Udhamini wa Nasser wakuza Bara Duniani...Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika
Imefasiriwa na / Zeinab Mekky
Dkt.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri alisema: “Sambamba na maadhimisho ya miaka sitini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (Umoja wa Afrika sasa), na maandalizi ya kuzindua toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ambalo limepangwa kufanyikwa Juni hii ya 2023, ambalo ni muendelezo wa juhudi za taifa la Misri, katika kutekeleza jukumu lake lililopewa katika kuimarisha nafasi ya vijana ndani, kikanda, Barani na kimataifa kwa kutoa aina zote za usaidizi, kuwezesha na mafunzo, kwa kuzingatia Ajenda ya Afrika 2063 kama mojawapo ya nyaraka za bara ambalo Udhamini huo unategemea.

Sobhy alisisitiza kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulikuwa na nia ya kupaza sauti ya bara la Afrika Duniani kote, ambapo Udhamini huo wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulizinduliwa katika toleo lake la kwanza mnamo Juni 2019 kama Udhamini wa (Kiafrika-Kiafrika) kwa ushiriki wa vijana 120 viongozi kutoka nchi zipatazo 28 za Afrika sambamba na Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, na
Kueneza kwa Nasser Barani na kimataifa kimefikia takriban nchi 93 Duniani kote, na sehemu ya bara la Afrika ni takriban nchi 49, akiashiria kwamba Udhamini wa Nasser kupitia toleo lake lilopita umejali kuangazia masuala ya Afrikia yaliyo muhimu zaidi ndani ya meza ya mazungumzo na umetoa mapendekezo mengi yaliyofikia wenye uamuzi
Vilevile Waziri huyo alielezea kuwa bara la Afrika mnamo kipindi cha miaka minne ndilo maarufu zaidi kwa Udhamini huo, akieleza kuwa toleo la kwanza lilizinduliwa kwa ushiriki wa Waafrika 100%, kisha Udhamini huo uliongezeka katika toleo lake la pili kwa kauli mbiu ya " Ushirikiano wa Kusini_Kusini”, kwa kupokea vijana wa Asia na Amerika ya Kusini, na bado Afrika ilirekodi idadi kubwa zaidi Idadi ya waombaji iliongezeka kwa takriban 56.7%, kisha idadi ya Vijana waafrika kupata Udhamini wa Nasser katika toleo lake la tatu mnamo 2022 iliongezeka hadi kufikia. takriban 84.6%, huku takwimu zikithibitisha kuwa licha ya nchi zipatazo 93 Duniani kwa Udhamini wa Nasser mwaka huo kama sehemu ya maandalizi toleo la nne, asilimia ya waombaji wa Kiafrika ilifikia takriban 84.7% ya jumla ya waombaji.