"Amany Khodair" Mwanachama wa timu ya kitaaluma kwa Udhamini wa Nasser, alitajwa kuwa Mhandisi mwanamke mwenye ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika 2021

Mhandisi Amany Khodair mjumbe wa kamati ya kitaaluma kwa Udhamini wa Nasser "Uongozi wa Kimataifa" na Mkuu wa Sekta ya Ufuatiliaji wa Miradi ya Afrika kwenye kampuni ya Arab Contractors, alishinda kwa matokeo ya kura iliyofanyika ndani ya orodha ya wahandisi wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika kwa mwaka 2021 uliopita.
Hiyo ilitokea kwenye mpango uliotolewa na kamati ya "Committee of Women in Engineering ", hiyo ni mojawapo ya kamati za shirikisho la mashirikia ya uhandisi Afrika "(FAEO) Federation of African Engineering Organizations", kusherehekea jukumu muhimu la wahandisi wanawake waafrika na kuwapa Shukrani ipasavyo kwa ushiriki wao kwa wahandisi wenzao wa kiafrika katika miradi ya maendeleo Barani Afrika.
Hiyo ilikuja kutokana na kuteuliwa kwake na kamati ya mahusiano ya kimataifa na masuala ya Afrika kwenye Chama cha Wahandisi wa Misri, kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kusaidia mahusiano kati ya Misri na ndugu zake katika nchi za Afrika katika uwanja wa uhandisi na kwa uzoefu wake mkubwa zaidi ya miaka 25 wakati wa kazi yake na kampuni ya Arab Contractors.
Katika muktadha huo, inatajwa kuwa Mhandisi Amany Khodair, kupitia kazi yake kwenye kampuni ya Arab Contractors, tangu kuhitimu kutoka Kitivo cha uhandisi, Chuo Kikuu cha Kairo, idara ya kiraia, amechangia katika utafiti, ufuatiliaji na usaidizi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kampuni katika nchi nyingi za bara la Afrika, ambayo ni pamoja na madaraja, barabara, majengo ya serikali, hospitali na mabwawa... Pamoja na jukumu lake la kipekee katika shughuli za kamati ya mahusiano ya kimataifa na masuala ya kiafrika kwenye Chama cha wahandisi kwenye uwanja wa mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa kiafrika na uhamisho wa uzoefu wa Misri kwao, ambayo huongeza kuunganisha na kuimarisha mahusiano na Misri.
Pia Mhandisi "Amany Khodair" alishiriki kama mzungumzaji na mhadhiri katika vikao vingi vya mazungumzo na mijadala ya jopo miongoni mwa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa "Uongozi wa Kimataifa", na baadaye, ikiwa ni pamoja na hotuba ukiwa na kichwa cha "jukumu la asasi za kiraia katika kusaidia mahusiano ya watu wengi kati ya Misri na nchi za bara la Afrika", na kikao kingine cha "Fursa za uwekezaji Barani Afrika",miongoni mwa shughuli za siku ya kumi kutoka Udhamini wa Nasser kwa "Uongozi wa Kimataifa", kundi la kwanza, Julai 2019, pamoja na Ufadhili wa Urais wa Baraza la Mawaziri.