Mwaliko wa dua na maombi... Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ahitaji sala zenu 

Mwaliko wa dua na maombi... Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ahitaji sala zenu 

Kwa matumaini, dua na maombi, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wasubiri kupona haraka kwa kiongozi kijana Abdullah Yassin, ambaye ana michango mingi kwenye nyanja za mawazo, mafunzo, Ukarabati na mipango ya jamii.

Mtafiti na Mwanaharakati kwenye kazi za jamii, "Abdullah Yassin", Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ni mmoja wa viongozi muhimu na maarufu wa asili kwenye Misri ya Juu, huko Mkoa wa Luxor, Mjumbe wa Sera na Maendeleo ya Biashara kwenye Ofisi ya Waziri wa Vijana na Michezo, na Mkuu wa Sekta ya Misri ya Juu kwenye Shirika ya Benki ya Al-Khair kwa Maendeleo endelevu pamoja na kuwa mratibu wa mpango wa maendeleo katika Wizara ya Vijana na Michezo, na mshauri wa Ufuatiliaji na tathmini ya mradi wa Forsa unaotekelezwa kupitia Shirika ya Misri kwa Maendeleo yenye Uhusiano na Wizara ya Mshikamano na Ustawi wa Jamii, pamoja na kuwa Katibu Mkuu Kwa Bunge la Vijana la Misri, mratibu wa mpango wa huduma kwa vijana wa Upainia, pamoja na kazi yake ya awali katika Idara ya mahusiano ya Umma katika Hospitali ya Al-Shifa Orman Oncology huko Luxor, na mratibu wa shamba la mpango wa Nour Hayat kwa kupambana na sababu za Upofu chini ya Ufadhili wa Mfuko wa Tahya Misr.

Jina lake lilijitokeza kwenye Uwanja wa mafunzo na Ukarabati huko Misri ya Juu na alikuwa na alama zake za kipekee katika kuinua Ujuzi wa makada wengi wa vijana, kama alivyofanya kazi kama mkufunzi kwenye Kamati ya Mafunzo ya Uongozi wa Vijana ya Wizara ya Vijana na Michezo, pamoja na jukumu lake kama mkufunzi kwenye Uwanja wa Ujuzi wa maisha kwenye Mfuko wa Kupambana na Dawa za Kulevya, na meneja na mkufunzi katika kampeni (Kwa sababu Mimi ni Mwanaume) chini ya Ufadhili wa Shirika la Baraza la Taifa la Wanawake, pamoja na kuwa mkufunzi katika mradi wa Ufahamu wa kifedha kwenye Taasisi ya Benki, pamoja na kazi yake kama mkufunzi katika mradi wa kuboresha fursa za kujiajiri, na kupunguza hali ya Uhamiaji haramu chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Biashara la Umoja wa Ulaya(EU). 

Kuhusu michango yake ya kiakili, hivi karibuni alichapisha kitabu kiitwacho (Jukumu la Miradi ya Maendeleo na Athari zao kwa Familia zilizo na Utunzaji wa Msingi), ambacho huja kama Upanuzi wa Tasnifu ya Mwalimu yake kwenye Uwanja wa sera za Umma.