Vijana na Michezo: Udhamini wa Nasser - Toleo la Nne wakusanya juhudi za Vijana wa Dunia Kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030
Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, toleo la nne, unashughulikia kuhamasisha juhudi za vijana wa Dunia kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Udhamini ambao uko na Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi.
Udhamini huo unatoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili, kama inavyooneshwa na lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, pamoja na kuwawezesha vijana na kutoa fursa kwa watendaji kutoka nchi mbalimbali za Dunia kuchanganyikana na kuanzisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali, sio tu katika ngazi ya bara lakini pia kimataifa, kama inavyooneshwa na lengo la kumi na saba la Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Udhamini huo pia unashughulikia kuongeza nafasi ya vijana ndani ya nchi, kikanda, bara na kimataifa kwa kutoa aina zote za msaada, ukarabati na mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kunufaika na uwezo na mawazo yao, na hivyo ndivyo Rais Sisi alivyoidhinisha na kutangaza wakati wa shughuli za Jukwaa la Vijana Duniani katika matoleo yake yote.
Katika muktadha unaohusiana, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ukapata Uangalifu wa Taasisi ya Kitaifa ya Uandishi wa Habari kwa maandalizi ya uzinduzi wa toleo lake la nne mnamo Juni ijayo, pamoja na Ufadhili wa kisiasa wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.