Wajumbe wa “Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa” watazama filamu ya “Kwaheri, Bonaparte” katika Kituo cha Ubunifu kwenye Nyumba ya Opera ya Kairo

Wajumbe wa “Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa” watazama filamu ya “Kwaheri, Bonaparte” katika Kituo cha Ubunifu kwenye Nyumba ya Opera ya Kairo

Wajumbe Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la nne, walitazama filamu ya “Kwaheri, Bonaparte” ya Mtoaji wa Sinema marehemu Youssef Chahine, iliyoigizwa na Mohsen Mohi El-Din, Michel Piccoli, Mohsna Tawfiq, Hoda Sultan, Patrice Sherou, Jamil Ratib, Salah Zulfikar na Tahia Carioca, wakati walipotembelea kituo cha ubunifu kwenye Nyumba ya Opera ya Kairo.

Kando ya ziara hiyo kulikuws na mkutano wa mazungumzo kuhusu filamu hiyo, mkutano huo pia ulihusisha mazungumzo kuhusu mwongozaji maarufu, Youssef Chahine na kazi zake muhimu zaidi, kwa mahudhurio ya Sayed Fouad, Mkuu wa Tamasha la Luxor la Sinema ya kiafrika, Sherif Mandour, Mzalishaji, Mkurugenzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Tamasha la Luxor la sinema ya Afrika la, na msanii Mohsen Mohi El-Din, bingwa wa filamu ya “Kwaheri, Bonaparte”, na mkutano ulisimamiwa na Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini huo.

Ghazali wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa Udhamini huo, alionesha kwamba msanii Mohsen Mohi El-Din, bingwa wa filamu ya “Kwaheri, Bonaparte”, alikuwa na bado anawakilisha kichwa hicho hata kwa jinsi alivyozungumza na hisia zake ambazo zilionekana wakati wa filamu na jinsi alivyotamka sauti za shangwe hizo, akieleza kuwa kupitia Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kuwatambulisha ndugu kutoka nchi mbalimbali haswa za kiafrika, kwamba tuna Sinema ambayo imekita mizizi, ambapo ni kongwe kuliko baadhi ya nchi za Ulaya, na kongwe kuliko baadhi ya nchi kubwa za kwanza Duniani, jambo ambalo linathibitisha kuwa Afrika haiko nyuma katika kila jambo kama inavyokuzwa daima.

Kwa upande wake Sayed Fouad, Mkuu wa Tamasha la Luxor la Sinema ya kiafrika, alisema kuwa tamasha hilo lilianza tangu miaka 13, na linajiandaa mwezi ujao wa Aprili kwa ajili ya shughuli za toleo la 13, huku akibainisha kuwa tamasha hilo linavutiwa na linahusu Sinema ya kiafrika tu ambapo ilifanikiwa kuwaleta watengenezaji wa filamu  Barani Afrika kwenda Misri, vilevile katika kurudisha filamu ya Misri kwa nchi za Afrika, tamasha hilo pia lilianzisha Klabu ya Sinema ya Kiafrika, na “Fouad” aliongeza kuwa Misri ilianza Sinema miaka 127 iliyopita, akisisitiza kuwa sinema ya kiafrika ni sinema muhimu Duniani.

Katika hotuba yake, Mkurugenzi Sherif Mandour aliwakaribisha washiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na akarejea mwanzo wa kazi yake katika uwanja wa Sinema, uliokuwa na mkurugenzi mkuu marehemu, Youssef Chahine, ambaye alijifunza mengi kutoka kwake, Mandour, na kupitia hotuba yake, Mandour alishughulikia safari kubwa ya Youssef Chahine iliyoanza kwa filamu ya “Baba Amin”, hadi filamu ya “Heya Fawda” akiongeza kuwa Youssef Chahine kwenye filamu ya “Kwaheri, Bonaparte” aliweza kuanzisha kipindi cha wakati kuhusu uvamizi wa Ufaransa, na pia alikuwa na lengo lingine ambalo alitaka kuliwasilisha, nalo linahusiana na wazo la kutokuwepo kwa vizuizi kati ya tamaduni tofauti.

Msanii, Mohsen Mohieldin, bingwa wa filamu ya “Kwaheri, Bonaparte” alieleza wakati wa hotuba yake kuwa, siku zote, sanaa ndiyo inayowakutanisha watu wote pamoja na tamaduni zao tofauti, akibainisha kuwa wapo hapa, kupitia mkutano huu, wakiwakilisha mbegu nzuri ili kufafanua tamaduni za kila mmoja na kuelewana zaidi, Mohi El-Din alisisitiza kuwa Mtoaji mkuu wa Sinema Youssef Chahine ni mwongozaji wa kimataifa ambaye siku zote alikuwa alijitahidi kufanya filamu ya Misri kuwa na mwelekeo mwingine wazi kwa dunia nzima, pamoja na kuvutiwa kwake na kuitangaza filamu ya Misri nje ya nchi na kushiriki katika matamasha ambalo alifanikiwa kuifanikisha haswa kupitia filamu nyingi alizozitengeneza akiwa mzalishaji kushirikiana na nchi nyingi, bingwa wa filamu hiyo alibainisha kuwa Youssef Chahine alikuwa akiwasilisha dhana ya kisiasa, kiutu na kiutamaduni ambapo alizungumzia kila jambo linalohusu maisha ya mtu, iwe vita, ubakaji au ukoloni, hata yale yanayohusiana na mahusiano ya kibinadamu ambayo madaraka yanaathiri mwingine kutokana na hitaji lake, ambapo kila mara alikuwa akitoa dhana ya jinsi ya kumkubali mwingine na utamaduni wake tofauti bila kuingilia kwa kumhukumu, akizingatia kuwa filamu ya “Kwaheri, Bonaparte,” iliyoanza kurekodiwa mnamo Mwaka wa 1983, sio hadithi tu juu ya uvamizi wa kifaransa huko Misri, bali pia inaendana na zama zetu za sasa na zama zote zijazo.

Inatajwa kwamba  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa inafanyikwa na usimamizi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na uangalizi wa waandishi wa habari na vyombo vya habari wa Mamlaka ya Kitaifa ya waandishi wa habari na Mamlaka ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari.