na Athari zake kwa Usalama wa kikanda wa eneo hilo", ndani ya muktadha wa mpango wa Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa kuongeza ufahamu wa hali za kikanda na kimataifa na masuala kwa wanachama wake, ikiwa ni pamoja na vijana na mabalozi wa Harakati, na majadiliano ya jopo yalisimamiwa na mtafiti katika masuala ya Afrika Islam Fikri Najm El-Din, Mtafiti wa Shahada kwenye Shule ya Uzamili ya Mafunzo ya Afrika na Mkurugenzi wa Uwajibikaji wa Jamii katika Kampuni ya Umoja wa Mkataba Mkuu.
Katika muktadha unaohusiana, majadiliano ya jopo yalishughulikia mada kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na:
- Harakati ya Kizayuni ya ulimwengu na asili yake.
- Mipango ya makazi ya Judaize ardhi ya Palestina ya kihistoria.
- Itifaki za Wazee wa Sayuni na Azimio la Balfour mnamo mwaka 1917.
- Mizizi ya mgogoro wa Waarabu na Israeli.
- Vita vya Waarabu na Israeli (vita vya upanuzi na sera ya utwaaji)
- Kampeni kubwa ya utakaso wa kikabila na kuhama makazi ya Wapalestina tangu mwaka 1948-1982.
- Hali ya ndani ya Kiarabu, mahusiano ya kisiasa ya Kiarabu na fursa ya Israeli.
- Mkataba wa amani.
- Mkataba wa Oslo, Madrid, mnamo mwaka 1991
- Intifada ya pili ya Palestina mwaka 2000-2005
- Mapambano ya watu wa Palestina tangu vita vya heshima 1968 hadi mafuriko ya Al-Aqsa 2023.
- Mgogoro wa silaha kati ya Fatah na Hamas mwaka 2007 na athari zake hadi mwaka 2023.
- Mamlaka ya kikanda na jukumu lao katika mgogoro wa Kiarabu na Israeli na athari zake.
- Hatari ya Uyahudi duniani kwa Uislamu na Ukristo.
Hii ilikuja ndani ya mfumo wa jitihada za Harakati ya Nasser kwa Vijana kuanzisha vijana na makada wa kisiasa kwa vigezo vya kikanda na kimataifa na athari zao kwa watu na uwezo wao.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy