Afya Barani Afrika ..kikao cha Mazungumzo Miongoni Mwa Shughuli za Siku ya Tano ya Udhamini wa Nasser

Kikao kimepangwa kwa Anwani "Afya Barani Afrika" miongoni mwa shughuli za Siku ya Tano kutoka Udhamini wa Nasser, kwa mahudhurio ya Dkt. Helmy Al-hadidi, Waziri wa Afya wa Zamani sana, na Waziri ea Taasisi ya Mshikamano wa watu wa Asia na Afrika "Afro-Asia", na Bw. Hassan Ghazali Mratibu wa Ofisi wa Vijana wa Afrika na Mwakilishi wa Mwenyeketi wa Umoja wa Vijana wa Afrika amesimamia kikao hicho.
Mheshimiwa Dkt. Helmy Al-Hadidi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mshikamano wa watu wa Asia na Afrika "Afro-Asia" amesifu majukumu ya Muktadha na Matarajio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika, akisisitiza kuwa marehemu kiongozi Mmisri Mheshimiwa Gamal Abdel Nasser amekuwa Mmisri wa kwanza aliyeamua kuweka misingi ya Mustakabali ya nchi za Afrika na huyo pia alikuwa mwanzilishi wa Kwanza wa vikundi vya Kiarabu na Kiafrika hapa kanda ya Afrika.
Mheshimiwa Al-Hadidi amesisitiza jukumu la marehemu Kiongozi Gamal Abdel Nasser katika kuanzisha harakati za ukombozi na kupata uhuru tena kuondoa ukoloni kutoka maeneo ya Kiafrika, wakati wa hali za ulimwengu zilizobainisha kupambana Marekani katika eneo la magharibi kwa ajili ya kupata uhuru, na vilevile alibainisha kuwa Rais Marehemu Mheshimiwa Gamal AbdelNasser ameinua bandari ya kuomba uhuru na kufikia utulivu unaotarajiwa kwa nchi zote za Afrika, na kwa hivyo ukoloni umeondolewa kwa namna rasmi, ili kujenga akili za Afrika na kufikia maendeleo na mabadiliko kwa nchi zote za Afrika.
Al-Hadidi ameweka wazi kuwa Mheshimwa Gamal AbdelNasser amekuwa na hisia maarufu kwani alikuwa na imani yenye nguvu kuwa thamani za nchi zimepatikana katika raia wake sio katika serikali , jambo hilo lililomsukuma kuanzisha taasisi ya raia kwa ajili ya kuunganisha raia wa nchi za ulimwengu wa tatu, iliyojulikana kama Taasisi ya Mshikamano wa Taasisi za Raia wa Afrika na Asia. Iliyofunguliwa kwa matawi yale katika nchi 103, na kisha imekuwa katika nchi 73, na baadaye jukumu lake limepunguza na baada ya Mapinduzi ya Arab wa masika na hata mabadiliko yake katika Taasisi hiyo, kisha imeanzishwa tena katika Afrika Kaskazini, huko nchini Morocco, Tunisia, Libya, Sudan, Chad, Congo na Brazil, na baadaye kuna tawi lingine limeanzishwa kwa mara yake ya kwanza nchini Pakistani.
AL-Hadidi ameangazia umuhimu wa kuthibitisha imani ya Mshikamano na Usalama inayochukuliwa kama asili thabiti kwa maendeleo, majengo, na mabadiliko kwa raia hawa; akidokeza kuwa Afya ni sehemu muhimu sana katika mbinu ya maendeleo ya kijamii kwani raia wenye magonjwa hawawezi kuzindulia jambo zuri; na kwa hivyo Gamal Abdel Nasser ameanzisha vitengo kadhaa jumuishi katika ngazi ya Jamhuri inayojumuisha maendeleo ya huduma za afya, elimu, na usimamizi wa ndani katika eneo moja ili kutoa huduma kwa jamii, jambo hilo linalidhihirisha upande wa kiraia kwa siasa ya Mheshimiwa Gamal Abdel Nasser, na vilevile upande wa vijana, na kupata wanawake haki zake katika uchaguzi, na hayo yanayofikia maendeleo na maisha bora kwa Bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mshikamano wa Raia wa Asia na Afrika "Afro-Asia" ameweka wazi upatikanaji wa rasilimali za kifedha na kielimu za kutosha unachangia kuendeleza huduma za afya nchini Misri na nchi za Afrika, akidokeza kuwa umasikini na ujinga sababu mbili za ugonjwa na kuwa kusambaza maradhi na magonjwa unaohusiana na hali za kijamii ,kiuchumi ,na hata katika ngazi ya kupatikana vyakula kwa nchi hizo.
Na kwa upande wake Hassan Ghazali, Mwakilishi wa Mwenyeketi wa Umoja wa Afrika amedokeza umuhimu wa uongozi wa kisiasa Barani Afrika katika Afya na hasa kupambana Virusi C, akidokeza kuwa Rais Abdel Fattah El-Sisi amezindulia mpango wa Afya kwa watu wa milioni 100 ili kutibu wana wa Bara la Afrika.
Pia Ghazali amesisitiza jukumu la Taasisi ya Afrika kwa urais wa Dkt, Gamal Shiha, inayochukuliwa kama taasisi kubwa zaidi Barani Afrika inayolenga kupambana virusi vya kiini kwa ujumla, na haswa virusi vya C, akielezea juhudi za wakala wa Kimisri katika ushiriki huu kwa ajili ya maendeleo kupitia kuchangia maendeleo katika nchi kadhaa., hasa nchi udugu za Afrika , katika uongozi wa Misri katika Umoja wa Afrika mnamo 2019, na pia kukamilisha Mfuko wa Afrika ulioanzishwa na Rais Gamal Abdel Nasser.