Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wakaribishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wakaribishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri


Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri iliwakaribisha viongozi  vijana  walioshiriki katika toleo la nne la  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo, pamoja na Ufadhili wa  Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri,  hilo kwa  ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka nchi 55 kutoka mabara ya Afrika, Asia, Ulaya, Amerika Kusini na Australia.

Ziara  hiyo ya washiriki wa Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa,  katika toleo lake la nne, lilijumuisha mihadhara kadhaa  ambayo ni miongoni mwa programu ya mafunzo iliyoandaliwa na Sekta ya Mashirika na Jumuiya za kiafrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, kwa  ushiriki wa Balozi Ahmed Nihad Abdel Latif, Mkurugenzi wa Kituo cha Kairo cha Utatuzi wa Mizozo kwa kueneza  Amani , na Balozi Mohamed Jaber, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kwa Mashirika na jumuiya za kiafrika, na Balozi Ihab Badawi, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa Masuala ya Kimataifa na Usalama wa Kimataifa ,  hayo kwa   mahudhurio ya Bw. Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa  Udhamini wa  Nasser  kwa Uongozi wa Kimataifa , na kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, watangazaji  na waandishi wa habari.

Balozi Ahmed Nihad Abdel Latif, Mkurugenzi wa Kituo cha Kairo cha Utatuzi wa Migogoro kwa kueneza Amani , wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa  Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  ,  aliashiria jukumu la Kituo hicho la Migogoro na kueneza Amani  katika kufanikisha  kongamano la COP27 katika mji wa  El- salam huko Sharm El-Sheikh, ambalo lilithibitisha kwa  ulimwengu  kwamba Misri inaweza Kuzingatia masuala ya hali ya hewa katika  hali halisi, na "Abdul Latif" alionesha jitihada kubwa ambazo Misri inazifanya  ili kuimarisha pamoja na  nchi ndugu za Kiafrika, pamoja na juhudi ambazo Misri inazifanya katika masuala mbalimbali muhimu ya kisiasa ya kimataifa. vilevile , alielekeza vijana  kwa umuhimu wa kuzingatia matatizo ya nchi zao na kushirikiana ili kutoa mawazo yanayosaidia kuunda  suluhu za kiubunifu kwa matatizo Duniani kote.

Kwa upande wake, Balozi Muhammed Jaber - Naibu na msaidizi  wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa Mashirika na Jumuiya za kiafrika - alifafanua hayo wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa Udhamini huo , jukumu muhimu linalofanywa na Misri Barani Afrika ambalo ni ndani ya juhudi za kuleta maendeleo kwa Bara la Afrika na kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu na malengo ya Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 hasa suala la usalama  wa Chakula na misaada inayotolewa na Misri kwa nchi za Afrika zinazokabiliwa na ukosefu wa chakula.

Balozi Ehab Badawi, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Kimataifa na Usalama wa Kimataifa, aliangazia, wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser wa uongozi wa kimataifa , vipengele vya msimamo wa Misri ili kuimarisha harakati isiyofungamana na upande wowote, na jinsi ya kushinda majanga ya   kimataifa ya sasa ambayo  inajumuisha Usalama wa nishati , chakula na mfumuko wa bei .Pia alizungumzia katika hotuba yake uzoefu imara wa Misri Katika  kiwango cha  bara katika nyanja za mawasiliano, teknolojia ya habari na ujasiriamali.

Mijadala wakati wa mihadhara hiyo ilijulikana  kwa ushirikishaji na mwingiliano ambapo viongozi vijana walioshiriki katika  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  wakijadiliana na mabalozi hao kuhusu masuala mengi muhimu yanayoonyesha kiwango cha ujali wako na mwingiliano wao , na miongoni mwa masuala hayo ni masuala ya maendeleo katika Afrika na kukabiliana na Ugaidi na yale yaliyokumba ulimwengu wakati wa janga la Corona na kilichotolewa na Misri wakati huo kutoka misaada   kwa ndugu zake, vilevile  masuala yanayohusu  vijana  na wanawake yalitiwa  maanani mkubwa kutoka kwa washiriki .


Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser  kwa Uongozi wa Kimataifa, Hassan Ghazali, alisema kuwa katika toleo la nne la Udhamini huo ,  viongozi vijana 150 kutoka mabara ya Dunia kutoka nchi 56 Duniani, haswa nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi marafiki wanashiriki katika Udhamini huo, pamoja na Ufadhili wa  Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, na uangalizi wa  taasisi ya kitaifa ya uandishi wa habari    ambapo waliteuliwa wanaoshiriki katika Udhamini huo  ambao ni wajasiriamali vijana , wafanyakazi  kwenye mashirika ya jamii ya kitaifa  na    idadi ya watoa maamuzi katika sekta ya umma katika nchi zao .


"Ghazali" aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuwawezesha vijana, na kutoa fursa kwa wenye  bidii kutoka nchi mbalimbali duniani ili  kuwasiliana  pamoja na kuanzisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali, siyo tu katika ngazi ya bara bali hata kimataifa na kati ya nchi za Kusini, na kuimarisha uwezo wa kujitegemea  kwa  nchi zinazoendelea kupitia kubadilishana ujuzi na kukuza uwezo wao wa kibunifu wa kupata suluhu kwa matatizo yao ya kimaendeleo jambo ambalo linaenda na  matarajio yao, maadili na mahitaji maalum.


Vilevile , inajulikana kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  ni mojawapo ya mifumo ya utendaji ya kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri,  ili kusaidia vijana waafrika wenye uzoefu, kuwawezesha kuunda maono ya kina na muhimu yanayohusishwa na masuala ya kimataifa na mipango ya maendeleo endelevu, na kuunga mkono fursa za kutangaza jukumu la Misri ulimwenguni kote . vilevile , inakuja ndani ya mfumo wa utekelezaji wa maono ya Misri ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.