Wakati wa ziara yao kwa Bi.Harusi wa Mediterania (Alexandrina) ... Wajumbe wa "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" wakutana na Mkurugenzi wa maktaba ya Alexandrina

Wakati wa ziara yao kwa Bi.Harusi wa Mediterania (Alexandrina) ... Wajumbe wa "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" wakutana na Mkurugenzi wa maktaba ya Alexandrina

Wajumbe wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la nne, walifanya ziara huko mkoa wa Alexandria, kwa mahudhurio Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Bw.Hassan Ghazali na kundi la viongozi kutoka Wizara ya Vijana na Michezo, watangazaji wa vyombo vya habari na waandishi wa habari.

Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea Maktaba ya Alexandria, ambapo walikutana na Dkt. Ahmed Zayed, Mkurugenzi wa Maktaba ya Alexandria, aliyekaribisha ziara ya washiriki wa Udhamini huo kwenye maktaba, akiashiria wakati wa hotuba yake kuwa ziara ya maktaba ya Alexandrina ni miongoni mwa matukio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni moja ya ziara muhimu zaidi kwa sababu inaakisi dhana ya utaasisi na kazi ya pamoja. Na katika hotuba yake, Zayed aligusia kuwa Udhamini wa Nasser ulikuwa sababu ya safari yake kwenda Uingereza, na alitaja idadi kadhaa ya masomo kwa ajili yake juu ya Rais wa zamani sana Gamal Abdel Nasser.

Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Bw.Hassan Ghazali, wakati wa hotuba yake, alielezea kuwa ziara hiyo inakuja miongoni mwa umakini wa Wizara ya Vijana na Michezo wa kunufaika na matukio na shughuli muhimu, mashindano na matukio ya kimataifa yanayofanyika nchini Misri ili kutangaza maeneo yake mbalimbali ya kitalii na kiakiolojia, kwa uratibu na mamlaka mbalimbali husika na kila ziara ili viongozi wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ili kujifunza kuhusu maeneo muhimu zaidi ya utalii na mambo ya kale nchini Misri.

Ziara hiyo ilijumuisha kuwatambulisha washiriki kwenye maktaba na sababu ya kujenga maktaba hiyo katika umbo la Duara la Jua, tarehe ya kuanzishwa kwake, na urithi na vitabu maarufu vilivyomo vinavyoelezea tamaduni zote, iliyoifanya kuwa moja ya picha muhimu zaidi za sayansi na utamaduni katika ngazi ya kikanda na kimataifa. Na pia, vijana walioshiriki katika Udhamini huo walitambulishwa kwa huduma mbalimbali za utafiti na kidijitali zilizotolewa na maktaba kwa watafiti na wageni.

Pia, Wajumbe  Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, walikagua kumbi za Maktaba ya Alexandria na makumbusho yake matatu, likiwemo jumba la makumbusho la Marehemu Rais Al-Sadat, pamoja na maonesho mbalimbali katika maktaba hiyo yaliyofikia idadi 16, kisha alitazama onesho la panorama ya kiutamaduni, ambapo usuli wa kihistoria wa ustaarabu wa Misri na Mafarao, Uislamu na Ukristo uliwasilishwa  nchini Misri.

Ziara ya washiriki wa Udhamini huo katika toleo lake la nne, ilihitimishwa kwa ziara  bure katika Jimbo la Alexandria,  kwa upande wao, Wajumbe Vijana katika Udhamini wa masomo hayo walielezea furaha yao kubwa ya kumtembelea Harusi wa Mediterania (Alexandrina), kwa kuona vivutio muhimu zaidi, na kufurahia hali ya hewa yake ya kiangazi, na pia walichukua picha nyingi na video za kuona.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mojawapo ya mifumo ya utendaji ya kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, ili kusaidia vijana waafrika waliohitimu, kuwawezesha kuunda maono ya kina na muhimu kuhusiana na masuala ya kimataifa na mipango ya Maendeleo Endelevu, na fursa za kusaidia kukuza jukumu la Misri Duniani kote.