"Hannibal Al-Saghir" Balozi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa azindua kampeni ya kusafisha mibuga huko Sirte, Libya 

"Hannibal Al-Saghir" Balozi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa azindua kampeni ya kusafisha mibuga huko Sirte, Libya 

Shughuli za vijana na kiraia  mjini Sirte nchini Libya, zikiwakilishwa na taasisi kadhaa za kiraia na vijana, zilizinduliwa kama tathmini ya hali ya mazingira, kisaikolojia na kiburudani inayoruhusu watoto kufurahia nyakati nzuri, kulingana na mwaliko wa Balozi Hannibal Al-Saghir, mmoja wa mabalozi mashuhuri wa Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa,  toleo la tatu na hivyo pia  baada ya mivutano inayothibitisha hali ya shinikizo la kisaikolojia na akili iliyoongezeka kati ya wanafunzi, watoto na vijana kutokana na shinikizo na ukosefu wa nafasi kubwa za kucheza na burudani.

Na baada ya kutangaza matokeo ya tathmini, ambayo inathibitisha ukweli wa haja ya watoto katika mji wa Sirte kwa maeneo ya kijani na maeneo ya burudani ambayo hubadilisha hali yao ya  saikolojia  na huchangia kuboresha ufahamu na uzingatio na kujenga mazingira  halisi ya maisha ya mijini na kurejesha faraja ya kisaikolojia kwa raia  na baada ya zaidi ya muongo mmoja ambapo mji halijapata  bado Uwezo wowote na msukumo katika upande huu nyeti, na kupitia uungaji mkono wa watu pale Serti, Hannibal  alitangaza kuongezea  kampeni za usafi na  urekebishaji wa Sehemu za burudani pamoja na kauli mbiu " ustawi na kujitolea "  na zilikuwa zikiungwa mkono na  mamlaka kadha za ufadhilii huko Libya ikiwa ni pamoja na mpango mpito pamoja na taasisi za serikali kama kampuni ya huduma za usafi   na Manispaa Chini ya usimamizi wa moja kwa moja na uangalizi wa kina wa Meya wa manispaa wa mji wa Sirte, Prof.Dkt.Mukhtar Khalifa Al-Madani, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe Agosti mosi hadi tarehe 15  Septemba, 2022,ambao unajumuisha mibuga na nafasi ya kijani , "kwa usaidizi  wa pamoja kutoka kwa watu na viongozi wa kijamii na wa kitaifa" 

Awamu ya kwanza ya kampeni ya ustawi na  kujitolea ya inalenga kusafisha bustani ya familia iliyo mbele ya mtaa wa  Al-Wafa, pamoja na bustani ya Uhuru iliyo karibu na kituo cha redio cha Sirte; kwa ushiriki wa idadi kubwa ya wajitoleaji kila siku ambapo idadi yao inazidi wanamji 150  ,   ndugu wageni na wahamiaji huko Sirte, na usaidizi mwingine wa logistiki na nyenzo katika suala la Ufadhili  kutoka kwa sekta ya  binafsi.

 licha ya  kampeni hiyo ya usafi, awamu ya kwanza itajumuisha kuweka nguzo za taa zinazotumia nishati ya jua baada ya kupatikana  ufisadi mkubwa kwenye mtandao wa umeme na nguzo za jadi katika bustani hizo ambazo zimesababishwa na vita na migogoro iliyowahi kupita katika bustani hizo. pamoja na kuweka viti   na matengenezo ya kushimba visima na mashimo ya  maji taka na mifereji ya maji ya mvua, kuhamisha mabaki ya vita na kupanda miti na kulima maua na miti ya mapambo katika mibuga zinazohusika na kampeni.

Kwa upande wake, Hannibal Al-Saghir alifafanua kwamba lengo la kampeni hiyo ni kupunguza ukali wa mzozo kati ya makundi ya jamii ya Libya kwa ujumla na haswa Al-Sartawi, na kuongeza juhudi kupitia kutia moyo wa ushirikiano na upendo kati ya wananchi wa mji, akisisitiza kuwa sababu kubwa ya kuanzisha kampeni hiyo ni kuamsha jukumu la vijana wanaoweza  kuunda mabadiliko ingawa kuwepo   upuuzaji , utengaji, ufukuzi,uvivu  na  uhasi ulioenea katika sekta mbalimbali, lililosababisha kuongezeka  kwa tabaka la ukosefu wa ajira, kupunguza ushiriki wa vijana wa Libya katika kujenga na kuendeleza nchi yao na kutunga maamuzi na kushiriki na kushirikia ndani yake .

Al-Saghir aliongeza, kwa kusisitiza kuwa kampeni hiyo inaangazia  kundi hili ambapo idadi kubwa ya vijana wanaoshiriki  miongoni mwa timu hiyo ambayo waliochaguliwa kuwa waandalizi na waratibu wa kazi za kampeni hiyo ambao wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 30, miongoni mwao ni mhandisi "Essam Fathi", ambaye anaona   kwamba jukumu la vijana huko Sirte ni muhimu ambapo  mji ambao vijana walishiriki kila wakati ili kuurudisha uhai, haswa baada ya Prof. Dkt. Mukhtar Khalifa Al -Maadani, Mkuu wa Manispaa ya Sirte na profesa wa zamani wa Chuo Kikuu cha Sirte, alishika usimamizi wa manispaa na alichaguliwa kuwa Mkuu tangu miaka iliyopita.


 
Ambapo inapaswa kuzingatiwa kuwa Meya wa Sirte ni mtu wa kutia moyo, haswa katika mawazo ya kiraia yanayofanya kazi kuamsha jukumu la kijamii mjini , alichangia kwa jukumu lake katika kuwahimiza vijana Al sertawi na kuwaunga mkono pamoja na kuanzisha ushirikiano nao na taasisi za jamii ya kiraia ikiwemo mashirika na vyama vya misaada na kiraia vyenginevyo .

Al-Saghir aliongeza  akiashiria kwamba kampeni itaendelea hadi katikati ya  mwezi wa Septemba, kwa ushirikiano na taasisi kadhaa, ikiwa ni pamoja na "Afaaq Al-Dhawar", timu ya "Wezi wa Nuru", timu ya "Teknolojia", na taasisi ya "Fanar". juhudi hizo zilikuja kuandamana na maombi yetu kama Balozi wa Udhamini wa Nasser huo ambao tulitambua  Uzoefu imara wa kimisri kupitia kwake  katika jamii ya kiraia, na idadi kubwa ya viongozi wa kazi ya kiraia katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, pamoja na mafunzo mbalimbali ambayo Udhamini wa  Nasser uliyachangia kiwemo kuboresha uzoefu , kukuza mitazamo ya kiraia, na kuchanganya kati ya programu za kupunguza ukali wa migogoro na kuimarisha mshikamano wa familia , akiashiria kwamba Udhamini wa Nasser ndio msukumo wa kimsingi kwa miradi mikubwa hiyo, ambayo ina umuhimu mkubwa zaidi kuliko  kuwa  tu kampeni ya kusafisha na kujenga upya .

vilevile , Al-Saghir  alisifu  mpangilio mzuri  na wa kipekee wa  wajitolea na timu na taasisi zilizoshiriki, kwani wao japo ukosefu wa kulitangaza vizuri tukio   ila walijaribu kuhifadhi kila kitu kwa muda wake kupitia kamera ya simu ya kibinafsi na hivyo kwa sababu ya ukosefu wa  vifaa vinavyotumika katika  kuhifadhi .

Al-Saghir alihitimisha katika taarifa  maalum  kwa tovuti ya  Harakati ya Nasser  kwa vijana  akisema: " wenzangu, jamaa, marafiki, majirani na watu wa Sirte kwa ujumla walishiriki nami  tumaini hili la  kurudisha maeneo haya ya kijani kwa asili yao ili kufaidisha mji kama yalivyokuwa, basi jukumu kuu la rafiki yangu Zakaria al-Faqihi lilikuwa jukumu muhimu zaidi katika kuunda wazo na kuligeuza kuwa mradi maalum ambao ulibadilisha mahitaji mengi na machafuko ya idadi na mawazo kuwa mradi uliopangwa kwa kulingana na miradi ya kazi za umma iliyoidhinishwa kimataifa, ambalo lilichangia kuwasukuma  wafadhili wanaounga mkono mradi katika awamu zake zote ,  mipango ya  mikakati na mipangilio ya kiutendaji ulioweka, licha ya msingi wa mradi na  lengo lake ndani ya mfumo wa kanuni za jumla za kazi ya kiraia na katika upatanishi wa kina na vigezo vya Harakati ya Nasser kwa Vijana inayolenga kuimarisha amani ya kijamii na kimataifa  ambapo shughuli kama hizo huongeza upendo, huchangia kutoa nafasi ya kiraia kwa ajili ya kufahamiana na kushikamana na kupunguza  ukali  wa mvutano, na zinaunda kutokana na jukumu lake , maoni  mpya ya umma unaokaribisha kuishi kwa amani, kupinga  ugomvi na migawanyiko, na kuchangia kugeuza mazingira kuwa bora.