Mhitimu wa Udhamini wa Nasser akutana na Msemaji rasmi wa Serikali ya Jamhuri ya Congo
Imetafsiriwa na: Hagar Moslleh abdelmoaty
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Mheshimiwa Jean-Christ Bondungu Bukaka, Mshirika wa Udhamini wa Nasser, alikutana na Waziri wa Mawasiliano na Habari, na Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Congo, Mheshimiwa Thierry Lizin Mongala Ijumaa, Julai 5, 2019.
Wakati wa mkutano wao, walizungumzia kuhusu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, ambayo ni fursa ambayo inafungua milango kwa vijana wa Congo, wakijua kwamba Bwana Jean-Christ aliheshimiwa kuchaguliwa kushiriki katika mpango wa Udhamini na kuwakilisha nchi yake Congo.
Pia walizungumzia umuhimu wa kufikisha taswira nzuri ya nchi na kueneza habari njema kuhusu nchi, ili dunia ijue kuwa Congo sio nchi inayounga mkono ukatili.