«Ghazaly» Mzungumzaji wa Mfumo wa kwanza wa Uigaji wa Bunge la Afrika
Mfumo wa Uigaji wa Bunge la Afrika, Mei huu 2022, ulimkaribisha "Hassan Ghazaly" Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, kama Mzungumzaji wa kikao cha mjadala, kikiwa na kichwa «Mifano ya Vijana katika Shughuli za umma», katika toleo lake la kwanza, linaloandaliwa na Kitivo cha Mafunzo ya Afrika , Chuo Kikuu cha Kairo, pamoja na ushiriki wa vijana viongozi 120, wakiwakilisha nchi takribani 24 za kiafrika, ambapo shughuli zake zilikuwa pamoja na mihadhara kadhaa na warsha za maendeleo ya elimu na ujuzi wa vitendo kwa vijana washiriki, ambapo Mfumo huo unazingatiwa kama Uigaji kikweli wa Pan-African Bunge, ambalo nguzo ya kisheria ya Umoja wa Afrika.
Katika muktadha huo, mnamo kipindi cha kuanzia 17 kwa 19 Mei, Mfumo huo wa Uigaji wa Bunge la Afrika umezungumzia Agenda 2063, kama mkakati wa maendeleo ya Bara, pamoja na kujadili dhana ya Usalama wa kitaifa wa Afrika na changamoto zake, kwa mujibu wa mwelekeo na jukumu la Misri Barani, na hivyo ni kutokana na uangalizi wa Chuo Kikuu kwa suala la Afrika, yakiwa na Usimamizi wa Dkt. Gamal El Shazly, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu kwa Masuala ya Elimu na wanafunzi, pamoja na Kuonesha tajriba kadhaa za vijana waafrika wanaoshughulikia Kazi ya Bunge na shughuli za umma.
Kwa upande wake, "Hassan Ghazaly" Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana wakati wa hotuba yake, alitoa majaribio yake kadhaa ya ndani katika nyanja za maendeleo, akielezea umuhimu wa uwezeshaji wa vijana kupitia miradi kadhaa ya ndani, kikanda, bara na kimataifa, ikiwemo Mradi wa Mbegu, Shule ya kiafrika ya majira ya joto , mpango Afromedia, pamoja na mradi na Umoja wa Bonde la Nile .. Maoni ya Baadaye, Hatimaye Udhamini na Harakati ya Nasser ya kimataifa kwa Vijana,ambapo anafurahi kuzindua toleo lake la tatu, mnamo Juni ijayo, kwa kushirikiana na viongozi vijana kutoka nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, akielezea mifano halisi katika kazi za ndani, kufikia Raia wa Ulimwengu mzima.