Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wahitimu kushiriki kwenye Mkutano "Nchi za Kiarabu katika Ghuba na Jamii za Armenia"

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wahitimu kushiriki kwenye Mkutano "Nchi za Kiarabu katika Ghuba na Jamii za Armenia"
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wahitimu kushiriki kwenye Mkutano "Nchi za Kiarabu katika Ghuba na Jamii za Armenia"
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wahitimu kushiriki kwenye Mkutano "Nchi za Kiarabu katika Ghuba na Jamii za Armenia"

Imetafsiriwa na:  Rana Ibrahim
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Bwana Hagop Makdis, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la tatu (2022), mwanzilishi wa Kituo cha Armarabia na mhadhiri wa chuo kikuu katika Chuo cha Utawala wa Umma, alishiriki katika mkutano wa kimataifa "Nchi za Kiarabu katika Ghuba na jamii za Armenia: mwenendo wa sasa na masuala", inayolenga kujadili fursa za ushirikiano kati ya Jamhuri ya Armenia na nchi za Kiarabu, pamoja na mwenendo wa maendeleo ya jamii za Armenia katika nchi hizi.


   
Mkutano huo ulihudhuriwa na wanadiplomasia kadhaa, ikiwa ni pamoja na Balozi wa kwanza wa Armenia katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Balozi wa Armenia nchini Jamhuri ya Tunisia na Ufalme wa Moroko Dkt. Arshak Bouladian, Balozi wa Armenia huko Erbil, Iraq Kurdistan Arshak Manoukian, Balozi Bahaa Desouki, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa Armenia na Georgia, Kaimu Balozi wa Falme za Kiarabu kwa Armenia Ahlam Rashid Al-Salami, Kaimu Balozi wa Iraq kwa Armenia Suhailan Khalil Al-Jubouri, na Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria kwa Armenia Nora Arisian na wengine, pamoja na wawakilishi wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Jimbo la Yerevan, wasomi na wageni.

Wakati wa mkutano huo, Hagop Makdis alizungumzia umuhimu na jukumu la vijana katika mfumo wa mahusiano ya Kiarmenia na Kiarabu kwa jamii zote mbili na jinsi ya kujenga daraja kwa nchi za Ghuba, nchi za Mashariki ya Kati na Afrika kupitia uwezeshaji wa vijana katika jamii, na katika hotuba yake aligusia umuhimu wa programu za vijana katika ulimwengu wa Kiarabu kama vile Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, iliyoshiriki katika toleo lake la tatu, lililofanyika chini ya Ufadhili ya Rais wa Jamhuri na chini ya kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", katika kipindi cha Mei 30 hadi Juni 15, 2022 katika mji wa Kairo. Hii inaonesha juhudi za serikali ya Misri na juhudi zake za kuimarisha jukumu la vijana ndani ya nchi, kikanda, bara na kimataifa.

Katika toleo lake la tatu, Udhamini wa Nasser  kwa  Uongozi wa Kimataifa unachukua marejeleo kadhaa, kama vile Dira ya Misri 2030, Ajenda ya Afrika 2063, Mkataba wa Vijana wa Afrika, Mpango wa Umoja wa Afrika wa Uwekezaji katika Vijana, Kanuni za Bandung, Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, kama nyaraka za kumbukumbu ambazo Udhamini huo unategemea.