Vijana na Michezo: “Sameh Kamel” Mwanachama wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashinda Uenyekiti wa kundi kuu la Umoja wa Mataifa kwa Watoto na Vijana

Vijana na Michezo: “Sameh Kamel” Mwanachama wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashinda Uenyekiti wa kundi kuu la Umoja wa Mataifa kwa Watoto na Vijana

Katika pongezi maalum, kupitia Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza ushindi wa Daktari wa Pua, Sikio na Koo wa Misri, Dkt. Sameh Kamel, Mwanachama wa timu ya kazi ya toleo la nne la Udhamini wa Kiongozi Gamal Abdel Nasser, katika uchaguzi wa Uenyekiti wa kundi kuu la Umoja wa Mataifa kwa Watoto na Vijana huko New York, ambao ni mkutano mkubwa zaidi wa Vijana Duniani ambapo uanachama wake unajumuisha zaidi ya mashirika 8,500 ya kimataifa, na yanafurahia uwezo wa kujadili ajenda za kimataifa kwa niaba ya Watoto na Vijana katika Umoja wa Mataifa.

Ushindi wa «Sameh Kamel» kwa nafasi ya Mkuu wa kimataifa unakuja akiwa Mwarabu wa pili katika historia ya kundi hilo, ambapo hapo awali, tangu mwaka wa 2012, ameshawahi kuwa mwakilishi wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika kundi hilo hilo na alisifiwa kwa utendaji bora na wa kipekee wakati ambapo alichangia katika kuendeleza maoni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana 2030, pamoja na mchango wake katika maendeleo ya Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji, pia alishiriki katika majadiliano ya ajenda nyingi za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Ajenda ya Maendeleo endelevu ya mijini “Habitat 3”, Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu 2030, pamoja na kujadili maazimio matatu ya Baraza la Usalama yanayohusiana na Vijana, Amani na Usalama, na Ajenda nyingine za kimataifa, kulingana na tovuti ya Umoja wa Mataifa
https://www.unmgcy.org/secretariat 

Mbali na kuwa Mwanachama wa kamati ya uteuzi kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne na Mwenyekiti wa kisasa wa Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Jukwaa la Vijana wa Kiarabu kwa Maendeleo Endelevu, “Dkt. Kamel” alishiriki kwa muda wa miaka 7 tangu mwaka wa 2016 katika maandalizi ya Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu kwa wadhifa wake ambapo ana jukumu la kukagua nchi za kiarabu zinazowasilisha ripoti za kitaifa za hiari kwa Maendeleo Endelevu, pamoja na maandalizi ya Jukwaa la Vijana la Baraza la Uchumi na Jamii katika Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Dkt. Sameh Kamel alisema kuwa Kundi la Umoja wa Mataifa la Watoto na Vijana lilianzishwa kwa pendekezo la “Mkutano wa Kilele wa Dunia” mnamo mwaka wa 1992 pamoja na kichwa cha Ajenda 21 na uamuzi wa kuanzisha ulianzishwa rasmi wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kikao cha Na. 67 kwa mujibu wa Azimio Na. 290 kwa mwaka wa 2012, akiashiria kwamba mikutano kadhaa ya ngazi ya juu imepangwa kuanza mwaka huu, ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Kilele wa Urais wa Maendeleo Endelevu, Jukwaa la Vijana la Baraza la Uchumi na Jamii, Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu, na jingine linaloitwa “Mkutano wa Kilele wa Mustakabali Tunayoitaka”, pamoja na kuandaa uzinduzi wa Ofisi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa.

Inatajwa kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne uko na Ufadhili wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari vya Kitaifa, pamoja na kupokea Ufadhili wa kisiasa kutoka kwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri kwa mara ya tatu mfululizo, na mwaka huu uko na kauli mbiu ya " Vijana wa kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini" na imepangwa kufanyikwa Juni ijayo.