Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Kenya akutana na Wahitimu wa Kundi la Kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi
 
                                Imetafsiriwa na: Hager Mohamed
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 
Wahitimu wa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi nchini Kenya walikutana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Kenya, Bw. Peter Minya, na maafisa mbalimbali wa serikali, wakati wa kuhudhuria uzinduzi wa Mashindano ya Udhamini ya MbeleNaBiz ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo kwa msaada wa kifedha kuendeleza miradi yao, inayokuja kwa ushirikiano kati ya serikali yao na Benki ya Dunia, na pia walishiriki katika vikao vya kujadili njia za ushirikiano na ubia kati ya sekta tofauti.
 
                         
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
                                        
                                     
            
            