Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa aelezea uzoefu wake katika mkutano wa Baraza la Kitaifa la Vijana nchini Gambia

Lisa Scat, Mhitimu wa kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa alishiriki katika mkutano wa robo mwaka wa Baraza la Kitaifa la Vijana nchini Gambia, ambapo washiriki walijadili ripoti zilizowasilishwa na viongozi  vijana wa kikanda kuhusu masuala ya vijana ya kitaifa.

Wakati wa mkutano huo, Lisa alionesha uzoefu wake nchini Misri wakati wa ushiriki wake katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, wakati wa hotuba yake, pia aligusia Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na jinsi vijana waafrika wanaweza kunufaika nayo.

Mwishoni mwa hotuba yake, Lisa alijadili ziara zake katika maeneo ya kiakiolojia ya Misri na miji ya Aleskandaria na Ismailia, ambayo ilikuwa miongoni mwa shughuli za Udhamini.

Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri ilikuwa imehitimisha shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa kushirikisha viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote  na nchi rafiki, mnamo kipindi cha kuanzia Mei 31 hadi Juni 17 iliyopita, katika Jumba la Mamlaka ya Uhandisi mjini Kairo.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa Misri katika kuunganisha na kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kuunda kizazi cha viongozi wa vijana kutoka nchi zisizofungamana na maoni sambamba na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la Jumuiya Zisizofungamana kwa upande wowote kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la mtandao wa vijana wa nchi wanachama wa Jumuiya ya NYM, na kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa katika ngazi ya nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki.

Pamoja na kutoa fursa sawa kwa jinsia zote, kama ilivyoainishwa na lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, vijana pia wanapewa fursa ya kujumuika na kufanya mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu Barani, bali pia kimataifa, kama inavyoonyeshwa na lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu.