Mapambano ya Algeria Sio Mapambano ya Algeria Tu... Lakini Ni Mapambano ya Waarabu wote

Imetafsiriwa na/ Ahmed Salama
Imehaririwa na/ Nourhan khaled
Nyini Wananchi wenzangu:
Mkutano huu unaofanywa na Umoja wa Kitaifa ... Mkutano huu ni ishara ya msaada wa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu kwa raia wa Algeria katika mapambano yao ili kupata uhuru, msaada huu unaendelea hadi watu wa Algeria wanapata uhuru wao. Msaada huu uliotangazwa kwa niaba ya watu wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu hautakomesha; ni msaada wa kila kitu tunachomiliki na msaada wetu hauwezi kuwa upande wa kiroho tu, kama ilivyotakia nchi za ukoloni; kwa sababu ya mapambano ya Algeria ni mapambano ya watu wote wa Kiarabu katika kila nchi miongoni mwa nchi zake.
Mapambano ya Algeria sio mapambano ya Algeria tu , bali ni mapambano ya Waarabu wote. Matukio yanathibitisha kuwa mapambano haya ni sehemu ya mpango ulioundwa na ukoloni kumalisha taifa la Kiarabu, na huo haukuwa mpango mpya, ilihali ni mpango uliowekwa wakati wa nyuma.
Katika karne ya 13 kulikuwa na kampeni za ukoloni za msalaba dhidi ya Syria, Palestina, Misri, na Morocco. Wafalme wote wa Ulaya walikusanyika katika kampeni hizo lengo lao lilikuwa kuwa chini ya jamii ya Kiarabu, na lengo lao pia lilikuwa kuondoa taifa la Kiarabu. Je! Matokeo yalikuwa nini?
Watu hawa wa kiarabu walipigana peke yake, na kushikamana kwa imani, na kwa Umoja wa Kitaifa na Umoja wa Kiarabu; walifanikiwa kuangamiza kampenj za ukoloni za msalaba, walifanikiwa kuvunja wafalme wa Uingereza na wafalme wa Ufaransa, na walifanikiwa kuondoa uvamizi wa ukoloni wa msalaba katika ardhi ya Waarabu. Hii ilikuwa zamani ... katika siku hizi, "Louis IX" alielekea nchini Misri kwa msalaba, lakini "Louis IX" alishindwa huko Misri na akakamatwa huko Misri, na jeshi lake likapigwa huko Misri, kisha akaenda Morocco baada ya kulipa fidia ili kupata uhuru, akenda kutawala Morocco ya Kiarabu lakini akashindwa huko pia.
Na huko nchini Syria na Palestina, majeshi ya Ulaya yaliungana chini ya jina la kampeni za msalaba ili kuangamiza utaifa wa Kiarabu, na majeshi haya yalikamata Palestina, na wakakamata Yerusalemu na wakajenga ngome katika Syria, na wakaamini kwamba kwa hivyo waliangamiza utaifa wa Kiarabu na wakaweka makao makuu ya kudumu kwa ukoloni, basi nini kilikuwa matokeo? Umoja ulianzishwa kati ya Misri na Syria kukabiliana na hatari ya kudumu, majeshi ya Kiarabu na watu wa Kiarabu waliungana; kwa sababu waliamini kuwa umoja wao ndio njia ya nguvu zao na pia njia ya uhuru wao. Nini kilikuwa matokeo?
Baada ya miaka 80 ya kukamata Yerusalemu ..
Baada ya miaka 80 ya kukamata Palestina, je! Watu wa Kiarabu walizisahau ardhi zao? Je! Watu wa Kiarabu walizisahau haki zao? Je! Watu wa Kiarabu walizisahau ukoloni ambao ulijenga ngome katika nchi yao? Je! Watu wa Kiarabu walizisahau kuwa lazima wajitolee uhuru wao kwa damu yao? Hawakusahau kamwe baada ya miaka 80 ardhi yao na haki zao, hawakusahau haki yao ya kulipiza kisasi na hawakusahau haki yao ya kusafisha nchi yao kutoka kwa uovu wa ukoloni.
Baada ya miaka 80 ya uvamizi wa Magharibi uliofanywa na kampeni za msalaba za ukoloni, watu wa Kiarabu walifanikiwa kusafisha Palestina na kurudisha Yerusalemu na kurudisha Palestina kuwa Kiarabu; kwa sababu waliamini Mola wao, na walijiamini, na waliamini haki yao karika kupata uhuru na maisha, na waliamini kuwa umoja ndio njia ya nguvu na njia ya maisha. Hii – Enyi ndugu zangu - ilikuwa historia yetu katika wakati wetu nyuma.
Je! kampeni za msalaba ambayo zilielekea kwenye Magharibi ya Kiarabu na Mashariki ya kiarabu imekwisha? Halafu je! Uzoefu wa ukoloni wa kuangamiza utaifa wa Kiarabu limekwisha? Haikwisha kamwe; bali iliendelea miaka baada ya miaka na siku baada ya siku na wakati ulipita, na tulikabiliana mara nyingi na kampeni tofauti za ukoloni; tulikabiliana hapa nchini Misri, na uvamizi wa Ufaransa katika siku za "Napoleon", na Palestina pia ilikabiliana na uvamizi wa Ufaransa katika siku za "Napoleon", na Syria pia ilikabiliana na uvamizi wa Ufaransa katika siku za "Napoleon", lakini watu wa Kiarabu nchini Misri na Palestina. Na Syria alisimama - akiwa ni watu hawakuwa na silaha - kukabiliana na "Napoleon" waliyeshinda juu ya wafalme wa Ulaya, na watu wa Kiarabu walifanikiwa kushinda kampeni ya "Napoleon", na kulazimisha "Napoleon" kurudi nyuma kutoka nchi yake. Na kutoka ardhini kwake, akamlazimisha akimbie kutoka ardhini kwake. Na kutoka nchi yake, ardhi nzuri, ardhi huru ikarudi kwa watoto wake Waarabu huru, Palestina ikawa huru, Syria ikawa huru, Misri ikawa huru, basi je! Hii ilimaliza kampeni za ukoloni ambazo zililenga kuangamiza utaifa wa Kiarabu? Hazikwisha.
Baada ya hii tulikabiliana na uvamizi wa Uingereza, mnamo mwaka 1801, na mnamo mwaka 1807, nchi ya Uingereza ulioshambulia Misri kuitawala; basi nini kilikuwa matokeo? Meli za Uingereza mnamo mwaka 1801, na meli na majeshi ya Uingereza mnamo mwaka 1807; haikuweza kusonga mbele katika kampeni yake, ilihali moto na uharibifu huko Alexandria , kisha ikachagua usalama baada ya kushindwa vibaya, na kurudi nyuma kwa nchi Uingereza, katika hali ya kukata tamaa na kushindwa. Na hii pia ilikuwa sababu moja ya sababu zilizosukuma umma wa Kiarabu kugusia hatari; kwa sababu baada ya hii tulikabiliana na kampeni ambazo tulikabiliana nazo zamani.
Mnamo mwaka 1830, Ufaransa ilikamata Magharibi ya Kiarabu na ilikuwa ikifuatilia njia ya kampeni za ukoloni za msalaba ambazo zilifuatilia katika karne ya 13 kisha baada ya hapo, mnamo mwaka 1882, Uingereza ilikamata Misri kwa udanganyifu, baada ya kushindwa kuendelea kutoka Alexandria hadi Cairo, na ikaingia kwa njia ya udanganyifu kupitia Mfereji wa Suez kwa njama na Wafaransa ambao walikuwa wakiendesha Mfereji wa Suez, na Uingereza iliikalia nchini Misri wakati huu, na Ufaransa ilikuwa inatamani Lebanon na Syria, na Uingereza ilikuwa inatamani kukamata sehemu zingine za ulimwengu wa Kiarabu.
Kisha mambo yaliendelea, na Uingereza iliweza kukamata Aden na vilevile maeneo yaliyohifadhiwa katika kusini mwa Rasi na Ghuba ya Kiarabu, lakini je! Hii ilikuwa uvamizi na je! Majeshi ya Uingereza yalikuwa na uwezo wa kuangamiza roho ya kupata uhuru na roho ya mapambano katika ulimwengu wa Kiarabu? Je! Uvamizi wa Ufaransa wa Algeria na Magharibi ya Kiarabu ulikuwa na uwezo wa kukomesha mambo ya mapambano katika nafsi ya watu wa Kiarabu katika MagharibiyaKiarabu? Au je! Uvamizi wa Italia kwa nchini Libya ulikuwa na uwezo wa kuangamiza roho ya mapambano huko nchini Libya?
Haiwezekani kamwe .. Nchi hizi ambazo zilikuwa na uwezo, na ambazo zilikuwa na silaha hazikuweza kuangamiza roho ya uhuru ya Kiarabu katika nchi yoyote ambayo wanajeshi wake walitembea ardhini kwake, au katika nchi yoyote ambayo walijenga ngome, au katika nchi yoyote ambayo walijenga silaha. Na walijenga majeshi ili kuangamiza roho yake ya kiarabu, na kuangamiza utaifa wake wa Kiarabu.
Kisha kulikuwa na Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, na kupitia Vita vya Kwanza vya Ulimwengu Uingereza na Ufaransa walifanyana njama, baada ya kufanya makubaliano kati yao kwamba wangeigawanya ulimwengu wa Kiarabu kuwa maeneo yenye utawala kwao.
Katika siku hizi pia, walifanyana njama dhidi ya umma wa Kiarabu ili kuangamiza utaifa wa Kiarabu, na njama kubwa ililenga Palestina. Katika siku kama hizi mnamo mwaka 1917, mnamo 2 Novemba mwaka 1917, “Balfour” alitangaza ahadi ya kuanzisha Nchi ya kitaifa kwa Wayahudi huko nchini Palestina,Hii ilikuwa mwanzo wa vita kubwa kwa ajili ya uhuru wa Kiarabu na utaifa wa Kiarabu na kwa ajili ya heshima ya Kiarabu na ubinadamu wa Kiarabu.
Na mipango ya ukoloni iliendana na Uzayuni wa kimataifa ili kuondoa utaifa wa Kiarabu huko Palestina, na kuanzisha taifa la Kizayuni huko, na mipango ya ukoloni iliendelea hadi ilifanikiwa kukalia ardhi na kuua wanaume, wanawake na hata watoto, lakini je, walifanikiwa kuua roho ambazo zimeazimia kupigana kwa ajili ya ukombozi wa Palestina? Je, walifanikiwa kuondoa roho ya Kiarabu ambayo inachukulia Palestina kuwa ardhi ya Kiarabu? Je, walifanikiwa kuondoa azma ya umma wa Kiarabu wote kurejesha Palestina? Katika karne ya 13, walijaribu kwa njia zote kuondoa roho hii, lakini watu wa Kiarabu waliendelea katika mapambano yao na harakati zao kwa muda wa miaka 80 hadi walirejesha ardhi ya Palestina.
Na leo nahisi kwa kina, kutoka roho yangu, kwamba watu wa Kiarabu ni wenye azma zaidi na azimia kuliko walivyokuwa zamani kwenda njia yao ili kulinda utaifa wao, kwa sababu heshima ya umma wa Kiarabu haiwezi kugawanyika, na heshima ya Palestina ni heshima ya Jamhuri ya Kiarabu iliyoungana, na heshima ya Algeria ni Heshima ya Jamhuri ya Kiarabu iliyoungana.
Sisi - enyi ndugu na raia tunapounga mkono watu wa Algeria, wakati huohuo tunaunga mkono suala la utaifa wa Kiarabu katika kila nchi ya Kiarabu, na tunaunga mkono suala la raia wa Palestina, na pia tunaunga mkono suala letu kwa ajili ya kupata uhuru, na kwa ajili ya kuimarisha kupata uhuru.
Enyi ndugu tunakumbuka , mnamo mwaka 1956 jinsi Ufaransa ilivyotangaza kwamba uvamizi dhidi ya Misri ulikuwa sehemu ya vita vyake dhidi ya harakati za ukombozi huko nchini Algeria, na waliamini kwamba ikiwa wangeweza kudhibiti nchini Misri, basi wangeweza kuzima moto wa uhuru wa Kiarabu na moto wa utaifa wa Kiarabu, na walisahau wakati huu kwamba moto wa uhuru wa Kiarabu na moto wa utaifa wa Kiarabu hauwezi kuzimika. Hawakuweza kuizima katika zamani katika miaka iliyopita, lakini katika karne zilizopita; katika karne 12, 13, 17, 19, na 20 walipoweza kuwa na silaha za uharibifu, na walipoweza kuwanyima umma wa Kiarabu kuwa na silaha za kutetea wenyewe, je! Silaha hizi ziliwawezesha kuondoa roho ya utaifa wa Kiarabu na roho ya uhuru na roho ya uhuru? Hawakuweza kamwe katika zamani wala hawataweza kamwe katika sasa au katika siku zijazo.
Katika mwaka 1956, ilikuwa tahadhari ya Uingereza- Ufaransa katika siku kama hizi, na sisi tulikuwa watu wadogo .. watu wasio na silaha waliokabiliana na nchi kubwa; kukabiliana na Uingereza na Ufaransa na meli za Uingereza na Ufaransa na nyuma yao Jumuiya ya Atlantiki, tulikabili tahadhari na hatukuwa na silaha ambazo zinaweza kutuwezesha kukabiliana na nchi kubwa; Uingereza na Ufaransa, lakini tulikuwa na imani kwa Mungu, na imani kwa nchi, na imani kwa haki yetu ya uhuru na haki yetu ya maisha, na kulikuwa na mawakala wa ukoloni waliofanya njama na ukoloni dhidi ya uhuru wetu na hatima yetu kwa bei rahisi, kama walivyofanya njama kabla ya hii katika vita vya Palestina, na ukoloni uliamini kwamba mawakala hawa ni nguzo yake kubwa katika vita yake ili kuondoa utaifa wa Kiarabu na kuondoa roho ya Kiarabu, lakini je! Ukoloni ulifanikiwa? Ukoloni haukufanikiwa, na akarudi akivuta mikia ya kukatishwa tamaa na kushindwa kama alivyovuta mikia ya kukatishwa tamaa na kushindwa katika karne ya 12, na katika karne ya 19.
Enyi ndugu - macho haya kutoka historia yetu inaonesha tu kwamba vita vya Waarabu katika sehemu yoyote ya nchi za umma wa Kiarabu ni vita moja inayoendelea, na inaonyesha tu kwamba njama za ukoloni na mipango ya ukoloni katika sehemu yoyote ya umma wa Kiarabu ni vita inayoendelea ili kuondoa utaifa wa Kiarabu, na kuondoa roho ya Kiarabu, na kuondoa motisha ambazo zinaundwa katika nafsi zetu kwamba tunajenga nchi yenye nguvu, yenye heshima, yenye kiburi; tunaijenga kwa maendeleo na viwanda na kazi inayoendelea ambayo ukoloni ulituzuia katika zamani kutoka kwenda.
Ukoloni unaamini kwamba umma wa Kiarabu utapata uhuru, basi utaenda njia yake yenye nguvu iliyokusudiwa kujiendeleza ili ichukue nafasi yake kwa namna imara sana, umma wenye nguvu, umma ambao kiwango chake cha maisha kinapanda; Na hivyo hakuna ukiritimba wa nguvu kwa ukoloni, wala hakuna ukiritimba wa nguvu kwa kikundi kidogo cha watu ambacho kilipendelea kutumia nguvu kuwanyenyekea watu wengine wa dunia.
Na sisi – enyi ndugu na raia - leo tunapoangaliq magharibi .. kwenda Algeria, na watu wa Algeria wanapokea mwaka wa saba wa mapinduzi yao; tunamshukuru Mungu ambaye aliwawezesha watu wa Algeria kuwa wavumilivu na wenye bidii na kupigana miaka 6 bila udhaifu au uchovu, na kuendelea njia yao kukabiliana na Ufaransa kwa vikosi vyake, kukabiliana zaidi ya 800 elfu askari kutoka vikosi vya Ufaransa kwa vikosi vyake vidogo. silaha ndogo, basi upeleke Ufaransa na majeshi yake, basi upeleke Ufaransa na silaha za Jumuiya ya Atlantiki ambazo hutegemea, basi upeleke pia nchi ambazo zinasema kuwa zinawakilisha ulimwengu huru katika karne ya 20. Ulimwengu huru uko wapi? Na wapi uhuru ambao wanajisifu nao?
Hatuuoni uhuru huu, hatuuoni isipokuwa uhuru wa kuua, na uhuru wa uharibifu, na uhuru wa utumwa, wanatangaza kwamba wanawakilisha ulimwengu huru ili wadanganye mataifa yaliyoshindwa juu yao wenyewe, na sisi ni watu wanaopigania, sisi ni watu wanaopigana kwa ajili ya uhuru wetu na kuthibitisha uhuru wetu na kwa ajili ya uhuru wetu na kuthibitisha uhuru wetu tunaelewa kuwa hizi ni kauli mbiu za uwongo, ikiwa ulimwengu huru ni ulimwengu huru kweli basi kwanini unapeleka Ufaransa silaha na pesa ili iue watoto wa Algeria, na iikalie Algeria, na iivamie uhuru wa watu wa Algeria, na kuwazuia watu wa Algeria kuwa watu huru na huru?
Ulimwengu huru unaozungumziwa ni adui wa uhuru na adui wa uhuru; hii ndio tunayoiona huko Algeria, na hii ndio tuliyogusa huko Algeria. Damu ya milioni moja ya Algeria haishuki tu kwenye bega la Ufaransa. Milioni hii ambayo ilishuhudia huko Algeria, ilishuhudia kwa sababu ya vikosi vya Ufaransa, na kwa sababu ya silaha za Ufaransa, lakini pia ilishuhudia kwa sababu ya silaha ambazo nchi za Magharibi ziliipeleka Ufaransa, na kwa sababu ya pesa ambazo nchi za Magharibi ziliisaidia Ufaransa. Mzigo katika hii haushuki tu kwa Ufaransa, lakini pia unashuka kwenye nchi hizi ambazo zinasaidia Ufaransa kuua watu wa Algeria, na kuifuta watu wa Algeria. Bila msaada wa nchi hizi kwa Ufaransa haiwezekani kwa Ufaransa chini ya hali yoyote kuendelea katika vita yake.
Ufaransa hutumia milioni mbili za pauni kila siku katika vita vyake huko Algeria, kutoka wapi Ufaransa inapata pesa hizi? Kutoka nchi za ulimwengu huru .. ulimwengu huru ambao unasaidia mauaji, na unasaidia mauaji, na unasaidia uhamishaji, na unasaidia uharibifu wa vijiji,،Na wanachangia katika kuangamiza watu huko Algeria kama walivyochangia katika kuangamiza watu wa Palestina.
Sote tunajua jinsi watu wa ulimwengu huru walivyochangia katika kuangamiza watu wa Palestina baada ya kutoka washindi kutoka Vita vya Pili vya Ulimwengu, jinsi walivyochangia kwa silaha, jinsi walivyochangia kwa pesa, jinsi walivyochangia kwa msaada wa nyenzo na msaada wa maadili, jinsi walivyochangia kwa kuruhusu Israeli kupata aina zote za silaha, na kuzuia Waarabu kupata aina zote za silaha.
Mzigo huko Palestina unashuka kwa Uzayuni na pia unashuka kwa nchi za ukoloni, nchi hizi ambazo zinatangaza kauli mbiu kuwa ni ulimwengu huru, na uhuru kutoka kwao ni safi; waliua watu wa Palestina, au waliamini kwamba waliua watu wa Palestina, na kwamba pesa zao na uwezo wao wa nyenzo utawawezesha kufikia lengo lao, na wanaamini kwamba uwezo wao wa nyenzo utawawezesha huko Algeria kuondoa roho ya watu wa Algeria na mapenzi ya watu wa Algeria kupata uhuru na uhuru, lakini hii haiwezekani; roho ya Kiarabu haiwezi kuzimika chini ya hali yoyote, roho ya Kiarabu ambayo ilipigana na ikashuhudia zamani iko tayari katika sasa na baadaye kupigana na kushuhudia.
Katika mwaka 56 waliamini kwamba kwa vikosi vyao na meli zao wangeweza kuwatisha watu wa Misri na watu wa Kiarabu katika kila nchi ya Kiarabu, na kampeni ya uvamizi ilianza, na wakatoa tahadhari yao, halafu wakafanya mashambulio yao juu ya Cairo na miji ya Jamhuri, halafu wakati huo huo wakafanya njama yao huko Syria wakitegemea mawakala wa ukoloni, halafu kampeni kubwa ilianza .. kampeni kubwa ya uchokozi dhidi ya Misri, ambayo Uingereza, Ufaransa na Israeli wanashiriki. Je! Walifanikiwa kuondoa roho ya utaifa wa Kiarabu na roho ya uhuru na uhuru?
Watu walitoka nchini Misri na katika kila nchi ya Kiarabu wakipiga kelele .. tutapigana kwa ajili ya uhuru wetu, na kwa ajili ya uhuru wetu, na tutapigana kwa ajili ya heshima yetu na kwa ajili ya heshima yetu, na kwa ajili ya watoto wetu. Hii ilikuwa kilio kilichotolewa mahali popote, na hii ilikuwa kilio kilichotolewa katika kila nchi ya Kiarabu, ilikuwa - ndugu - ni kilio chetu mwaka 56 na pia ni kilio chetu leo.
Tunapotazama watu wa Algeria na tunaona milioni moja ya watoto wa watu wa Algeria wameshuhudia katika njia ya haki na katika njia ya uhuru; hatutiririkwi machozi juu yao lakini tunajisikia fahari kwamba kuna .. kuna watu wa Algeria ambao wamenunua maisha kwa mauti, na azimio lao halikulegea lakini waliamua kununua uhuru wao kwa mauti.
Na sisi – enyi ndugu na raia - tunapotazama mashariki na tunatazama Palestina, na tunatazama njama za ukoloni katika eneo hili la ulimwengu wa Kiarabu; matukio hayatutishi wala njama ambazo ziliwezesha Uzayuni kutoka Palestina mwaka 48, wala njama za ukoloni na Uzayuni, wala njama za mawakala wa ukoloni na Uzayuni; kwa sababu tunajua kwamba watu wa Kiarabu katika Mashariki pia wamenunua maisha kwa mauti, na wamependelea kujitoa kwa nafsi zao na roho zao na damu yao katika njia ya uhuru wa nchi yao, na katika njia ya uhuru wa nchi yao, na katika njia ya kuthibitisha uhuru huu. Sio hivyo tu; lakini pia walipendelea kujitoa kwa roho zao na uhuru wao na damu yao katika njia ya heshima yao, na katika njia ya heshima ya nchi yao. Na tunatazama Mashariki ya Kiarabu na tunakumbuka mfano wa karibu; mfano wa Adnan Madani alipokataa kununua maisha kwa kusaliti nchi yake, au kusaliti heshima ya nchi yake, lakini alinunua maisha kwa mauti akawa miongoni mwa wenye umri wa milele.
Hii - ndugu na raia - ni vita vyetu katika kila nchi ya Kiarabu .. Hii - ndugu na raia - ni roho ya Kiarabu .. Hii - ndugu na raia - ni roho ya mapambano ya Kiarabu.
Tumejitolea wenyewe na tumeahidi Mungu kuwa tutanunua maisha kwa mauti; ili nchi zetu ziwe zenye heshima, huru, zenye heshima. Na Mungu atawafanikisha.
Waalsalmu Alaikum warahmat Allah.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika sherehe ya Umoja wa Taifa siku ya Algeria kutoka Chuo Kikuu cha Cairo. Tarehe 1, Novemba 1960.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy